Mwakinyo athibitisha ubora wake. Amchapa Mjeda wa Ghana raundi ya saba

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Bondia Hassan Mwakinyo wa Tanzania athibitisha ubora wake baada ya kumchapa Mjeda wa Ghana raundi ya saba katika pambano la ubingwa wa WBO.
---
Bondia Hassan Mwakinyo ameshinda pambano usiku huu kwa kumpiga Bondia wa Ghana Elvis kwa KO katika round ya 7 ya pambano hilo la kuwania ubingwa wa WBO Africa ambalo limepigwa New Amaan Complex Zanzibar.

---

Bondia Hassan Mwakinyo baada ya kumpiga Bondi wa Ghana Elvis kwa KO katika raundi ya 7 amewashukuru Waandaji wa pambano hilo kwa kumpa fursa ya kuwaonesha Mashabiki kuwa yeye ni Mpiganaji wa aina huku akisema anaamini kufa kwa Imam sio mwisho wa kufanya Ibada hivyo hata wakati ambao alikuwa hapati nafasi haikumvunja moyo.

Mwakinyo amenukuliwa akisema “Namshukuru Mungu pia Waandaaji wa pambano kwa kunipa nafasi ya kuonesha Mashabiki zangu kuwa Mimi ni Mpiganaji wa aina gani, mara zote nimekuwa nikiamini kwamba kufa kwa Imam sio mwisho wa kufanya Ibada, akifa Imam inabidi utafute Imam mwingine Ibada ziendelee”

“Hata wakati ambao nilikuwa sipati nafasi ilikuwa hainivunji moyo nilikuwa naamini ipo siku nitapata nafasi ambayo inastahili sawa na heshima yangu, nawashukuru Mashabiki zangu kwakuwa wamenivumilia muda mrefu
 
Kawanunue na wewe, yaani bondia anawania mkanda anunuliwe kwa nauli na chakula, zinakutosha kweli? Au hujui hata mambo ya boxing yalivyo?
Wewe ndio hujui boxing na humjui Mwakinyo.

Mmwakinyo aligoma kupanda ulingoni baada ya kuletewa bondia ambae hamjui ingawa huyo bondia ana hadhi kubwa kuliko Mwakinyo. Mwakinyo alitaka aletewe bondia ambae yeye alishamuandaa hadi bei amekubaliana nae, promota akakataa, mwakinyo akakimbia ulingo.

Mwakinyo sio bondia.
 
Sasa Julius Indongo mbona alishapigana na Mwakinyo na akapigwa tena kwa TKO iweje tena useme alikataa kupigana nae kwa mara ya pili kisa hamjui?
Huyo Indongo toka Namibia hata Jana tu alikuwa na pambano Tanga na amepigwa kwa TKO na bondia wa kawaida tu
Screenshot_20240128-104425_Chrome.jpg
 
Ukweli usemwe huyu dogo Mwakinyo uwezo anao,pia ana misimamo,hayumbishwi.
Kubwa zaidi anaijua biashara yake ya ngumi atafanikiwa zaidi na zaidi.

Mungu amtangulie kwenye kazi zake inshaallah.
 
Wewe ndio hujui boxing na humjui Mwakinyo.

Mmwakinyo aligoma kupanda ulingoni baada ya kuletewa bondia ambae hamjui ingawa huyo bondia ana hadhi kubwa kuliko Mwakinyo. Mwakinyo alitaka aletewe bondia ambae yeye alishamuandaa hadi bei amekubaliana nae, promota akakataa, mwakinyo akakimbia ulingo.

Mwakinyo sio bondia.
Una matatizo Kapimwe.

Nakushauri siku zingi usiwe unasema vitu usivyovijua unadhalilishia ukoo wako.
 
Ukweli usemwe huyu dogo Mwakinyo uwezo anao,pia ana misimamo,hayumbishwi.
Kubwa zaidi anaijua biashara yake ya ngumi atafanikiwa zaidi na zaidi.

Mungu amtangulie kwenye kazi zake inshaallah.
Wapigaji matapeli mapromota wamemshindwa.
 
Wewe ndio hujui boxing na humjui Mwakinyo.

Mmwakinyo aligoma kupanda ulingoni baada ya kuletewa bondia ambae hamjui ingawa huyo bondia ana hadhi kubwa kuliko Mwakinyo. Mwakinyo alitaka aletewe bondia ambae yeye alishamuandaa hadi bei amekubaliana nae, promota akakataa, mwakinyo akakimbia ulingo.

Mwakinyo sio bondia.
Julius Indongo ana hadhi ya juu kuliko mwakinyo?
Si alishadundwa hapa na mwakinyo.
 
Back
Top Bottom