Matumla apigwa

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,963
3,805
Mbwana Matumla Adundwa kwa Knockout Philippines
2011870.jpg

Sunday, May 17, 2009 4:30 AM
Mbwana Matumla 'Golden Boy' usiku wa kuamkia leo ameshindwa kuwika nchini Philippines mbele ya bondia wao AJ 'Bazooka' Banal baada ya kupewa makonde mazito yaliyomfanya aliage pambano hilo kwa Knockout katika raundi ya pili. Kabla ya pambano hilo Matumla alikuwa gumzo nchini philipines kutokana na historia yake nzuri katika ndondi akionekana ni tishio kubwa kwa bondia huyo wa Philipines.

Katika pambano hilo lililofanyika kwenye mji wa Cebu nchini Philippines, AJ Banal au maarufu kama "Bazooka" alilitawala pambano hilo akimpa makonde Matumla kuanzia dakika ya kwanza ya mpambano huo.

Matumla ambaye alionekana dhahiri kuelemewa na mfilipino huyo katika raundi ya pili, ilimbidi aliage pambano hilo katika raundi hiyo baada ya kupewa makonde mawili mazito yaliyomdondosha chari kwa nyuma.

Matumla alijaribu kuamka bila mafanikio na refa wa pambano hilo alilimaliza pambano hilo katika raundi ya pili dakika ya 2:59.

Banal kwa ushindi wake dhidi ya Matumla, amefanikiwa kupata nafasi ya kuzipiga kwenye usiku wa mpambano wa kukata na shoka kati ya Mmarekani Floyd Mayweather na Juan Manuel Marquez julai 18 jijini Las Vegas.

Katika mpambano mwingine wa leo mkenya Morris "Virus" Chule alitandikwa kwa pointi na mfilipino mwingine Czar Amonsot.
source nifahamishe.com
 
Matumla ambaye alionekana dhahiri kuelemewa na mfilipino huyo katika raundi ya pili, ilimbidi aliage pambano hilo katika raundi hiyo baada ya kupewa makonde mawili mazito yaliyomdondosha chari kwa nyuma.

Matumla alijaribu kuamka bila mafanikio na refa wa pambano hilo alilimaliza pambano hilo katika raundi ya pili dakika ya 2:59.

Mwosha huoshwa..!
Asitafutwe mchawi hapa, ni ngoma ilikuwa nzito kwa Matumla.

Ajiandae tu kwaajili ya mapambano mengine mbele ya safari, atashinda.
All in all , nampa pole.. ndo mchezo.
 
hayo ndo matatizo ya kumtumia baba yake kama coach mbadala ya kutafuta poffesionals
 
Hirizi alopewa na babake naona imeishiwa nguvu, pia uwezo wake umeisha sana kwanini asistaafu yule bondia wa Morogoro Cheka amemdunda mara nyingi sana!
 
Hirizi alopewa na babake naona imeishiwa nguvu, pia uwezo wake umeisha sana kwanini asistaafu yule bondia wa Morogoro Cheka amemdunda mara nyingi sana!

Masa, Mbwana hajawahi kupigana na Cheka, unamzungumzia kaka yake Rashid.
 
Hii familia naona sasa ni wakati wa kuacha ngumi siku hizi kila siku wanapigwa
 
Huo ndo utamu wa mashindano . Piga nikupige. Itabidi akajipange upya. Wahenga walisema, "asiyekubali kushindwa siyo mshindani"
 
Boxing kama michezo mingine ya kutumia nguvu inakwenda sana na umri...kwa sasa Mbwana Matumla ana kama 34/35 na ameshapigana sna anastahili kupumzika kwa heshima zote...wale wafilipino wapo fit sana kwa boxing ....nadhani hiv karibuni si mliona chamoto alichopewa Ricky Hatton na mfilipino yule PAciano.Tatizo la mastar wa bongo hawana kitu mbadala cha kufanya ndo maana wanaendelea kukomaa na game mpaka wafie kwenye ulingo au kwa maradhi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom