Matumizi ya usemi "kupata matokeo"

MGILEADI

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,621
1,543
Sina tatizo na mada ya ndugu mmoja aliyoileta humu hapa leo akitumia maneno hayo hapo juu. Ila naomba nitumie nafasi hii kuuliza kuwa haya matumizi ya maneno au usemi wa "kupata matokeo" pasipo kutumia pamoja na kisifa kwa mfano, mazuri, yanayofaa, mabaya, au yasiyopendeza ni sahihi kisarufi? Nimesikia sana usemi huu ukitumika kwenye kipindi cha michezo Redioni pale wanapohojiwa makocha, wachezaji ama maofisa wa timu za mpira. Hawamalizii usemi huo kwa kisifa husika. Tunatarajia kupata matokeo. Matokeo gani mbona hamsemi. Mazuri? Bora? Yanayofaa? Yanayoridhisha? Yatakayofurahisha wapenzi wa timu? Hawamalizii! Hebu nisaidieni jamani.
 
Back
Top Bottom