Matumizi ya usemi "Kupata matokeo"

Matumizi ya usemi "Kupata matokeo"

MGILEADI

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
1,621
Reaction score
1,545
Sina tatizo na mada ya ndugu mmoja aliyoileta humu hapa jana akitumia maneno hayo hapo juu. Ila naomba nitumie nafasi hii kuuliza kuwa haya matumizi ya maneno au usemi wa "kupata matokeo" pasipo kutumia pamoja na kisifa kwa mfano, mazuri, yanayofaa, mabaya, au yasiyopendeza ni sahihi kisarufi? Nimesikia sana usemi huu ukitumika kwenye kipindi cha michezo Redioni pale wanapohojiwa makocha, wachezaji ama maofisa wa timu za mpira. Hawamalizii usemi huo kwa kisifa husika. Tunatarajia kupata matokeo. Matokeo gani mbona hamsemi. Mazuri? Bora? Yanayofaa? Yanayoridhisha? Yatakayofurahisha wapenzi wa timu? Hawamalizii! Hebu nisaidieni jamani.
 
Kweli kabisa mkuu, hata Mimi hako kausemi huwa kananikera sana, kama unasema unatarajia kupata matokeo ni vizuri ukabainisha matokeo unayoyatarajia kama ni mabaya, mazuri, ya kuridhisha n.k
Kwa kuwa katika mchezo wowote lazima kuwe na matokeo, hivyo ni bora ukatupia hicho kisifa mwishoni kutuweka wazi.
 
Ukiona hivyo hawajiamini ndio maana wanashindwa kutoa jibu lilokamili,.wanabaki kutupa tungo zao tata zisizo na mashiko.
 
Kwanza mimi kwa ufupi huwa wananitia hasira sana.

Kwa wenzetu, uchambuzi wa mpira unafanywa na wakongwe ambao wamecheza ligi mbalimbali kwa mafanikio na kwa viwango vya juu kabisa.

Chukulia mf kama Sammy Kuffor, Ryan Giggs, Michael Owen,..........! Hawa watu wakichambua soka wanatoa uzoefu wao kutoka uwanjani na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Hawa ni wachezaji wastaafu. Hii pia ni pamoja na watangazaji wa soka kwenye TV na Radio, ni wazee wenye uzoefu wao!

Njoo kwetu sasa. Utakuta mtangazaji wa Radio au TV ana miaka 24, 25, 26! Kwa umri huo inawezekana hata Lunyamila, Nteze John, Chumila, Mohamed Hussein (machinga) amesimuliwa tu uwezo na uchezaji wao achilia mbali kina Sunday Manara.

Ukija kwa wachambuzi wa soka ktk Radio na TV za Tanzania, mtu pekee ninayemfahamu na kumuona akicheza mpira kwa kiwango cha juu ni Ally Mayay Tembele (naweza kusahihishwa).

Kwa hiyo kwa hali hii siyo ajabu kukutana na msemo maarufu 'kupata matokeo'! Labda wachangiaji tumesahau pia jinsi watangazaji wanavyochanganya lugha wakati wa kutangaza. Utasikia goli likifungwa, 'yeesssss, he has made it', 'ame switch kutoka flank ya kushoto kwenda kulia', 'amepiga square pass' na mbwembwe zingine nyingi tu! Sisi wa Tz akili zetu tunazijua sisi na zinatufaa wenyewe tu!
 
Asante mleta mada.

Hiyo kitu mie inanikera sana sana sana. Wanaharibu lugha taratibu.

Hasa hao wachambuzi uchwara huwa wananikera mnoo wanavyotumia hilo neno.

Mchezo wowote ule huleta matokeo. Ukifungwa umepata matokeo, ukifunga umepata matokeo. Ukitoka sare umepata matokeo.

Utangazaji unapoteza maadili kila kukicha. Unakuta mtu anatangaza mpira robo saa yote bila kusema matokeo ya muda huo.

Juzi Azam tv wakati mchezo umesimama wa Simba wakarudi studio...bila aibu score board yao ilikua inasoma bado 1-2 alafu ndio inasifiwa tv makini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom