Neno Mkuu limetumika na magwiji wa hoja ili kupoza mzuka.
Jf ya zamani ilikuwa uwanja wa hoja, unatoa hoja inajibiwa kwa hoja.
Sasa mjadala unakuwa mkali na hoja huwa za moto, likatumika neno Mkuu ili kujenga urafiki na mahaba na yule unayejadiliana naye ili kupunguza munkali.
Ni kama vile mawakili walivyochagua Kuitana 'Wakili msomi' wakiwa kwenye kurushiana vifungu vya sheria mahakamani.
Nia ni moja tu, kujenga undugu na urafiki na kupunguza uhasama unaotokana na vichapo vya hoja.