SoC02 Matumizi ya muda katika Elimu na jinsi ya kukuza kipato

Stories of Change - 2022 Competition

Jay48

New Member
Jul 18, 2022
1
1
UTANGULIZI;
Elimu ni ujuzi au maarifa ambayo mtu anayapata kwa kufundishwa kutoka kwa watu wengine.kuna njia au sehemu nyingi za kupata ujuzi au elimu kama vile darasani, au kwenye runinga au kwenye mikutano.

Katika sehemu hii ningependa kuzungumzia zaidi kuhusu elimu ya darasani ambayo huwa tunaipata shuleni, kwenye vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Kutokana na mfumo wa elimu katika nchi yetu huwa tunapata elimu kwa awamu tatu au nne, awamu ya kwanza ni kwaelimu ya shule ya msingi, awamu ya pili ni elimu ya sekondari na awamu ya tatu ni elimu ya chuo kikuu.

Katika muda wote huu wa kupata elimu hua kuna muda tunaupoteza pale unapotoka ngazi moja ya elimu kuelekea ngazi nyingine muda ambao ukiujumlisha nisawa na muda wa mwaka mmoja na miezi miwili (miezi 14) kama ifuatavyo Unahitimu darasa la saba mwezi wa tisa unajiunga na kidato cha kwanza mwezi wa kwanza hapa kuna wastani wa miezi mitatu upo tu nyumbani.

Pia unahitimu kidato cha nne mwezi wa kumi na moja (11) unajiunga na kidato cha tano mwezi wa sita (6) hapa kuna wastani wa miezi mitano hadi sita upo nyumbani umekaa.
Hivyo hivyo unahitimu kidato cha sita mwezi wa tano unajiunga na chuo mwezi wa kumi na moja hapa kuna wastani wa miezi minne au mitano upo tu nyumbani.

LENGO;
Kutokana na tatizo la ajira serikalini kijana ambae bado upo katika muda wa kuapata elimu nivyema ukafanya yafuatayo ilikuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kujiajili na kujipatia kipato

1. Ukiwa umehitimu kidato cha nne katika hichokipindi cha miezi mitano au sita unasubilia kwenda kidato cha tano nivyema ukatafakari kujifunza fani za muda mfupi ambazo mwenyewe binafsi utakua unazipenda mfano kuwa kinyozi, kusuka au mpishi na fani nyingine nyingi hii itakusaidia hata baada ya kuhitimu chuo kupata ajira za muda na kujipatia kipato.

2. Njia nyingine ni kutafuta ajira za muda mfupi kutoka kwenye mashirika au kampuni au kwawatu binafsi au pia kujiajili wewe mwenyewe binafsi hata kwa mtaji mdogo mfano kuuza matunda hii itakupatia uzoefu wa kujisimamia na elimu jinsi ya kuendesha biashara yako hivyo unaweza kuja kufanya biashara hata baada ya kumaliza chuo kwakua umeshapata uzoefu angalau kidogo.

3. Kwa kijana ambae yupo elimu ngazi ya sekondari au chuo nivyema ukatafuta kazi za muda (part time) hii itakusaidia kupata uzoefu wa kazi au kuwa na rasilimali watu kwa kujuana na watu mbalimbali na kukupatia kipato na kukuweka kwenye nafasi nzuri ya ajira hata baada ya kuhitimu shule au chuo

HITIMISHO
Vijana tuwe makini na matumizi ya muda hivyohivyo pia wazazi wapende kuwahimiza watoto (vijana) wao katika kujifunza fani katika kipindi ambacho wapo nyumbani wakiwa wanasubili kuendelea na masomo hii itawasaidia kuwapa mwanga vijana katika utafutaji na uwajibikaji

Pia itapunguza tatizo la vijana kuwa tegemzi mara baada ya kuhitu elimu zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom