Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,653
- 218,143
Miaka ya nyuma kidogo wakati wa Kugombea ubunge wa Africa Mashariki ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mh Mwakyembe alitoa hoja kwa Spika Anna Makinda kwamba wagombea watumie lugha ya kiingereza kuomba kura ili kupima uwezo wao wa lugha wasije wakaifedhehesha nchi kwenye mijadala ya bunge la africa Mashariki , Spika Makinda akakubali mwongozo wa Mwakyembe hatimaye wagombea wakaanza kuomba kura kwa lugha ya kiingereza , huku Le Mutuz Super brand mmoja wa wagombea wa ccm akiangukia pua .
Hapa ndipo ulipoibuka msemo maarufu wa " IAM SORRY , IAM GLAD " msemo uliotokana na mmoja wagombea kuomba kujitoa kwenye kinyang'anyiro , lakini miaka michache tu siku ya leo Mwakyembe huyohuyo safari hii akiwa waziri wa michezo anawataka washiriki wa Miss Tanzania kutumia kiswahili kujibu maswali akidai ni lugha inayotumika dunia nzima !
Je ameusahau mwongozo wake wa Bungeni ?
Kwetu Tandika Mwembeyanga kuna msemo maarufu kwamba UKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU .
Naomba kuwasilisha .