Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,777
Wadau, nimefanikiwa kupata waraka wa ndani ya CHADEMA kutoka katika chanzo changu ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Amini usiamini, wakati ofisi za CHADEMA zikiwa katika hali mbaya, Dr Slaa anatumia shilingi laki tatu (300,000) kwa ajili tu ya kununulia betri za Megaphone. Pia mdau wangu amenitonya kuwa Dr Slaa AMELAZIMISHA ziara hiyo iwe ndefu kwa lengo tu la kujiongezea posho. Hii hapa ni summary ya waraka huo.
Ziara ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK WILBROAD SLAA katika mikoa ya Singida, Shinyanga, Kigoma na Tabora ambayo ilitarajiwa kuanza tarehe 3 Desemba 2013 na kumalizika tarehe 23 Desemba 2013 inatarajiwa kugharibu shilingi Milioni 19,833,300/=. Gharama hizo ni pamoja na posho ya Dr Slaa (80,000 x siku 22 = TSH.1,760,000), posho kwa wana timu 7 (40,000 x siku 22 x watu 7 = TSH.6,160,000), mafuta kwa ajili ya magari 3 (lita 2071 x 2300 = TSH. 4,763,300), vikao vya ndani 19 (TSH. 1,900,000), posho ya waandishi wa habari na watangazaji wa ITV, Nipashe, Mwananchi, Star TV na Tanzania Daima (TSH. 4,550,000), matengenezo ya Gari la ALLAN (TSH. 730,000), Batery za Megaphone ya Katibu Mkuu (TSH 300,000) pamoja na Dharura na Uratibu (TSH. 450,000).
Katika ziara hiyo, Dk Slaa atazungumzia mambo yafuatayo;
Kuhusu suala la usalama wakati wa ziara hiyo, imeelezwa kuwa kuna harufu imenuswa ya magenge ya wahuni kuandaliwa na wale marafiki zake ZZK walioko Usalama ili waanzishe vurugu. Kwamba wameandaliwa kwa silaha za moto, baridi na vimiminika (tindikali). Kwamba, wakitumia mwanya huu, haraka dola itasema tukio hilo ni sehemu ya mgogoro wa uongozi ndani ya CHADEMA kwamba kuna watu hawajafurahishwa na kitendo cha ZITTO kuondolewa madaraka. Mytake, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA ngazi ya mikoa na wilaya kuwa uongozi wa chama hicho makao makuu umekuwa ukiibua mbinu nyingi za kujipatia posho huku ofisi za mikoa na wilaya zikiwa hohehahe. Shilingi milioni 19 ambazo zitatumika wakati wa ziara hiyo zingeweza kuwa na manufaa zaidi kama zingeelekezwa kuimarisha chama badala ya kutumika kukagua uhai na uimara wa chama ambao Dk Slaa anajua kuwa chama bado hakijawa Imara. Aidha, kitendo cha CHADEMA kupindisha ukweli kuhusu hofu ya kutokea vurugu wakati wa ziara hiyo kwa madai kuwa eti Usalama ndo wameandaliwa kufanya fujo ni ulaghai mkubwa wa kisiasa. Sote tumeshuhudia jinsi ripoti ya Mkoa wa Kigoma ilivyotahadhalisha juu ya ziara hiyo kutokana na wafuasi wengi na wapenda demokrasia kupinga maamuzi ya CC ya CHADEMA yaliyowavua madaraka ZITTO KABWE, DR KITILA MKUMBO na SAMSON MWIGAMBA. Pia tumeshuhudia Dr Slaa akitahadhalishwa juu ya kukanyaga ardhi ya Mkoa wa Singida.

MAMBO YA KUZINGATIA
- Mambo yaliyoibuliwa na CAG ambayo taarifa zake zitajadiliwa bungeni
- Ripoti ya CHC kuhusu ubinafsishaji wa makampuni
- Ripoti maalum ya uchunguzi wa Spika kuhusu posho za wabunge
- Posho ya Kamati Maalum za Bunge
- Harufu ya ufisadi kwenye mradi wa maji Singida