Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Kuna nguvu huamua hatima yetu.. Kuna nguvu hutuandalia matokeo tusiyopanga wala tusiyoyataka
Kwa waamini wa kiimani nguvu hiyo huuita Mungu au miungu na kwa wasio waamini nguvu hiyo huuita Asili
Kwamba Mungu, miungu ama Asili ndio vimebeba hatima yetu..! Iwe hasi ama iwe chanya
Ukipanga jambo na likatimia kwa usahihi na kwa matarajio yake basi tambua ya kwamba jambo hilo ni baraka na kibali cha hizo nguvu tatu kulingana na imani ya mhusika!
Ukipanga jambo na likaenda kinyume na matarajio yako ama likakengeuka kwenye matokeo basi tambua jambo hilo halina kibali na badala na hizi nguvu husika
Unaweza ukalazimisha kwa kila namna jambo lako lifanyike na likafanyika lakini kwenye matokeo hali ikawa tofauti kabisa na matarajio.. Hapo tambua asili imekukataa
Waswaheli wanasema acha inyeshe ili panapovuja paonekane.. Kuna wakati Asili hutushurutisha kufanya mambo ili mengine yatokee.. Waamini huita unabii
Ziara ya Mwenezi kuizunguka Tanganyika kwa misafara mirefu ya magari ya serikali kwa gharama za mlipa kodi fukara ilitikisa vilivyo kutokana na style ya ziara yenyewe
Ikitarajiwa iwe ziara ya kukijenga chama, ikageuka ziara ya kukiangamiza chama, kutokana na matendo ya Mwenezi kila alikopita
Msafara uliokuwa na magari yasiyopungua 30 na watendaji na maofisa wa wizara mbalimbali serikalini, ulilitia taifa hasara kubwa kutokana na
Gharama za mafuta
Gharama za vipuri
Gharama za chakula na malazi
Gharama za posho kwa kila aliyehusika kwenye msafara
Gharama za matibabu na dharura nyinginezo nyingi
Gharama za muda na uchakavu wa magari nknk
Watendaji na maofisa wa serikali walioitwa mbele ya pilato Mwenezi walinyanyasika vilivyo mbele ya kadamnasi ya wananchi
Watendaji na maofisa wa serikali waliokuwa kwenye ziara ya Mwenezi ukiuliza walikuwa na majukumu gani huwezi kuambiwa
Kuelekea mwishoni mwa ziara iliyopambwa vilivyo na mamluki na chawa wa Mwenezi .. Asili ikaamua kuchukua hatamu.. Kuna jambo kubwa baya likatokea! Msafara ukapata ajali, iliyosababisha majeruhi na uharibifu mkubwa wa magari yasiyopungua 10
Ajali hii ilibadili mazima turufu ya ziara.. Kila kitu kiliishia pale.. Kilichokuwa kimetarajiwa kuhitimisha kama ziara ya mafanikio makubwa.. Kikawa ni kaburi la mwenezi na ziara yake
Ajali haikuwa mwisho bali mwanzo wa mengine yatakayomtesa mwenezi na chama chake kwa muda mrefu ujao..
Magari yaliyoharibika kwenye ajali yanahitajika kutengenezwa
Ili yapate kutengenezwa yanahitajika ripoti nzima ya ajali.. Mhusika kwenye hili ni mwenezi
Mwenezi kagoma kutoa ripoti anasema alitumwa na chama! Chama kiko kimya.. Mbaya zaidi watendaji na maofisa wa serikali waliokuwa kwenye ziara wanatakiwa kujieleza ilikuwaje wakawa kwenye ziara husika na kwa ruhusa ya nani.. Hakuna mwenye majibu yanayotosheleza
Iliyoyarajiwa kuwa ziara ya kukiimarisha chama kimegeuka na kuwa zimwi litishalo kwa mwenezi na chama chake...!!!
Asili huwa haipangiwi... !!!!