Matumizi ya kifisadi ya Dr. Slaa kwenye ziara ya mkoa wa Kigoma, Singida, Tabora na Shinyanga

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, nimefanikiwa kupata waraka wa ndani ya CHADEMA kutoka katika chanzo changu ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Amini usiamini, wakati ofisi za CHADEMA zikiwa katika hali mbaya, Dr Slaa anatumia shilingi laki tatu (300,000) kwa ajili tu ya kununulia betri za Megaphone. Pia mdau wangu amenitonya kuwa Dr Slaa AMELAZIMISHA ziara hiyo iwe ndefu kwa lengo tu la kujiongezea posho. Hii hapa ni summary ya waraka huo.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK WILBROAD SLAA katika mikoa ya Singida, Shinyanga, Kigoma na Tabora ambayo ilitarajiwa kuanza tarehe 3 Desemba 2013 na kumalizika tarehe 23 Desemba 2013 inatarajiwa kugharibu shilingi Milioni 19,833,300/=. Gharama hizo ni pamoja na posho ya Dr Slaa (80,000 x siku 22 = TSH.1,760,000), posho kwa wana timu 7 (40,000 x siku 22 x watu 7 = TSH.6,160,000), mafuta kwa ajili ya magari 3 (lita 2071 x 2300 = TSH. 4,763,300), vikao vya ndani 19 (TSH. 1,900,000), posho ya waandishi wa habari na watangazaji wa ITV, Nipashe, Mwananchi, Star TV na Tanzania Daima (TSH. 4,550,000), matengenezo ya Gari la ALLAN (TSH. 730,000), Batery za Megaphone ya Katibu Mkuu (TSH 300,000) pamoja na Dharura na Uratibu (TSH. 450,000).

MAMBO YA KUZINGATIA
Katika ziara hiyo, Dk Slaa atazungumzia mambo yafuatayo;

  1. Mambo yaliyoibuliwa na CAG ambayo taarifa zake zitajadiliwa bungeni
  2. Ripoti ya CHC kuhusu ubinafsishaji wa makampuni
  3. Ripoti maalum ya uchunguzi wa Spika kuhusu posho za wabunge
  4. Posho ya Kamati Maalum za Bunge
  5. Harufu ya ufisadi kwenye mradi wa maji Singida

Kuhusu suala la usalama wakati wa ziara hiyo, imeelezwa kuwa kuna harufu imenuswa ya magenge ya wahuni kuandaliwa na wale marafiki zake ZZK walioko Usalama ili waanzishe vurugu. Kwamba wameandaliwa kwa silaha za moto, baridi na vimiminika (tindikali). Kwamba, wakitumia mwanya huu, haraka dola itasema tukio hilo ni sehemu ya mgogoro wa uongozi ndani ya CHADEMA kwamba kuna watu hawajafurahishwa na kitendo cha ZITTO kuondolewa madaraka. Mytake, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA ngazi ya mikoa na wilaya kuwa uongozi wa chama hicho makao makuu umekuwa ukiibua mbinu nyingi za kujipatia posho huku ofisi za mikoa na wilaya zikiwa hohehahe. Shilingi milioni 19 ambazo zitatumika wakati wa ziara hiyo zingeweza kuwa na manufaa zaidi kama zingeelekezwa kuimarisha chama badala ya kutumika kukagua uhai na uimara wa chama ambao Dk Slaa anajua kuwa chama bado hakijawa Imara. Aidha, kitendo cha CHADEMA kupindisha ukweli kuhusu hofu ya kutokea vurugu wakati wa ziara hiyo kwa madai kuwa eti Usalama ndo wameandaliwa kufanya fujo ni ulaghai mkubwa wa kisiasa. Sote tumeshuhudia jinsi ripoti ya Mkoa wa Kigoma ilivyotahadhalisha juu ya ziara hiyo kutokana na wafuasi wengi na wapenda demokrasia kupinga maamuzi ya CC ya CHADEMA yaliyowavua madaraka ZITTO KABWE, DR KITILA MKUMBO na SAMSON MWIGAMBA. Pia tumeshuhudia Dr Slaa akitahadhalishwa juu ya kukanyaga ardhi ya Mkoa wa Singida.

ZIARA YA DR SLAA KIGOMA.jpg ZIARA YA DR SLAA KIGOMA 2.jpg ZIARA YA DR SLAA KIGOMA 3.jpg ZIARA YA DR SLAA KIGOMA 4.jpg
 
Hayo matumizi ya kifisadi yako wapi hapo? Kama nyaraka yako uliyotumia ni sahihi......maana CCM mtahangaika sana mwaka huu.....

Kinana yeye posho kwa siku ni shilingi 300,000 , unalinganisha nini?
 
View attachment 125003View attachment 125004View attachment 125006View attachment 125007

Hizi gharama gani, mbona ziko halisia? Sioni ufisadi hapa. Zikiwekwa za CCM huko kusini kwa siku 22, utafunga mdomo wako.
 
SASA mnataka chadema kiwe chama cha ofisini? sasa 80 pa diem mnaona ni kitu kikuuubwa kwa mtu mwenye inclination ya uraisi...... chadema ichanje mbuga...... na bado mtakoma sana mwaka huu.... mlitaka kuzuia ziara sasa mnarudi kinyumanyuma kama kunguru..... DR wakatishe tamaaa zaidi

CHADEMA maji ya shingo babu
 
Hayo matumizi ya kifisadi yako wapi hapo? Kama nyaraka yako uliyotumia ni sahihi......maana CCM mtahangaika sana mwaka huu.....

Kinana yeye posho kwa siku ni shilingi 300,000 , unalinganisha nini?
TUWEKEE basi nyaraka ya ziara ya CCM?
 
Kwa kazi anayoifanya dr hyo ni pesa ndogo sana,tuwekee na pesa anayotumia nape na kinana toka mwanzo mwa ziara yao mpk leo hii.

Ni mwendewazimu pekee anatakaesema hyo ni pesa kubwa au kuna harufu ya ufisadi ndani yake
 
Mbona huelezi msafara wa kinana utatumia shilingi ngapi katika ziara yake inayoendelea mikoa ya kusini na nyanda za juu?
Wewe ultaka hiyo ziara ya siku 18 itumie sh ngapi?
Mbona husemi ziara za kikwete zinatumia sh ngapi huko nje anakokwenda kila mara kama vile yeye ni waziri wa mambo ya nchi za nje?
 
Document ni feki, hasa ukisoma palipoandikwa Angalizo kuwa , zingatieni .....alikuwa anamwandikia nani kuhusu hilo la kuzingatia ?
 
Na bado mtahangaika na CDM mtachoka
Hata angetumia 3 m what is your problem?
Maccm mmetufanya tumekuwa maskini wa kutupwa
Unapoongea hapa kuna watu wako hoi hawajui watakula nini leo
Hata maji safi na salama hawana
huduma mbovu mahospitalini hatuna hata pakugeukia
we need change hii serekali ni ya mafisadi ya watu wachache
wengine wanasema mtanzania asiyemudu kulipia umeme akae gizani
Tena anayasema haya hadharani
shame on you maccm matapeli mafisaidi tumewachoka
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom