Matumizi ya kifisadi ya Dr. Slaa kwenye ziara ya mkoa wa Kigoma, Singida, Tabora na Shinyanga

Wadau, nimefanikiwa kupata waraka wa ndani ya CHADEMA kutoka katika chanzo changu ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Amini usiamini, wakati ofisi za CHADEMA zikiwa katika hali mbaya, Dr Slaa anatumia shilingi laki tatu (300,000) kwa ajili tu ya kununulia betri za Megaphone. Pia mdau wangu amenitonya kuwa Dr Slaa AMELAZIMISHA ziara hiyo iwe ndefu kwa lengo tu la kujiongezea posho. Hii hapa ni summary ya waraka huo.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK WILBROAD SLAA katika mikoa ya Singida, Shinyanga, Kigoma na Tabora ambayo ilitarajiwa kuanza tarehe 3 Desemba 2013 na kumalizika tarehe 23 Desemba 2013 inatarajiwa kugharibu shilingi Milioni 19,833,300/=. Gharama hizo ni pamoja na posho ya Dr Slaa (80,000 x siku 22 = TSH.1,760,000), posho kwa wana timu 7 (40,000 x siku 22 x watu 7 = TSH.6,160,000), mafuta kwa ajili ya magari 3 (lita 2071 x 2300 = TSH. 4,763,300), vikao vya ndani 19 (TSH. 1,900,000), posho ya waandishi wa habari na watangazaji wa ITV, Nipashe, Mwananchi, Star TV na Tanzania Daima (TSH. 4,550,000), matengenezo ya Gari la ALLAN (TSH. 730,000), Batery za Megaphone ya Katibu Mkuu (TSH 300,000) pamoja na Dharura na Uratibu (TSH. 450,000).

MAMBO YA KUZINGATIA
Katika ziara hiyo, Dk Slaa atazungumzia mambo yafuatayo;

  1. Mambo yaliyoibuliwa na CAG ambayo taarifa zake zitajadiliwa bungeni
  2. Ripoti ya CHC kuhusu ubinafsishaji wa makampuni
  3. Ripoti maalum ya uchunguzi wa Spika kuhusu posho za wabunge
  4. Posho ya Kamati Maalum za Bunge
  5. Harufu ya ufisadi kwenye mradi wa maji Singida

Kuhusu suala la usalama wakati wa ziara hiyo, imeelezwa kuwa kuna harufu imenuswa ya magenge ya wahuni kuandaliwa na wale marafiki zake ZZK walioko Usalama ili waanzishe vurugu. Kwamba wameandaliwa kwa silaha za moto, baridi na vimiminika (tindikali). Kwamba, wakitumia mwanya huu, haraka dola itasema tukio hilo ni sehemu ya mgogoro wa uongozi ndani ya CHADEMA kwamba kuna watu hawajafurahishwa na kitendo cha ZITTO kuondolewa madaraka. Mytake, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA ngazi ya mikoa na wilaya kuwa uongozi wa chama hicho makao makuu umekuwa ukiibua mbinu nyingi za kujipatia posho huku ofisi za mikoa na wilaya zikiwa hohehahe. Shilingi milioni 19 ambazo zitatumika wakati wa ziara hiyo zingeweza kuwa na manufaa zaidi kama zingeelekezwa kuimarisha chama badala ya kutumika kukagua uhai na uimara wa chama ambao Dk Slaa anajua kuwa chama bado hakijawa Imara. Aidha, kitendo cha CHADEMA kupindisha ukweli kuhusu hofu ya kutokea vurugu wakati wa ziara hiyo kwa madai kuwa eti Usalama ndo wameandaliwa kufanya fujo ni ulaghai mkubwa wa kisiasa. Sote tumeshuhudia jinsi ripoti ya Mkoa wa Kigoma ilivyotahadhalisha juu ya ziara hiyo kutokana na wafuasi wengi na wapenda demokrasia kupinga maamuzi ya CC ya CHADEMA yaliyowavua madaraka ZITTO KABWE, DR KITILA MKUMBO na SAMSON MWIGAMBA. Pia tumeshuhudia Dr Slaa akitahadhalishwa juu ya kukanyaga ardhi ya Mkoa wa Singida.

View attachment 125003View attachment 125004View attachment 125006View attachment 125007

Hivi ni walaka gani hauna muhuri wala sahii ya mtu anaeizinisha?Toka hapa gamba weeeeee
 
SASA mnataka chadema kiwe chama cha ofisini? sasa 80 pa diem mnaona ni kitu kikuuubwa kwa mtu mwenye inclination ya uraisi...... chadema ichanje mbuga...... na bado mtakoma sana mwaka huu.... mlitaka kuzuia ziara sasa mnarudi kinyumanyuma kama kunguru..... DR wakatishe tamaaa zaidi

CHADEMA maji ya shingo babu

Mkuu, mbona hauhoji matumizi ya shilingi laki tatu kwa ajili ya kipaza sauti cha babu?
 
Msipende kutuaminisha vitu visipokuwepo
Nenda kamwambie mwajiri wako ZZZK akulipe ujira wako maana yeye ndo aliyekutuma
shame on you all!
 
Hivi ni walaka gani hauna muhuri wala sahii ya mtu anaeizinisha?Toka hapa gamba weeeeee

Mkuu, kwa chadema, nyaraka zote zinatengenezwa kwa maelekezo ya dr slaa na mbowe. usitegemee ikifika kwa babu ikataliwe kwani yeye ndiye aliyeagiza
 
Wadau, nimefanikiwa kupata waraka wa ndani ya CHADEMA kutoka katika chanzo changu ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Amini usiamini, wakati ofisi za CHADEMA zikiwa katika hali mbaya, Dr Slaa anatumia shilingi laki tatu (300,000) kwa ajili tu ya kununulia betri za Megaphone. Pia mdau wangu amenitonya kuwa Dr Slaa AMELAZIMISHA ziara hiyo iwe ndefu kwa lengo tu la kujiongezea posho. Hii hapa ni summary ya waraka huo.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK WILBROAD SLAA katika mikoa ya Singida, Shinyanga, Kigoma na Tabora ambayo ilitarajiwa kuanza tarehe 3 Desemba 2013 na kumalizika tarehe 23 Desemba 2013 inatarajiwa kugharibu shilingi Milioni 19,833,300/=. Gharama hizo ni pamoja na posho ya Dr Slaa (80,000 x siku 22 = TSH.1,760,000), posho kwa wana timu 7 (40,000 x siku 22 x watu 7 = TSH.6,160,000), mafuta kwa ajili ya magari 3 (lita 2071 x 2300 = TSH. 4,763,300), vikao vya ndani 19 (TSH. 1,900,000), posho ya waandishi wa habari na watangazaji wa ITV, Nipashe, Mwananchi, Star TV na Tanzania Daima (TSH. 4,550,000), matengenezo ya Gari la ALLAN (TSH. 730,000), Batery za Megaphone ya Katibu Mkuu (TSH 300,000) pamoja na Dharura na Uratibu (TSH. 450,000).

MAMBO YA KUZINGATIA
Katika ziara hiyo, Dk Slaa atazungumzia mambo yafuatayo;

  1. Mambo yaliyoibuliwa na CAG ambayo taarifa zake zitajadiliwa bungeni
  2. Ripoti ya CHC kuhusu ubinafsishaji wa makampuni
  3. Ripoti maalum ya uchunguzi wa Spika kuhusu posho za wabunge
  4. Posho ya Kamati Maalum za Bunge
  5. Harufu ya ufisadi kwenye mradi wa maji Singida

Kuhusu suala la usalama wakati wa ziara hiyo, imeelezwa kuwa kuna harufu imenuswa ya magenge ya wahuni kuandaliwa na wale marafiki zake ZZK walioko Usalama ili waanzishe vurugu. Kwamba wameandaliwa kwa silaha za moto, baridi na vimiminika (tindikali). Kwamba, wakitumia mwanya huu, haraka dola itasema tukio hilo ni sehemu ya mgogoro wa uongozi ndani ya CHADEMA kwamba kuna watu hawajafurahishwa na kitendo cha ZITTO kuondolewa madaraka. Mytake, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA ngazi ya mikoa na wilaya kuwa uongozi wa chama hicho makao makuu umekuwa ukiibua mbinu nyingi za kujipatia posho huku ofisi za mikoa na wilaya zikiwa hohehahe. Shilingi milioni 19 ambazo zitatumika wakati wa ziara hiyo zingeweza kuwa na manufaa zaidi kama zingeelekezwa kuimarisha chama badala ya kutumika kukagua uhai na uimara wa chama ambao Dk Slaa anajua kuwa chama bado hakijawa Imara. Aidha, kitendo cha CHADEMA kupindisha ukweli kuhusu hofu ya kutokea vurugu wakati wa ziara hiyo kwa madai kuwa eti Usalama ndo wameandaliwa kufanya fujo ni ulaghai mkubwa wa kisiasa. Sote tumeshuhudia jinsi ripoti ya Mkoa wa Kigoma ilivyotahadhalisha juu ya ziara hiyo kutokana na wafuasi wengi na wapenda demokrasia kupinga maamuzi ya CC ya CHADEMA yaliyowavua madaraka ZITTO KABWE, DR KITILA MKUMBO na SAMSON MWIGAMBA. Pia tumeshuhudia Dr Slaa akitahadhalishwa juu ya kukanyaga ardhi ya Mkoa wa Singida.

View attachment 125003View attachment 125004View attachment 125006View attachment 125007
Wandishi wa habari nao wanalipwa na CHADEMA?
 
siku 22 kwa 19m ni wastani wa tsh 1m kwa siku. Aliyeweka hizi data ni kada wa chadema. sitaki kuamini wana bajeti finyu hiviyo
 
Umenichekesha mtoa maada kumbe hadi leo CDM inatumia 80,000 per diem
Kweli CDM ndo chama pekee kitakacho mkomboa mtanzania
Hii 80,000 nakumbuka ilikuwa inatumika hadi kufikia 2009
Mungu akulinde Dr wetu wa ukweli
 
jamani bado anaiba tu mbona alizoa hela nyingi sana wakati anajenga nyumba yake hajarudisha lakini tena kazoa zingine huyu mzee wutu hatufai.

Posho ya Dr Slaa (80,000 x siku 22 = TSH.1,760,000), ndivyo alivyoandika Chabruma, sasa mbona kama ni kweli hii hela ndogo hata mimi wa kawaida tu kwenye kampuni, (sio serikalini) nikisafiri nalipwa zaidi ya hapo kwa siku!
 
elfu 80000/= kwa siku ni hela ndogo sana kwa hadhi ya dr.Slaa.
jiulize Kinana anajilipa sh ngapi kwa siku kwenye ziara ya ccm ndio uje kutema pumba hapa.!!
 
waandishi wa habari wa Bongo ni balaa tupu. hivi unategemea wataandika against na mtu anayewalipa?
 
Bila letterhead wala hata signature? Come on this is just another made up document

attachment.php
 
kwa nini wandishi wa habari wanalipwa na chadema badala ya kulipwa na taasisi zao hapa utapata picha kwa nini wandishi huweza kuandika kwa matakwa ya watu binafsi.
 
kajipange wewe uache kutoka mapovu, huwezi zuia CDM.

Hivi watanzania mmelogwa nini? Mada nzuri kama hizi hamtaki kuziona kwa nini? kuna mambo mengi sana ya kujifunza kuhusiana na mada hii, Kuna kitu najifunza hapa kwa kipengele kimoja tu cha WANDISHI wa Habari kulipwa na CHADEMA kwenye ziara hii, ili iweje? siku zote CHADEMA walikuwa wakiwalipa kwenye ziara zao?
 
elfu 80000/= kwa siku ni hela ndogo sana kwa hadhi ya dr.Slaa.
jiulize Kinana najilipa sh kwa siku kwenye ziarq yq ccm ndio kutema pumba hapq.!!

wewe umeona elfu themanini tu. lakini nikuhakikishie kuwa kati ya milioni hizo 19, Dr Slaa pekee atakula zaidi ya milioni tano
 
Ufisadi ni matumizi mabaya, yasiyoidhinishwa na ambayo yamechukuliwa kwa njia ya kughushi...hizo kama ni kweli mbona ziko wazi kabisa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom