Matumizi ya computer

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323

Kwa siri yake mtungi, aijuaye ni kata,
Na nyumba bila msingi, utapasuka ukuta,
Kila palipo na wengi, na mambo ya yatambata,
Kugunduliwa kompyuta, bin'Adamu hana kazi.

Binadamu hana kazi, kugunduliwa kumpyuta,
Si fumbi hili ni wazi, wala si ndoto kuota,

Dunia hakuna kazi,isoweza kompyuta
Kugunduliwa kompyuta, bin'Adamu hana kazi.

Vidato utapitia na cheti utakipata,
Kwa madhumuni na nia, ajira kutafuta,
Patupu taambulia, au kama siyo kusota,
Kugunduliwa kompyuta, bin'Adamu hana kazi.

Daima unapotwanga, ni lazima kupepeta,
Kutenga chuya na chenga, ungo utaukamata,
Hapa ukishaboronga, mchele hataupata,
Kugunduliwa kompyuta, bin'Adamu hana kazi.

Kuadimika ajira, kwa wasomi ni ukata,
Makubwa yake madhara, binadamu kumkuta,
Ni faida na hasara, kompyuta imeleta,
Kugunduliwa kompyuta, bin'Adamu hana kazi.

Dr Hamza, Yousuf Al Naamani (Barubaru)
Mapumzikoni
Mwera. Zanzibar
 
Back
Top Bottom