GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,652
- 14,247
Wanasema "hata akienda juu Kapungu hafikii kwa Mungu" ndiyo. Sisi wazee wa zamani tumekutana na mengi hadi kufika umri huu...kutekwa kisiasa,kiuchumi na kimapenzi pia. Lakini tumeweza ku survive katika jamii yenye kujawa watu na viumbe visivyo vya kawaida. Hivyo wanaotumia IDs zetu bado hawawezi kuwa sisi.
Duniani hatupo peke yetu. Ni ukweli ulio na utupu, uso fichika. Kuna watu na waso watu. Tumechanganyika wote kwenye kapu moja. Na JF imekuwa kama kokoro. Inakamata kila kitu na hatimaye kuvua samaki na waso samaki. So ni jukumu la kila member kujenga utulivu wa akili.
Binafsi kwa siku lazima asubuhi na usiku nipitie JF kujua nini kimejiri ulimwenguni.
Kumeibuka matumizi yasofaa ya IDs za members wakongwe humu ndani katika mitandao mingine ya Kijamii. Mfano mara kadhaa kuna watu wanasema Gudume yupo Twitter. Hapana. Sina account ya jina langu Twitter na mtu yeyote anayetumia jina hili nitamke tu kuwa huyo ni tapeli kama wale wanaosema "ile ela itume kwenye number ii"
Gudume anabaki JF akifurahi na wanaofurahi na kulia na waolia. Wapo wazee wenzangu humu tunaendelea kusomana na kubadilishana mawazo. Naamini tutafikia hatua siku moja hadi ya kubadilishana mademu " ashakum si matusi" maana pia inachosha kila mara kubadilishana mawazo tu.