Mkuu hi si kweli.
Unamaana hakuna wasomi hapa nyumbani? Mbona wengi tu.
Ni kweli wasomi wa majina (Dr...) wapo, lakini vilaza ni wengi katika hilo kundi unalodai, kuliko wasomi.
Wasomi wengi ambao wako kwenye nafasi za maamuzi digrii zao zinatokana na vyuo vinavyotiliwa mashaka kama PWU ambacho ni unaccredited university. Kumnukuu mzee Moshi Augustine, kuhusiana na vyuo kama PWU, gazeti moja la Marekani, Pacific Business News limeandika "In the academic world it's just about as useless as it can be." Unaweza kuipata habari nzima hapa,
http://quackfiles.blogspot.com/2005/...es-boffin.htm
Mzee Moshi alipendekeza hatua za kuchukua ili tuwe na jeuri ya kusema tunao wasomi:
(1) Wale ambao wametoa vyeti kutoka PWU na "diploma mills" nyingine, wafutiwe hizo digrii kwenye CV zao. NI CV CHEATS. Wasifukuzwe kazi, kwani waajiri nao wana udhaifu; walipashwa kuchunguza hivyo "vyuo" kabla ya kuzikubali hizo CV. Waendelee na kazi kwa kutegemea vyeti vyao vingine, mradi viwe vinaridhisha.
(2) Mwajiri ambaye hana uwezo wa kuhakiki usahihi wa digrii anazopewa kwenye CV, awe na uwezekano wa kuzituma kwenye Baraza la Vyuo Vikuu kuhakikiwa (at a fee). Hili baraza liwe na wasomi wa kufanya uchunguzi unaotakiwa, na kutoa ripoti ambayo inajadliwa na kikao rasmi cha baraza, ambacho ndicho kitatoa uamuzi wa mwisho.
Sasa kusema tuna wasomi, wakati hatuna chujio la kuwatolea wababaishaji, inanitia mashaka, na inanitia mashaka kuwa na kiburi cha kusema wasomi wapo wengi tu, wakati vyuo havina wataalam na in desperation, hata wenye vyeti feki wanakula ajira na hakuna jitihada za makusudi kuwaondoa kwanza.