Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 228
- 249
Matokeo ya darasa la saba yametoka jana lakini sasahivi hayana msisimko kama zamani nimewiwa kuandika historia yangu ya kupata matokeo ya darasa la saba ilivyokuwa baada ya kuona kaandika comrade Habibu Mchange
Nilimaliza darasa la saba mwaka 2004 na matokeo kipindi hicho yalikuwa yanatoka mwezi wa 12 karibia na christmas. Matokeo hayo yalikuwa yanaleta hisia sana kwa sababu shule ziliilkuwa chache. Tarafa yetu ya Kamachumu ilikuwa ina sekondari moja ambayo ni Rutabo sec na ilikuwa kupata nafasi si shughuli ndogo maana shule nyingi zilikuwa zinaitegemea. Ila mimi sikuwa na ndoto ya kusoma katika hiyo shule hata kwenye selection sikuwahi kuiweka nakumbuka nilijaza Bwiru Boys, Tabora Boys na Ilboru. Nikiamini kuwa lazima nitafaulu na kwa bahati nzuri nilikuwa najitahidi hata darasa letu lilikuwa na ushindani. Basi siku matokeo yametoka ilikuwa Ijumaa, basi kila mtu alienda kuangalia matokeo uzuri sisi wengine tulikuwa tunaishi karibu na matokeo yanapobandikwa. Waandishi wa habari wa kujitegemea huwa hawakosi kabla hujaenda ushaletewa fununu. Basi nikaambiwa jina langu halipo shule ya Rutabo nilifurahi sana nikaona ndoto yangu imetimia ila sijajua bado naenda shule gani. Baadae nikachukua baiskeli ya mzee wangu fasta Phonex hadi kwenye ubao. Nikaangalia kwa makini sikuona jina langu. Kuna rafiki yangu mmoja tulikuwa tunakaa siti jirani nilimsaidia kwa kiasi fulani naye nikaona ametoboa ndio nikajipa imani kama huyu kafaulu basi mimi nimetoboa.
Watu wengi walikuwa wananijua kwa sababu tulikuwa tunashindana mitihani ya kata na tarafa na wengine tulisoma tuition pamoja ya mzee wangu almaarufu Kibanza Z basi nikawa naulizwa nimechaguliwa wapi? Mimi nawaambia bado sijapata matokeo yangu ila wakawa wanaamini lazima nimefaulu kwenda shule za vipaji kwa ajili ya uwezo wangu wa darasani. Darasa letu lilifanya vizuri tulikuwa wanafunzi 46 walifaulu 27 wote kwenda Rutabo na ni mimi tu nilikuwa sijajua matokeo yangu.
Mzee wangu wala hakuwa na wasiwasi kwamba nimefeli ila kuna watu wakaanza kusema kuwa hata mtoto wa Mwl Abdul naye kafeli ila mimi nikachukulia kawaida tu. Ila classmates wangu wote hakuna ambaye angeweza kuamini kama ningefeli kwa sababu walikuwa wananijua nilivyo vizuri. Tukafika hadi Jumamosi matokeo sijapata ila bado ninajipa nguvu. Basi hapo watu kila mtu akaanza kusema nimefeli ila na mimi bado siamini. Ikafika siku ya Jumapili sijapata matokeo na mimi hapo sijajua matokeo yangu na imani nilishaanza kuipoteza kwa kiasi fulani. Siku hiyo aliukuwepo binamu yangu alikuja kututembelea basi nikamsindikiza hadi stendi.
Siku ya jumapili huwa ni siku ya gulio na huwa ni sehemu ya watu kukutana basi njiani nakutana na makundi mbalimbali wa wale tuliosoma wote na kiasi kikubwa waoliofaulu shule moja huwa wanakutana na kupanga mambo yao. Wakati narudi nikakutana na Macklina Clemence alikuwa ni mtu ambaye ni kama mpinzani wangu hakuwa na furaha sana kwa sababu naye hakupenda kuchaguliwa shule ya Rutabo. Tulivyokutana akanipa hongera ya mimi kufaulu nikamuambia mimi sijachaguliwa akaniambia wewe lazima uende shule za mbali. Basi nikaagana naye nikarudi zangu nyumbani. Ila hapo watu nikipita wanasonteana vidole kuwa nimefeli na mimi ninaona. Na kitu kingine mimi nilikuwa mtundu sana sasa watu wengi wananijua hivyo lazima watake kujua habari zako na vilevile mtoto wa walimu hivyo lazima ujulikane.
Nilivyorudi ndani nikajifungia chumbani na kuanza kulia kuwa nimefeli na Macklina niliona kama kanikebehi eti nimefaulu mbali wakati sijajua matokeo yangu siku ya pili. Nililia sana mama yangu akaja kunibembeleza wapi sikumuelewa akaja baba naye sikumuelewa ninalia tu kwa ajili ya matokeo ya darasa la saba. Nilikuwa nawaza mbona kuna watu nimewasaidia wamefaulu halafu mimi nifeli au nimefutiwa mtihani? Ni maswali ambayo nilikuwa najiuliza sipati majibu. Mlo wa mchana nikagoma kula. Sasa baba yangu akaniambia ndio hata kama umefeli nitakupeleka private lazima usome ila mimi sikumuelewa na private nilikuwa naona siyo shule.
Siku hiyo alikuja Baba yangu mdogo ambaye nilikuwa hata simjui maaana aliondoka tukiwa bado wadogo sasa walikuwa wana ile furaha ya kurudi kutoka huko ughaibuni. ila mimi wala hata sikwenda kumsalimia ikabidi mzee anitie mkwara kunitia bakora nikamsalimia kiushingo upande nikajificha tena chumbani nalia. Ile siku ilikuwa ya uchungu sana kwangu. Mama yangu akanifuata akanieleza kuwa lazima nitasoma ila mimi hicho hakikua kipaumbele changu mimi nilitaka nifaulu nichaguliwe shule nzuri.
Binamu yangu Sauda kumbe nilivyomsindikiza aliona kabisa kuwa nimepagawa ikabidi aende mkoani kuangalia kama atapata matokeo yangu. Ilikuwa muda wa saa kumi ninalia ninasikia baba anaongea sauti kwa juu kuuliza nimechaguliwa shule gani? Nikasikia anasema Bwiru! Bwiru basi walikuja wote chumbani wakanibeba kwa juu ilikuwa ngumu kwangu kushangilia maana nilikuwa nishamkufuru hadi Mungu kwa kumlaumu. Basi binamu yangu Elisha Chizanye acha anibebe juu kwa juu. Mimi nilikuwa bado nabubujikwa na machozi kwa sababu nilishalia sana sema roho yangu ilitulia na nikaona ndoto yangu imetimia. Kumbuka mlimwengu mimi hata Bukoba mjini sipajui Mwanza ndio kabisa napasikia redio Free Afrika.
Hapohapo nilinawa uso nikavaa na pamba zangu nikaeenda kutamba mjini kwamba walikuwa wanasema nimefeli sasa naenda kuwapa matokeo waliyoyataka. Nikamtafuta ndugu yangu Mohamed Suleimani maana yeye alikuwa anaingia kidato cha pili pale Bwiru boys ndio tunaweza kuongea lugha moja aweze kunipatia moja mbili na tatu kuhusu shule yetu.
Ninachosikitika sasahivi matokeo hayana hisia kwa sababu shule za serikali hazifanyi vizuri. Mtu anafaulu serikali ila lazima ahamishwe tu. Mzazi anamsomesha mtoto shule ya serikali huku roho yake inasononeka. Shule zimekosa mvuto kipindi chetu ilikuwa raha sana.
Matokeo yangu ya darasa la saba siwezi kuyasahau.
#mlimwengumimi