Mtihani nimeufanya, tuliopata kuanzia 70 sidhani kama tunafika hata 40 kati ya watu 14,000. Sijafuatilia sana sababu namba yangu ipo page ya kwanza, pages nyingine mia ngapi sina hakika wameita kuanzia alama zipi. Ila naambiwa kuna zero kama kumi hivi.
Marks nilizojua nitapata nimekosa mbili kuzifikisha, nina historia ya kuwa accurate kukadiria marks nitakazopata kama swali sina hakika sihesabii, kama sijui sijui, sina kubahatisha na nikitoka nahakiki na wale top cream kichwani.
Tuliopata alama za juu tunakwambia mtihani ulikuwa na mitego, uliyepata chache unadai mitego haikuwepo.
Na mtihani wa Customs haukuvuja, sijaona aliyekuwa anastahili akilalamika. Wanaolalamika ni wale hata tukijadili kitu hawajui, solvings wanakariri badala waelewe, wanalalamikia kutokuwa na calculation swali nyanya lile kuzidisha % za mamilioni yaliyo kamilifu. Mtu % ya 105,000,000 analalamika hana calculator.