Matokeo ya kupenda misaada

Matokeo ya kupenda misaada

Troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,809
Reaction score
40,560
Sijui ni kuathiriwa na malezi au tabia tu.

Mimi najua kuomba au kutarajia msaada huwa ni hatua ya mwisho sana.
Kuna baadhi ya watu hudhani msaada ni haki yao. Na matokeo yake ni yafuatayo.

Kuwa wazembe. Kutafuta wa kumtweka matatizo na majukumu yao.
Chuki hasa kwa pale walipoomba msaada na kushindwa kupewa.. Wanasahau msaada si lazima.

Huzalisha uvivu wa akili na mwili mtu kudhami yeye hawezi kufanya lolote mpaka asaidiwe.
Kupenda misaada huabisha na kushusha utu wako.

Wanapaswa kujua kila mtu huwa anakabili hali ngumu ni vile sababu anabaki nalo moyoni.
 
Hivi kwanini umchukie mtu kisa ameshindwa kukusaidia?? Mimi nipo tofauti sana hata ukiahidi kunipa msaada na usinipe bado nakuwa kiroho safi na wewe. Msaada sio deni kwamba lazima alipe.
 
Back
Top Bottom