Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Gonga hapa kupata matokeo ya Kidao cha Nne - 2010
au
Hapa


• SHULE ZA SERIKALI ZAGARAGAZWA TENA, SEMINARI JUU

na Betty Kangonga




JUMLA ya watahiniwa 177,021 waliofanya mtihani wa taifa wa Kidato cha Nne Oktoba mwaka jana wamefaulu huku wasichana wanane wakishika nafasi kumi bora kitaifa.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, kiwango cha ufaulu kimeporomoka kwa asilimia 22.11 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka juzi.

Shule za binafsi hususan seminari zimeendelea kung’ara wakati zile za umma zikifanya vibaya na kushika nafasi za mwisho.

Katika matokeo hayo, wanafunzi wanne wamefutiwa matokeo kutokana na kuandika lugha ya matusi katika mitihani ya masomo ya Biolojia, Historia, Kemia na Jiografia.

Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Joyce Ndalichako, alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo ni zile zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na zaidi, ambazo ni Uru Seminari (Kilimanjaro), Marian Wasichana (Pwani), St Francis (Mbeya) na Canossa (Dar es Salaam).

Nyingine ni Msolwa (Morogoro), Feza Wavulana (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph’s Iterambogo (Kigoma) na Barbro - Johnson (Dar es Salaam).

Aliwataja wanafunzi walioshika nafasi kumi bora kitaifa kuwa ni Lucylight Mallya, Maria –Dorin Shayo wa Shule ya Wasichana ya Marian, Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson, Diana Matabwa na Neema Kafwimi wa Shule ya Wasichana ya St Francis.

Wengine ni Beatrice Issara wa St Mary Goreti, Johnston Dedani wa Ilboru, Samwel Emmanuel wa Moshi Technical, Bertha Sanga wa Marian na Bernadetha Kalluvya wa St Francis.

Hata hivyo, pamoja na wasichana kung’ara katika nafasi kumi za kwanza kitaifa, bado wavulana wameendelea kufaulu kwa wingi.

“Wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimia 43.47 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.28,” alibainisha Ndalichako.

Alizitaja shule kumi za mwisho kitaifa zilizokuwa na watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni Changaa, Kolo, Kikore, Hurui, Thawi, (Dodoma), Pande Darajani (Tanga), Igawa (Morogoro), Makata (Lindi), Mbuyuni na Naputa (Mtwara).

Ndalichako alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo zipo katika kundi la watahiniwa chini ya 40 ni pamoja na Don Bosco (Iringa), Feza wasichana (Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro) na Queen of Apostle Ushirombo (Shinyanga).

Nyingine ni Sengerema Seminari (Mwanza), Sanu Seminari (Manyara), Bethelsabs Wasichana (Iringa), St Joseph –Kilocha Seminari (Iringa), Dungunyi Seminari (Singida) na Mafinga Seminari (Iringa).

“Pia zipo shule za mwisho ambazo zimefanya vibaya zilizokuwa na watahiniwa chini ya 40 kati ya hizo ni Sanje ya mkoani (Morogoro), Daluni (Tanga), Kinangali (Singida), Mtanga (Lindi), Pande (Lindi), Imalampaka (Tabora), Chongoleani (Tanga), Mwamanenge (Shinyanga), Mipingo (Lindi) na Kaoze (Rukwa)”, alisema.

Jumla ya watahiniwa 311 na watahiniwa wawili wa kujitegemea wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

“Baraza pia limefuta usajili wa kituo cha watahiniwa wa kujitegemea P1189 cha Biafra kutokana na kukiuka taratibu za uendeshaji mitihani…maana kituo hicho kilikuwa na watahiniwa wengi kuliko uwezo wake, jambo lililosababisha usumbufu,” alisema.

Pia baraza hilo limetangaza kusitisha matokeo ya wanafunzi 1,448 ambao walifanya mitihani bila ya kulipa ada ya mtihani, ambapo watatakiwa kulipa na faini katika kipindi cha miaka miwili ili waweze kupewa matokeo hayo.

“Wanafunzi wawili wamefanya mtihani kwa sifa zinazofanana, hivyo tumesitisha matokeo yao hadi wakuu wa shule hizo watakapowasilisha nyaraka kuthibitisha uhalali,” alieleza.

Ndalichako alisema watahiniwa 35 wa Shule ya Sekondari Bara wamefutiwa matokeo na kuondolewa katika usajili baada ya kutumia majina ya watahiniwa ambao walichaguliwa kujiunga na shule hiyo lakini hawakwenda kuripoti.

Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2010 walikuwa 458,114 wakiwamo wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 na wavulana 242,030 sawa na asilimia 52.83, ikilinganishwa na mwaka 2009 ambao walikuwa 351,152, hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa watahiniwa 106,962.

“Watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 441,426 sawa na asilimia 96.36 na watahiniwa 16,688 hawakufanya mtihani sawa na asilimia 3.64 ya waliosajiliwa,” alifafanua.
source: Tanzania Daima
 
hey crashwise are u serious kuwa tokeo limetoka au wataka kutia watu presha,halafu mbna matokeo yamechelewa and no body seems to care,are we serious kweli ama ?
 
hey crashwise are u serious kuwa tokeo limetoka au wataka kutia watu presha,halafu mbna matokeo yamechelewa and no body seems to care,are we serious kweli ama ?
angalia hiyo link hapo juu....wamechelewesha labda walikuwa wanachakachua ................
 
Jamani hali ni mbaya sana matokeo ya shule za kata kama ilivyotarajiwa. Je sasa hii ndo itakuwa turning point ya wanavijiji huko vijijini kuwahusudu CCM? Je serikali itatoa tamko gani? Hapa ndo tunaona umuhimu wa kutenganisha siasa na maswala yanayohitaji taruma.

WANANCHI AMKENI SASA DOWANS + MATOKEO VYATOSHA KUWAWEKA BALABALANI MPAKA KIELEWEKE!
 
hey crashwise are u serious kuwa tokeo limetoka au wataka kutia watu presha,halafu mbna matokeo yamechelewa and no body seems to care,are we serious kweli ama ?


Mkuu hapo kweye red. Kwani yalitakiwa yatoke lini. Manake mtihani wamemaliza Oktoba mwishoni. Mie nadhani tuwapongeze NECTA this time wamewahi ukizingatia idadi ya shule za kata zilizoongezeka
 
Shule zenye majina ya rais wa Tanzania na viongozi wastaafu zimehaibisha majina yao. Nakusudia kupeleka pingamizi Wizarani majina yabadilishwe ili tuendelee kuyaenzi majina yao ktk njia nyingine mfano viwanja vya ndege,vya mpira,magari n.k Mfano:1. J.K.kikwete div.one 0,div.two 4,div3 2 div4 ni 29 na FLD 52. Na shule ya Jakaya Kikwete div1 0,div2 ni 1,div3 ni 5 ,div4 48 na FLD 76. Pia ana mkapa FLD 107. Aidha mwanaJF mwenzetu Mwanalugali kama ID yake ilivo imefeli vibaya div.1&2 ni 0,div3 1 na div4 30, FLD 107,naye atafute ID nyingine kukwepa aibu. Kwa ujumla nawapongeza wote Tanzania waliohitimu elimu iyo,ambayo mpaka leo serikali imesema ni Elimu ya lazima yani itakuwa compulsory/primary Education. Hongera.
 
Shule za Dini Zimeendelea Kutesa kama Kawaida sijui kama kuna Shule ya Serikali kwenye top ten
 
Shule za Dini Zimeendelea Kutesa kama Kawaida sijui kama kuna Shule ya Serikali kwenye top ten
kuna shule inaitwa bondeni ni shule ya ndugu zetu waislam daah yaani hii shule kila mwaka wao balaa....
 
Back
Top Bottom