samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Seminari wanasimamia misingi ya nidhamu, maadili na uwezo wa kitaaluma. Wastani wa kuvuka kuingia darasa lingine ni hamsini jini ya hapo huna chako hata ule wastani wa serikali wa form two hawaujali ukichemka wastani wao wanakutimua. Kila mwezi wanafanya monthly test. Pia wanazingatia muda wa kusoma taa zote zinazimwa sa nne usiku na hakuna anayeruhusiwa kusoma zaidi ya hapo labda kwa kujificha. Zaidi ya hapo wako wachache darasani hivyo inakua rahisi kuwa administer. Ukiwa mtukutu wanakutimua bila kujali una uwezo gani darasani ndio maana wengi wanaotimuliwa seminari wakienda shule nyingine za private wanaendelea kuongoza labda na huko wanafanya udanganyifu...