Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 607
jee wanapoingia vyuoni mbona bogas?
Sio kweli wanafanya vizuri sana. Kaangalie pass za Bernard Membe waziri wako, ni mseminari yule! wako wengi tu! Wanafanya vizuri, usiloelewa kusoma inatakiwa nidhamu! Enzi zile za mitihani ya NABOCE, na NAD kwa upande wa wahasibu, wapo watu wengi waliokuwa wamefeli form four, lakini baada ya kugundua makosa yao, waliweza kufanya masomo ya jioni na leo hii hawa wana CPA na ni viongozi wakubwa katika mashirika na makampuni. Yaani hata huyo aliyeharibiwa udogoni kwa kupitia shule zisizokuwa na mwenendo wa kitaaluma, anao uwezo bado, ilmradi ajiwekee nidhamu mbele!
Umewahi kupanda basi za kwenda mkoani akawepo mzungu? Utaona sisi tunapiga porojo au tumesinzia, lakini yeye anasoma. Wao hufunzwa wakiwa miaka 2 tu kuwa na nidhamu ya kusoma, matokeo yake siku zote watatuzidi! Ndiyo watatuzidi, sisi tutabaki kubishana tu na kulalamikia uchovu wetu kwa wengine, kumtafuta mchawi, na kwako wewe mchawi ni mkristo kwa sasa hivi, lakini nchi inavyozidi kuangamia, mchawi atabadilika, maana hata huko seminari naona nidhamu zimeanza kushuka, na matarajio utaona matokeo mabaya! TUJILAUMU KWA KUKOSA NIDHAMU- hivi unajua ni maeneo ya pwani ambako watu hukaa na kutokemea kabisa watoto wakitukana matusi!?