MATOKEO kutoka vituo mbalimbali, Arumeru Mashariki

Status
Not open for further replies.
Mwisho wa Siku mgombea wa ccm ndiye atakaye tangazwa mshindi - hii nchi bwana!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa kupata uhakika tunaomba matokeo yawekwe yote hata kama si mazuri kwa M4C tuweze kujua

Tukiyaweka tutapata BAN mkuu, ila vituo vingi sasa wanashinda CCM tena kwa tofauti kubwa mno. Hali si nzuri kwa CDM na kuna tetesi baadhi ya viongozi wao hawaonekani.
 
Jamani tafadhali sana msitutanie tunasubiri kwa hamu ushindi wa CCM mbona mnataka kuleta za kuleta wakati mnajua matokeo ni kinyume? CCM Hoyee!!!
 
Wanabodi,
Hatimaye matokeo ya awali ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki yameanza kutolewa na kuonyesha Chadema inaongoza na kuiacha CCM kwa mbali!.

kituo cha Nshapu 3 kata ya Nkoaranga Chadema 110- CCM 74
Kituo cha Ngarasero:
Chadema 116-CCM 51
Kituo AFP - CHADEMA - 141 CCM - 32
Majiyachai Chadema 130 CCM 53
Chadema 105 CCM 68
Chadema 115 CCM 42
Chadema 118 CCM 48
Mjimwema
Chadema 125 CCM35
Chadema 129 CCM 37
Usa River
Chadema 151 CCM 17

Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya ITV ya saa 12:00 yameonyesha Chadema kuongoza katika vituo vifuatavyo!.


NB: Matokeo haya ni ya awali tuu ambayo yanaonyesha nyota njema huonekana asubuhi ila wapenzi na mashabiki wa Chadema msianze kushangilia. Ya Busanda na Biharamulo Magharibi yananikumbusha kuwashauri mzianze kushangilia, uchaguzi ulishaisha leo ni uthibitisho tuu!.
 
hv jamani nchi hii bado kunawatu wengi bado wanaipigia ccm.
Mimi nataka ifike wakati cdm 150 ccm 2
kwanza mgombea mwenyewe hajipigii anataka apate toka wapi!?

Haya matokeo ni MAPINDUZI! CCM na tamba zote na kuwaleta kina Mkapa hasa hapo Usa River na Tengeru hospitali, ama kweli CHADEMA NI DUME!

Na naomba nikisali sana CCM akubali kushindwa, asije akafanya mizengwe ya kuchakachua mahesabu, maana hawa waliopigia chama inaonekana ni wengi na hasira ya wengi inaweza kuleta madhara makubwa, CHONDE CHONDE NKAPA, WAASIE BASI WATU WAKO -WATAELEWA UKISEMA WEWE KWANI WAO SI WAVIVU WA KUFIKIRI KAMA ULIVYOSEMA CHADEMA WAKO HIVYO
 
Hivi haya matokeo ni ya kwali au mnatudanganya, isijekuwa ndiyo ule utaratibu wa kutufurahisha na matokeo mazuri halafu mwishoni mnaanza kutoa yale ambayo CCM wameshinda? Hata Igunga ilikuwa hivihivi, tukafarijika, halafu mambo yakageuka. Tupeni matokeo yenye uhakika wakuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom