Kwa hili tunajidhalilisha. Na akitokea mwendawazimu akasema kuna hisa na Hospitali ya Apollo inayotaka kujenga Hospitali kubwa ya Moyo nchini katika eneo la UDSM anaweza kuaminiwa na Watanzania wengi.Hii inamaanisha madaktari wa hapa Tanzania uwezo wao ni mdogo.
Hapo ndiyo tuna anza kuelewa kuwa,viongozi na familia zao wakiumwa hata mafua huwa wanaenda India.mimi nashindwa kufahamu hata maralia inaweza mpandisha mtu ndege, hadi sasa sijajua ni ugonjwa gani zaidi ya maralia unaompeleka huyu mbunge india. Nadhani ikiwa ndivyo ninavyofikiri basi maralia itatuua wengi
Wana-mind kwenda kupata pilipili, lakini wawe macho mifisadi wan mtandao, waweza kurudi kama baba wa taifa!
Wanasiasa wa Tanzania wamejazana bara hindi wanatafuta nini? Au babu wa loliondo kahamia India? nini! Au ndio historia inajirudia ya akina vasco da gama kutafuta pilipili manga bara hindi.[/QU Kuna machinjio ya wazalendo.
Wanasiasa wa Tanzania wamejazana bara hindi wanatafuta nini? Au babu wa loliondo kahamia India? nini! Au ndio historia inajirudia ya akina vasco da gama kutafuta pilipili manga bara hindi.
Mkuu inahuzunisha sana hata mgonjwa wa malaria anapelekwa huko. Mwishowe hata mtu akipata jipu basi atapelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Yaani hela ya radar na kulipa Dowans tunayo lakini hela ya kugharamia ujenzi wa hizo medical centers hatuna!
Ukiona hivyo hana Malaria
Wanajamvi nalileta hili tulijadili na ikiwezekana tusaidiane, Kama mnavyojua ni kawaida sana hawa wenye nchi wakiugua kidogo faster wanapelekwa India kwa matibabu zaidi, Kina mwakyembe, Zito na wengine wengiiiiiii unaowajua hii nimeitoa tu kama mfano. Ni kweli hawa ni viongozi wetu lakini je na watanzania wengine tena wenye matatizo ambayo hayatibiki hapa mbona wanachwa? Namkumbuka Mh. Kafulila alipoongea bungeni Mama Nagu alimbeza, Naomba niwape mfano; Na Ndugu yangu ambaye kitaaluma ni tabibu na alikuwa akiongeza ujuzi pale muhimbili miaka kama minne iliyopita akapata ajali ya kuanguka ghorofani, infact aliangukia jiwe lililopiga spinal cord na kumfanya kupooza toka kiunoni mpaka miguuni, bahati mbaya zaidi siku anapata ajali madaktari pale muhimbili walikuwa kwenye mgomo kkwahiyo alikuja kufanyiwa upasuaji after 3 days, hakupona mpaka leo yuko kwenye wheel chair. Huyu ni kijana, tena jembe haswaa, na mpaka sasa anaingia na wheel chair yake na anatibu watu na watu wanamkubali saaana, huyu bwana ana kila dalili kuwa akipata matibabu ya kiwango husika kuna uwezo mkubwa sana wa kuja kutembea na kulijenga taifa letu kwa kuboresha afya za watu. Amepeleka maombi ya kwenda India pale wizara ya afya lakini mpaka leo kimyaaa. Lakini hawa wenye nchi yao ni seconds tu mtu yuko India. Hivi hasira za watu wanaokosa tiba muafaka mnaionaje? ni kwanini wengine iwe rahisi hivi na wengine iwe balaa? Inabid uwe mwanasiasa ili upate kila kitu duniani smoothly, kwa yeyote mwenye password ya kuaccess njia za kumsaisia huyu bwana kwa kweli mchango wake utakuwa wa thamani sana.