Matibabu India, Bomu jingine linalotegwa

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,401
Huwa najiuliza maswali mengi na ninakosa majibu,kwa nini viongozi wetu hukimbilia kutibiwa india??je huduma walizonazo hatuwezi kuziboresha tukatibiana kwetu??na kwa nini ni india pekee??je unafuu wa gharama za matibabu?na kwanini wasikimbilie nchi za Ulaya na America au Asia Pacific(korea ya kusini na Japan)
Kama hawa viongozi wanayomamlaKa ya kuamua nini kifanyike katika Taifa letu na nini sikifanyike katika Taifa letu kwa nini wasiamue kuboresha huduma za afya wakijua hipo siku nao watahitaji hiyo huduma badala ya kujirimbikizia mali nyingi na kutufanyia ufisadi katika Taifa leo?..

HAKIKA KWA MUNGU HAKUNA UPENDELEO MASKINI NA TAJIRI WOTE WATAKUFA TOFAUTI NI MDA NA WAKATI.
GLORY TO GOD
 
Hivi karibuni kumekuwapo taarifa za Mawaziri na wabunge kuugua na wote kupelekwa India kupata matibabu. Kinachoniskuma kuhoji kwamba Bunge linapata kamisheni katika Hospitali za India ni kutokana na Wabunge kuhudumiwa kwa takriban asilimia 100 na Bunge. Hivi hakuna Hospitali katika nchini nyingine zenye uwezo wa kuwatibia Wabunge?
 
Nadhani ni suala tu la ubora wa Tiba itolewayo huko na unafuu wa gharama.
 
Nchi hii haki ya kuishi tunatofautiana kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi wa kawaida!Wabunge wanahaki zaidi kuliko wananchi.
 
Suala la kutibiwa nje ya nchi lisiwasumbue sana kwasababu hata mke wa Obama mwenyewe alishawahi kwenda Afrika ya Kusini kupasuliwa jipu. Nadhani ni suala la maamuzi tu na hakuna kingine hapo.
 
Wangepelekwa marekani ungeitisha maandamano.
Tumia akili.
OTIS.
 
Hivi karibuni kumekuwapo taarifa za Mawaziri na wabunge kuugua na wote kupelekwa India kupata matibabu. Kinachoniskuma kuhoji kwamba Bunge linapata kamisheni katika Hospitali za India ni kutokana na Wabunge kuhudumiwa kwa takriban asilimia 100 na Bunge. Hivi hakuna Hospitali katika nchini nyingine zenye uwezo wa kuwatibia Wabunge?

Serikali ione umuhimu sasa wa kujenga Muhimbili nyingine nje ya mji
Kuliko kuwanufaisha hao wahindi kwa matibabu
 
Wangepelekwa marekani ungeitisha maandamano.
Tumia akili.
OTIS.
Lazima tufikiri nje ya boksi kwa sababu Prof Mwandosya, Dk. Mwakyembe, Chami na hata Zitto naye anataka kupelekwa huko kwa mujibu wa Katibu wa Bunge.
 
At least wanaenda India, wangekuiwa wanaenda Marekani ndo tungezidi kuumia zaidi.
 
Kweli hapa Tanzania wameshindwa kumtibu Malaria mpaka apelekwe India? Sasa hizi Hospital zetu zipo kwa ajili gani ikiwa kila siku viongozi Mafisadi wakiumwa wanakimbizwa India? Wizara ya Afya ni Matatizo matupu hapa nchini.
 
Kwa kweli inasikitisha kwenda kutibu maumivu ya kichwa 'Kipanda Uso' na malaria India. Kama mtu ana maradhi mengine yanayohitaji matibabu huko waseme tu kuliko kujaribu kutugeuza mazuzu.
 
Kulikuwa na mpango wa Mh. Kikwete na serikali ya India kujenga hospital kubwa pale karibu na Mlimani City, hii mambo imeishia wapi?
 
Suala la kutibiwa nje ya nchi lisiwasumbue sana kwasababu hata mke wa Obama mwenyewe alishawahi kwenda Afrika ya Kusini kupasuliwa jipu. Nadhani ni suala la maamuzi tu na hakuna kingine hapo.
Kwa nini tusiwe na hospitali hapahapa nchini ambazo zinatoa huduma bora zaidi ili na sisi tuhudumie viongozi wa nchi nyingine?
 
Kujibu swali lako kwa kifupi ni kwamba" hakuna hospitali ya kuwatibu viongozi wetu"

hivi karibuni kumekuwapo taarifa za mawaziri na wabunge kuugua na wote kupelekwa india kupata matibabu. Kinachoniskuma kuhoji kwamba bunge linapata kamisheni katika hospitali za india ni kutokana na wabunge kuhudumiwa kwa takriban asilimia 100 na bunge. Hivi hakuna hospitali katika nchini nyingine zenye uwezo wa kuwatibia wabunge?
 
Kulikuwa na mpango wa Mh. Kikwete na serikali ya India kujenga hospital kubwa pale karibu na Mlimani City, hii mambo imeishia wapi?
Lile lilikua CHANGA LA MACHO,we humjui Mkulu kwa sanaa?
 
Back
Top Bottom