Wanajamvi nalileta hili tulijadili na ikiwezekana tusaidiane, Kama mnavyojua ni kawaida sana hawa wenye nchi wakiugua kidogo faster wanapelekwa India kwa matibabu zaidi, Kina mwakyembe, Zito na wengine wengiiiiiii unaowajua hii nimeitoa tu kama mfano. Ni kweli hawa ni viongozi wetu lakini je na watanzania wengine tena wenye matatizo ambayo hayatibiki hapa mbona wanachwa? Namkumbuka Mh. Kafulila alipoongea bungeni Mama Nagu alimbeza, Naomba niwape mfano; Na Ndugu yangu ambaye kitaaluma ni tabibu na alikuwa akiongeza ujuzi pale muhimbili miaka kama minne iliyopita akapata ajali ya kuanguka ghorofani, infact aliangukia jiwe lililopiga spinal cord na kumfanya kupooza toka kiunoni mpaka miguuni, bahati mbaya zaidi siku anapata ajali madaktari pale muhimbili walikuwa kwenye mgomo kkwahiyo alikuja kufanyiwa upasuaji after 3 days, hakupona mpaka leo yuko kwenye wheel chair. Huyu ni kijana, tena jembe haswaa, na mpaka sasa anaingia na wheel chair yake na anatibu watu na watu wanamkubali saaana, huyu bwana ana kila dalili kuwa akipata matibabu ya kiwango husika kuna uwezo mkubwa sana wa kuja kutembea na kulijenga taifa letu kwa kuboresha afya za watu. Amepeleka maombi ya kwenda India pale wizara ya afya lakini mpaka leo kimyaaa. Lakini hawa wenye nchi yao ni seconds tu mtu yuko India. Hivi hasira za watu wanaokosa tiba muafaka mnaionaje? ni kwanini wengine iwe rahisi hivi na wengine iwe balaa? Inabid uwe mwanasiasa ili upate kila kitu duniani smoothly, kwa yeyote mwenye password ya kuaccess njia za kumsaisia huyu bwana kwa kweli mchango wake utakuwa wa thamani sana.