Wanajamvi
Mimi kama mtanzania mpiga kura,nasikitishwa sana na kasumba tuliyoiendekeza ya viongozi wetu kupelekwa kutibiwa India huku sisi wapiga kura tunagombania panado katika hospital zetu.wakati wanatuomba kura walisema wanataka kututumikia na waliahidi kuboresha huduma za afya,najiuliza tu kuwa gharama zinazotumika kuwatibu,safari,masurufu n,k hazingetosha kuleta vifaa bora vya tiba na tukatumia madaktari wetu waliopo na kuwaboreshea maslahi.Huu ni uzembe mkubwa wa kufikiri wa viongozi wetu.
Nadhani ni wakati mwafaka na sisi wapiga kura tudai kupelekwa India kutibiwa tunapougua,kwani ndio tuliowaweka hao wanaopelekwa India kwa kodi zetu.
Nchi hii viongozi wameigeuza kama geto tu au chimbo la mavuno,then wanastarehe ulaya,tiba India,watoto masomo nje n.k
Ipo siku nasi tutalazimisha India na kama hawataki basi nao wasiende au tuwape hospitali zetu wahindi ili wote tutibiwe hapa nchini,imekuwa kasumba, mwenye safura India,surua India,Malaria nayo inataka kupelekwa India,mafua India,India! India! India! walalahoi kwenda India mpaka Uchangiwe kwa m-pesa wakati viongozi wanatanua kwa kodi zetu.
2015 kitaeleweka,sitamani ya Misri ila inauma sana.
am out!