samaki wa mbao
Member
- Apr 15, 2021
- 82
- 123
Amani na upendo kwenu nyote!
Kwanza nikiri wazi Mimi nimefanyakazi ktk kiwanda hiki katika vitengo mbalimbali jikoni, nondo na skrepa toka 2018 Hadi 2021 oktoba nikaacha kazi, jamaa na rafiki zangu wanaendelea kutaabika na kupata mateso mpaka sasa.
Katika kiwanda hiki Kuna MATESO NA UNYANYASAJI MKUBWA SANA KWA WAFANYAKAZI. Kiwanda hiki kinazalisha Nondo, kipo wilaya ya Mkuranga kata ya Vikindu ktk eneo la Kisemvule. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Wachina.
Wafanyakazi karibu vitengo vyote wanateseka sana, wachina wanatesa Sana wafanyakazi!
Kupigwa wafanyakazi, kukatwa mshahara, kunyimwa stahiki zao wapato Ajali na kufukuza hovyo wafanyakazi.
Kuhusu kupiga wafanyakazi hii ni kero kubwa sana hasa ktk kitengo cha jikoni na kitengo cha mafundi umeme.
Malalamiko yashapelekwa labour zaidi ya mara tatu, wamekuja Mara moja tu, baada ya hapo Hali ikaendelea vilevile, kibaya zaidi wale Wachina wakazidisha ukatili na wanajisifu wanatoa tu pesa na hakuna cha kuwafanya.
Wapo waliokatika mikono, miguu, na majeraha mengine lkn hawajapewa haki yao.
Tunaomba serikali iingilie kati haraka haya mateso na manyanyaso wanayopitia Watanzania wenzetu.
Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya ndani, Waziri wa kazi, Waziri wa Uwekezaji na mbunge wa Mkuranga Mheshimiwa Ulega mtusaidie , watu wanakuwa watumwa kwenye nchi yao.
Mchina wa umeme na jikoni ndo vinara wakutesa na kupiga wafanyakazi.
Uwekezaji na wawekezaji tunawapenda lkn haya mateso tunaomba sana yafanyiwe kazi.