Pwani: NEMC yawapeleka Wabunge kuona walivyodhibiti Moshi kiwanda cha Chuma cha LODHIA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Kamati ya Bunge Maji na Mazingira imetembelea Kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani Kuona wanavyoendesha shughuli zao kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira pamoja na kufuatilia hatua zilizochukuliwa kutoka kwao baada ya kupewa maelekezo na Serikali kuhusu maelekezo kadhaa ya utunzaji mazingira.
Screenshot_20231113-140040.png

Akizungumzia juu ya ziara hiyo ya Kamati ya Bunge Maji na Mazingira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Saidi Jafo ambaye naye aliongozana na Kamati, amesema lengo la ziara ni kuendelea kufanya uhakiki ili kuona maendeleo mbalimbali yanayozingatia matakwa ya utunzaji wa mazingira.

Amesema awali aliagiza mambo kadhaa katika kampuni hiyo ikiwemo kuhakikisha moshi hauwi kero kwa wakati, kutengeneza eneo kubwa kwa ajili ya kutunza chuma chakavu na utaratibu wa kuingiza chuma chakavu unaofuata Sheria.

“Nimetembelea kiwanda chao hiki na kile cha Arusha, wametekeleza maelekezo ya Serikali na wamezingatia utunzaji wa mazingira, natoa wito kwa wawekezaji wengine wenye viwanda wazingatie utunzaji wa mazingira.
Screenshot_20231113-140109.png

“Moshi unavyotiririka kwenda angani ndivyo ambavyo unasababisha ongezeko la joto, mkataba wa Paris unasema kuwa joto lisiongezeke isifike nyuzi mbili, joto linavyodhibitiwa ozone itabaki kuwa salama,” amesema Waziri Jafo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Anna Richard Lupembe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Maji na Mazingira amesema “Nampongeza Rais kwa mwendelezo wa kutoa fursa ndani ya Nchi yetu, tunaona jinsi ambavyo vifaa tulivyokuwa tukiagiza kutoka Nje, tunavipata kutoka ndani ya Nchi yetu.

“Kuna miradi mingi ambayo inalishwa na kiwanda kama hiki, tumekuta maagizo yametekelezwa.

“Kiwanda hiki kilikuwa kikitoa moshi sana, sasa hivi moshi sio kero kwa Wananchi, tunapenda mazingira ya viwanda yawe rafiki na jamii, baada ya Waziri Jafo kutoa maelekezo yamezingatiwa na kufanyiwa kazi.

“Wameajiri watu zadi ya 1,000 hiyo ni faida kwa Nchi, tunahitaji fursa kama hizi ziendelee kwa kuwa pia kuna uwekezaji unafanyika kwenye vyuo vya Veta na nimejulishwa kuwa Kiwanda hiki kina mpango wa kuajiri madereva Wanawake, hilo ni jambo zuri na fursa nzuri kwa Wanawake.”
IMG_20231113_141941_282.jpg

Upande wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Lodhia, Sailesh Pandit amesema anashukuru kutembelewa na Kamati hiyo pamoja na Waziri kuona maendeleo katika utunzaji wa mazingira kulingana na maelekezo waliyopewa.

Ukosefu wa Chuma chakavu (dongo) imekuwa ni changamoto kwani chuma chakavu kinatoshwa na kupelekwa nje ya nchi hivyo kiwanda kinakosa mali ghafi.

Akizungumza baada ya ziara hiyo amesema “Tuangalie upande wa mipaka ya Nchi kwa kuwa huko ndipo chuma chakavu kinapotorishwa.”

Kuhusu kiwanda chake amesema kimeajiri Watu 1,060 ambao ni Wazawa na kati yao Wanawake ni 167 na wana mpango wa kuongeza madereva Wanawake kutoka vyuo vya VETA.
 
Huyo waziri angewauliza wafanya kazi mshahara wanalipwa sh ngapi na mazingira yao ya kazi yakoje?

Isijekuwa kuna mambo yaliwekwa sawa kabla ya ujio wa waziri

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom