Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 370,438
- 857,729
Usiku huu, ulimwengu wa roho unashuhudia matembezi makali ya shetani na jeshi lake la mapepo, usiku unaoambatana na dhoruba za kila aina ya uharibifu ambapo mkuu wa giza anajipenyeza kama upepo wa sumu akitafuta milango ya fikra na ndoto zilizowazi ili kupandikiza mbegu za hofu ya kifo, magonjwa ya ghafla, na umaskini wa kutisha.
Ni majira ambayo nguvu za uchawi, majini ya baharini, na roho za fujo zinatumwa kuharibu amani ya nyumba, zikileta ndoto mbaya za kulishwa vitu usingizini, vifungo vya uasherati wa kiroho, na mawazo ya kukata tamaa yanayowafanya waamini walale na vinyongo, chuki, na hasira ili kupoteza baraka zote walizozipokea kanisani...!!!
Lakini katikati ya maharibu haya yote yanayorushwa kama mishale ya moto gizani, mamlaka ya Jina la Yesu na muhuri wa Damu ya Kondoo inasimama kama ukuta thabiti usiopenyeka, ikisambaratisha kila mkakati na ajenda ya adui, na kuacha anga lako likiwa salama chini ya ulinzi thabiti wa malaika wa mbinguni...