Matatizo ya vishikwambi vya walimu

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Kwanza niipongeze serikali kwa kutoa vishikwambi kwa walimu, Kuna ufanisi na urahisi Fulani wa kazi umeongezeka katika shughuli za kujifunza na ufundishaji..
mpaka Sasa nimekutana na zaidi ya vishikwambi 10 vya walimu hususani "PRITOM 10 MAX"
Na nimeona matatizo karibu sawa kama ifuatavyo..
1. Kugoma kuwaka... Kuna ambavyo Hadi leo havijawahi kuwaka Ile power button ni kama haifanyi kazi kabisa.
2. Kupoteza network.. hili limekuwa common yaani ghafla tu kishikwambi ni NO SERVICE na hata maeneo Yale Yale ambayo mwanzo ulikuwa unapata mtandao
3. Kugoma kusoma line, hapa pia Kuna vingine line mpaka urudie rudie kuweka kama mara 5 hivi ndio ikubali ..
4. Camera mbovu.. usitegemee kupiga document kwenye camera ya kishikwambi ikatoka inasomeka... Sahau

Hayo ni matatizo ambayo walimu wengi wamekutana nayo..
Lakini kwa upande mwingine viko poa kwenye...
1. Kukaa na chaji.. hapa Sina neno.
2. Inaruhusu kasi ya 4g na kwenye net hakina shida
3. Gb 60+ storage sio haba kuweka mafaili n,k
Asante
 
kama umezoea smartphone yako ya laki 2 mwalimu ni ngumu sana kutumia na kukizoea kishkwambi.

ukikiona kwa nyuma unawezadhania ni kifaa cha maana sana,ukiisha kigeuza mbele ktk screen hata haya uliyoyaandika hapa hutashangaa kukutana nayo.

ni jambo gumu sana nchi hii kununua kitu bora kwa matumizi ya serikali ni kwenye magari tu
 
Kikivunjika kioo hv vina replacement kweli? kuna mdogo wangu huko mtwara mwanae kashafanya yake
 
Unesahau screen kuzima ghafla mkuu vile vidubwana ni fake kuliko fake yenyewe..
Ni vile tu waalimu hawajui mambo ta tech hivyo wanabeba tu ..
Serikali ta Tz kwenye magari ya kifahari tu ndo wanaweza mana hata ndege na treni wameshidwaa.
Hata bandari wameshidwaa
 
kama umezoea smartphone yako ya laki 2 mwalimu ni ngumu sana kutumia na kukizoea kishkwambi.

ukikiona kwa nyuma unawezadhania ni kifaa cha maana sana,ukiisha kigeuza mbele ktk screen hata haya uliyoyaandika hapa hutashangaa kukutana nayo.

ni jambo gumu sana nchi hii kununua kitu bora kwa matumizi ya serikali ni kwenye magari tu
Kabla hawajaleta hivi vya "ZTE Blade X10S" yani hivi vya sensa walimu wakuu walikuwa wanatumia Samsung Galaxy Tab A10.1 (2016). Kwa kweli ukiachana na RAM na Storage, vishikwambi vya kwanza vilikuwa vizuri kushinda hivi vya sasa.
Hivi vya sensa nilivishika mara kadhaa aisee vina display mbovu sana. Nimefuatilia mtandaoni naona vina 150ppi ila mwanga ni hafifu mno na rangi zimepauka, sijajua kuhusu kamera ila nina uhakika itakuwa ni ukungu tu

Kama serikali inataka kutoa tablet nzuri za bei rahisi ni heri hata wangewapa tablet kama Redmi Pad au hizi Lenovo na Realme za bei rahisi. Au hata Samsung Galaxy Tab A model za 2017 kuliko huu upuuzi wa sasa

Hata Amazon Fire HD 10 ina afadhali
 
Back
Top Bottom