Matarajio. . . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,778
59,133
Unrealistic expectations are planned resentments.

Kila mtu anapoingia kwenye mahusiano/ndoa anakua na matarajio yake. Wapo wenye matarajio ambayo napenda kuyaita "reasonable/realistic" na wengine wana matarajio ambayo ni "unrealistic".

Realistic:
. . . Nampenda nae ananipenda ila migongano ya hapa na pale haitokosekana - TUTAITATUA PAMOJA.
. . . Ananifurahisha nami namfurahisha ila kuna wakati tutakasirishana - TUTASHIRIKIANA KUITAFUTA HIYO FURAHA TENA.
. . .Napenda/nafurahia uwepo wake nae wangu ila kuna wakati tutachokana - NI JUKUMU LETU KUTAFUTA NAMNA YA KURUDI KWENYE HALI HIYO.
. . .Maisha sio mabaya ila kuna wakati mahitaji yanaweza yakazidi uwezo - TUTAKABILIANA NA HALI HIYO PAMOJA.
. . .Tuna afya ila magonjwa/ajali zaweza tokea - TUTASIMAMA PAMOJA.
. . . Tutabadilika kadiri muda unavyoenda (muonekano, fikra, mazoea n.k) - TUTAJITAHIDI TUENDANE NA MABADILIKO YA KILA MMOJA WETU.
N.k. . . . . .

Unrealistic:
. . . Ndoa/mahusiano ndio mwisho wa matatizo yangu ya kifedha.
. . . Ana gari sitokaa nipande daladala tena.
. . . Kila siku tutakua tunacheka na kufurahi pamoja.
. . . Aliyonivutia nayo yote yataendelea kuwepo.
. . . Yeye ndie mtoaji mimi ni mpokeaji tu.
. . . Hamna mawazo ya yanayoweza kutokea na kubadili kila kitu mf. matatizo ya kifamilia na magonjwa.
N.k. . . . .

Matarajio unayokua nayo wakati unaingia kwenye mahusiano yana nafasi kubwa sana katika kustahimilisha mahusiano yako, pia hisia/mapenzi uliyonayo juu ya mwenzi wako.

Unapokua unaelewa kuwa maisha ndani ya mahusiano yako hayatokua mteremko kila siku, ukaelewa kwamba kutakua na milima, mabonde na viunzi basi unakua umejiandaa kifikra namna ya kukabiliana na vikwazo vyovyote vinavyoweza kutokea. Badala ya kulaumu na kulalamika unasaidiana na mwenzi wako kukabiliana na matatizo yenu. Kinyume cha hapo, utajikuta unamchukia mwenzi wako kwa kushindwa kutimiza/fikia matarajio yako ambayo hayakua yamekaa kihalisia toka mwanzo. Hii inatokana na wewe kuishi katika ulimwengu wa kufikirika huku ukijivua uwajibikaji linapokuja swala zima la kufikia matarajio yako na kumvisha mwenzi wako kana kwamba yeye anaweza kucontrol kila kinachotokea. Kwa style hiyo utajikuta unaingia na kutoka katika mahusiano kwa sababu zile zile kila mara.

Kuwa na matarajio yaliyokaa kiuhalisia ili kupunguza kama sio kuepuka kabisa disappointment.
 
mie naona ingekuwa simple kama wanwawake wangeingia kwenye relationship wakijua kuiwa guys would love free kitumbua any time of the day so women should also luk for free muhogo
 
i am sorry to say this..

hiyo orodha yako ya unrealistics

ndio matarajio ya 99 percent ya wanawake wa TZ.............

hapana, labda uwe unawazungumzia wanawake wa Dar es salaam, na penyewe bado si asilimia 99

Asilimia kubwa ya watanzania wanashi vijijini kusiko na maisha mazuri,hali ya kilimo ni mbaya,ajira hamna,vifo ni vingi,hizo unrealistic expectation wanazitoa wapi?? Manake expectation zinatokana na mazingira unamoishi na exposure yako...sasa kwa hali anayopitia tangu utoto hadi anafikia ndoa na kwa aina ya wanaume waliomzunguka ambao ndo potential husbands,hawawezi kuwa na hizo unrealistic expectation kwa kiasi kikubwa hivyo....halafu hapo hujaweka wale wanaoolewa kisa tu umri umeenda anakubali yeyote,kapewa mimba anaolewa tu ili mradi etc....99% is not realistic

Haya ukija wasichana wa mjini,wengi wanasoma,wanafanya kazi,biashara, na wanauelewa na hali halisi inavyobadilika kila siku ya kiuchumi as wanajitegemea kabla ya ndoa....iweje nao wawe kwenye asilimia 1 wote hao,haiwezekani kabisa....usitu-underestimate kiasi hicho....wanawake wanauelewa wa uhalisia wa maisha ya ndoa kuliko hata wanaume na waga wako tayari kukabiliana na changamoto na ndo maana sisi ndo tunapigana kufa kupona kulinda ndoa zetu.
 
Realistic:
. . . Nampenda nae ananipenda ila migongano ya hapa na pale haitokosekana - TUTAITATUA PAMOJA.
. . . Ananifurahisha nami namfurahisha ila kuna wakati tutakasirishana - TUTASHIRIKIANA KUITAFUTA HIYO FURAHA TENA.
. . .Napenda/nafurahia uwepo wake nae wangu ila kuna wakati tutachokana - NI JUKUMU LETU KUTAFUTA NAMNA YA KURUDI KWENYE HALI HIYO.
. . .Maisha sio mabaya ila kuna wakati mahitaji yanaweza yakazidi uwezo - TUTAKABILIANA NA HALI HIYO PAMOJA.
. . .Tuna afya ila magonjwa/ajali zaweza tokea - TUTASIMAMA PAMOJA.
. . . Tutabadilika kadiri muda unavyoenda (muonekano, fikra, mazoea n.k) - TUTAJITAHIDI TUENDANE NA MABADILIKO YA KILA MMOJA WETU.
N.k. . . . . .

You get my standing ovation for this one.

Ukimpata anayefikiria hivyo jua huyo ni tunu!
 
i am sorry to say this..

hiyo orodha yako ya unrealistics

ndio matarajio ya 99 percent ya wanawake wa TZ.............

99% ni kubwa sana Boss, though nakubali kwamba hao ni wengi kuliko wenye matarajio yanayoendana na uhalisia wa maisha na mahusiano.
 
Nakubaliana na wewe kwamba unapokuwa na matarajio ya kiuhalisia basi uwezekano wa kumudu kuwa na uhusiano mzuri na wenye kuhimili mikikimikiki ya maisha ni mkubwa, zaidi ya hayo ni vizuri kujishughulisha kwenye maisha na kuacha utegemezi...itapunguza dissapointments kwenye mahusiano....na kuacha utegemezi nikimaanisha kuanzia ule wa kuamini bila fulani mis sina raha au maisha hadi ule utegemezi wa kifedha....!!
 
Well said Lizzy, lakini pia naomba kuongezea hii kitu ya peer pressure ambayo ina influence matarajio ya akina dada wengi.

Hawa sasa ndio wale tunawaita vichwa panzi, wanafanya wanayoona wengine wanafanya au wanayosukumwa kufanya, matokeo yake leo na kesho maisha na mahusiano yake yanakosa muelekeo unaoeleweka.

@Dearest kweli Boss kachakachua matokeo. Ila kuna wasomi waliopita madarasa tu bila kuelimika, matarajio yao sio madogo.
 
...nilipooa, matarajio yangu yalikuwa nitaishi nae, nizae nae mtoto/ watoto...
sikujua kwenye ndoa kuna zaidi ya hayo mawili....

...matarajio uliyoyaweka [ambayo ni general] yanapimwa na matukio na mabadiliko mbali mbali
baina ya wawili waliooana kila siku, kila wiki, kila mwezi, kila mwaka...

ukisikia 'wale' wameachana sababu ya "irreconciable differences," usidhani hawakuwa na matarajio mwanzoni...
ni "mitihani" tu ya maisha ya ndoa.
 
Nakubaliana na wewe kwamba unapokuwa na matarajio ya kiuhalisia basi uwezekano wa kumudu kuwa na uhusiano mzuri na wenye kuhimili mikikimikiki ya maisha ni mkubwa, zaidi ya hayo ni vizuri kujishughulisha kwenye maisha na kuacha utegemezi...itapunguza dissapointments kwenye mahusiano....na kuacha utegemezi nikimaanisha kuanzia ule wa kuamini bila fulani mis sina raha au maisha hadi ule utegemezi wa kifedha....!!

Utegemezi ni mbaya kuliko haya dearest, wenyewe unaweza ukampelea mtu kufanya mambo ambayo hapendi wala hakuwahi kufikiria, kubaki kwenye mahusiano/mtu asiemtendea haki ili tu asipoteze hicho anachotegemea (fedha, hisia, fikra n.k)
 
labda kama ni short term relation
long term relation lazima kutakuwa na responsibillities

mie naona ingekuwa simple kama wanwawake wangeingia kwenye relationship wakijua kuiwa guys would love free kitumbua any time of the day so women should also luk for free muhogo
 
...nilipooa, matarajio yangu yalikuwa nitaishi nae, nizae nae mtoto/ watoto...
sikujua kwenye ndoa kuna zaidi ya hayo mawili....

...matarajio uliyoyaweka [ambayo ni general] yanapimwa na matukio na mabadiliko mbali mbali
baina ya wawili waliooana kila siku, kila wiki, kila mwezi, kila mwaka...

ukisikia 'wale' wameachana sababu ya "irreconciable differences," usidhani hawakuwa na matarajio mwanzoni...
ni "mitihani" tu ya maisha ya ndoa.

Mbu matarajio yapo kwa kila mtu, swali ni je yalikua realistic or not? Hata kupanga tutazaa bila kufikiria uwezo huo mnaweza msiwe nao kunanyima tarajio hilo uhalisia, na ndio maana tunasikia watu wananyanyasana/chukiana au hata kuachana kisa hawajajaaliwa mtoto.
 
mimi kuna kitu ambacho wanawake wanacho ambacho kinanifanya
niwe pessimistic na wanawake saana

naacho ni kuwa 'emotional....na maamuzi'

hasa 'revenge tendencies'

na kutaka 'ku replace their bad feelings so fast' kiasi

akiwepo mtu pembeni wa ku 'trigger tu' hizo feelings baasi.....
 
Back
Top Bottom