Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Tunajua fika CHADEMA na Act wazalendo ni vyama ambavyo kwa ushahidi wa wazi kabisa ambao hauna chembe kuwa ni vyama vya wasaka matonge. Wao kuweka pesa mfukoni ndio lilikuwa jambo la kwanza kuliko maslahi ya Tanzania na raia wake.
Tulishuhudia Zitto Kabwe akizurula Ulaya na Usa na kunadi kuwa hakuna demokrasia nchini,na hata haki ya watoto wa kike kusoma wakiwa na mimba inaminywa,akaandika barua tunyimwe mkopo. Hakuwa na muda wa kutumikia wananchi wa Kigoma, muda wote alikuwa anazurula nje ya nchi kusaka ufadhili wa mabeberu ili ajinufaishe kwa madai ya kutetea demokrasia kama vile Tanzania hakuna Demokrasia.
Chadema wao ndio wananchi walisha wachoka na siasa zao za kishamba za harakati zisizo na mashiko, kudai maandamano, kuvamia magereza, kupinga maendeleo ya wananchi huku nao wanayafaidi, wananchi waliwachoka hata kabla ya kupiga kura. Na kwenye boksi la kura wamepata wanacho stahili.
Act wazalendo na Chadema walizoea kupata ruzuku na michango ya wananchi bure kabisa, sasa kimoja kimekufa mende style hakuna ruzuku ya mil 360, hakuna michango ya wabunge zaidi ya mil 100 kwa mwezi.
Kilichobaki wanasaka msaada kwenye tuta, Eu iinyime misaada Tanzania ili wao wafurahi! Watanufaika nini? Tril 2 ambazo ni msaada wa EU kwa Tanzania mimi naona ni kitu kidogo sana kwa nchi ambayo inakusanya tril 1.5 kwa mwezi, achana na mapato mengine.
Watanzania tunajua siasa ni mtaji wenu, mlikuwa mnakula kwa kupitia vyama vyenu sasa wananchi wamewakataa, kuomba dua mbaya kwa Tanzania ni kupoteza muda.