Matangazo ya TV yanachanganya sana

kaisa079

Member
Nov 16, 2007
20
20
Kweli nakubali kwamba sisi ni masikini sana na ili vyombo vya habari vijiendeshe vinahitaji fedha ambayo inatokana na matangazo,kinachoniudhi na kunikwaza ni pale ambapo unaangalia TV mara linatokea tangazo la sabuni mara 'Revola ni sabuni nzuri' baada ya dakika mbili unaona'Protex hulinda ngozi yako' kidogo tu unaona'Rungu ni sabuni bora' mara geisha mara sijui nini au katika mitandao ya simu ,ohh 'Vodacom inaongoza kidogo tu Celtel imeenea mara kidogo tu 'Tigo viwango nafuu' yaani ndani ya nusu saa matangazo kibao yote yanatangaza huduma moja sasa sisi watazamaji hasa mimi nashindwa kufanya uamuzi kipi bora,mimi nadhani vyombo vya habari vingekuwa na policy kama wanaamua kupromoti Revola au Tigo iwe ni siku nzima kama ili kuepuka kutuchanganyachanganya hivi.Hoja iko wazi kujadiliwa.
 
Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,338
1,250
ndo maana halisi ya matangazo ya biashara hiyo mzee na ndo raha ya freedom ya medias....
 
Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
1,250
Kweli nakubali kwamba sisi ni masikini sana na ili vyombo vya habari vijiendeshe vinahitaji fedha ambayo inatokana na matangazo,kinachoniudhi na kunikwaza ni pale ambapo unaangalia TV mara linatokea tangazo la sabuni mara 'Revola ni sabuni nzuri' baada ya dakika mbili unaona'Protex hulinda ngozi yako' kidogo tu unaona'Rungu ni sabuni bora' mara geisha mara sijui nini au katika mitandao ya simu ,ohh 'Vodacom inaongoza kidogo tu Celtel imeenea mara kidogo tu 'Tigo viwango nafuu' yaani ndani ya nusu saa matangazo kibao yote yanatangaza huduma moja sasa sisi watazamaji hasa mimi nashindwa kufanya uamuzi kipi bora,mimi nadhani vyombo vya habari vingekuwa na policy kama wanaamua kupromoti Revola au Tigo iwe ni siku nzima kama ili kuepuka kutuchanganyachanganya hivi.Hoja iko wazi kujadiliwa.

Nafikiri hii inatokana na ubovu wa marketing strategies za hizo kampuni. Vodacom inaponunua commercial airtime, inatakiwa ihakikishe inachagua muda ambao hauko karibu na Celtel or Tigo. Kazi ya marketing team ni pamoja na ku-monitor running ads. Kwa hiyo, huu ni uzembe wa marketing team wa hizi kampuni na sio Tv.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom