Mr. Samson
Member
- Feb 16, 2013
- 38
- 13
Nionavyo mimi,suala la 'nani achinje kitoweo cha nani' linalazimishwa na watu wachache, wapenda vurugu kuwa la kidini. Kwa hakika nijuavyo mimi,hakuna dini inayomtaka muumini wake amlazimishe mtu asiye wa imani hiyo kufuata misingi au kanuni na sheria za dini yake, tena kwa ncha ya upanga na kumwaga damu! Kama ipo nathubutu kusema, 'si dini ya Mungu!' Aidha serikali kwa upande wake, iache kuonesha upendeleo au udhaifu kama inavyoshuhudiwa katika tukio la Geita.
Dini ya kiislam kama inamtaka muumini wake kutokula mnyama aliyechinjwa na mtu asiye muislam, basi muislam ni wajibu wake kuhakikisha anatafuta mchinjaji wake anayemwamini, na si kulazimisha watu wote kumwamini mchinjaji wake pekee. Kila mtu ana haki na uhuru wa kuabudu anachokiamini bila kuingilia uhuru wa watu wengine.
Mambo haya yakiachwa yaendelee, si ajabu siku moja wasabato (SDA) nao wataamua kupiga marufuku kambale kuuzwa sokoni, na kuanza kukata mapanga watu ovyo, kwani kwa imani yao, kambale ni haramu!
TAFAKARI HOJA YANGU KABLA HUJANIHUKUMU!