Omulangi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 1,036
- 267
Katika misiba ya watumishi wa Mungu Mch Mathayo Kachira Buselesele na Askofu Thomas Laizer Arusha matamko mawili ya mabaraza ya wakristo yaani CCT na PCT yametolewa yakiweka wazi msimamo wa jamii ya wakristo kuwa kuanzia sasa wakristo watachinja kitoweo chao. Kwa vile sasa imeonekana suala la waislamu kuchinja ni ibada yao, wakristo hawatashiriki katika ibada isiyo wahusu.
Jambo hili ni muhimu tulifikiri na kujadili mapema maana linaamua mustakabali wa jamii ya watanzania. je hotel zitakuwa labelled kama zina nyama iliyochinjwa kiislamu au kikristo? Na vipi katika sherehe za pamoja zitakuwepo buffet mbili moja ya nyama iliyochinjwa na waislamu na nyingine wakristo? Naona media zinajitahidi jambo hili lisizungumzwe wala kutangazwa maana tv zote tangu jana zinakwepa kulizungumzia. Mimi naona hii ni hatari zaidi!!!