Cardinal Polycap Pengo,aliwahi kukemea sana CCM isiibe kura za Cuf Zanzibar enzi za
awamu ya Mkapa.Ila nadhani mnachoshindwa kujua ni kwamba adui wenu mkubwa ni Ujinga mlonao.Mafisadi wa CCM ambao ni Waislam kama,Makamba, Rostam,Nazir K,Jk etc hutumia dini kuwagawanya ili waendelea kuwanyonya kupita mikataba feki. Alafu hawa hawajengi wala kuchangia ujenzi wa hospitali na shule za Kiislam badala yake huwa wanawapikia Pilau na chai,na tende kidogo kwisha habari yenu.wenzetu waikristo wakiwa bize na harambee za ujenzi wa shule na hospitali.
Mnahitaji maombezi mtolewe pepo la "ulalamishi". Kikwete Wanae wanasoma shule za Kiikristo(Katoliki) anaelewa sana Uwezo mzuri wa shule hizi angalia matokeo ya Form IV 2010 na Kikwete hana udini ila anataka awalaghai mgawanyike ili msahau shida tulonazo muweze kutawalika vizuri.
TAMKO LA WAISLAMU DHIDI YA KAULI ZA MAASKOFU
Utangulizi
Oktoba 31, 2010 Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi walipata fursa ya kumchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani. Katika uchaguzi huo, Watanzania kwa ujumla wao walikichagua Chama cha Mapinduzi, CCM, kuongoza tena nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Hata hivyo, wakati wananchi wakiamini kwamba wanaongozwa na watu waliowapigia kura, matukio yanayoendelea hivi sasa yanaashiria serikali kutelekeza majukumu yake na kuwaacha maaskofu wakielekeza nchi wanakotaka.
Itakumbukwa kwamba awali kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walikuwa wametoa Ilani yao ya uchaguzi bila kueleza kipi chama chao kitakachosimamia na kutekeleza Ilani hiyo. Baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala, CCM, walishabikia Ilani hiyo na kuwatetea maaskofu. Kwa hakika taarifa za vyombo vya habari zilifahamisha kwamba baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya serikali walishiriki katika kuandaa Ilani hiyo.
Ilipofika wakati wa kampeni hadi kuingia siku ya kupiga kura, ilikuwa imedhihiri kipi kilikuwa chama cha maaskofu ambacho walitarajia kitekeleze Ilani yao. Haikuwa tena jambo la siri kwani walisimama wazi wazi kuwaelekeza waumini wao wampigie nani kura. Na katika juhudi zao za kutaka wafuasi wao wawaelewe vizuri, maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha binafsi ya ndoa ya mgombea.
Hata hivyo, matokeo ya kura yalitoa majibu kwamba Watanzania walikuwa wameikataa Ilani ya Maaskofu.
Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kunyenyekea kwa maaskofu hao.
Tumeona na tumemsikia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akihangaika kuwapigia magoti na kuwaomba radhi maaskofu kule Sumbawanga. Tumesikia jinsi viongozi wanaojaribu kuwaambia maaskofu kwamba kama wanataka kuingia katika siasa wavue majoho na vyeo vyao vya kikanisa kama Padiri mwenzao waliyekuwa wakimpigania kuingia Ikulu, wanavyokemewa na kutakiwa wawaombe radhi maaskofu hao.
Lililo baya zaidi maaskofu walioshindwa kuwashawishi wananchi waipokee na kukubali Ilani yao, wamekuja na kampeni za kuchochea uasi kwa serikali iliyopo madarakani. Lakini pamoja na hali hiyo, viongozi wa CCM na serikali wamebaki wanagwaya. Hakuna aliyeweza kupata ujasiri wa kukemea hali hii. Kinyume chake Waziri Mkuu na Mzee John Samwel Malecela wanahangaika huku na kule wakiwapigia magoti maaskofu hao na kuwakemea wanaothubutu kuwakosoa.
Hali kama hii ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. Ni hali ya kuchochea udini na kuweka ombwe la uongozi wa kisiasa ambao utazua balaa. Waislamu hatuwezi kukubali hali hii. Kwa hiyo, ama CCM na serikali vitekeleze wajibu wao wa kuongoza au kama wanaona hawawezi, basi waseme rasmi ili Maaskofu na wengine wenye Ilani zao za uchaguzi waingie tena ulingoni kuomba ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi kuliko kuishi katika hiki kiini macho ambapo maaskofu na mawakala wao ndani ya serikali wameachwa waikokote nchi wanakotaka.
Kiini cha Hali hii ya Kisiasa
Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni watawala wapewe elimu ya juu na wanfundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda kuuana.
Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa jukumu la kuwaelimisha Waafrika likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..
Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake, baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary Tanganyika, March-April 1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. Na ni mkakati huu ndio ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimuhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mtakatifu!
Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui hao.
Matokeo ya Hujuma Hizo
Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali kabla na baada ya Uhuru. Ifuatayo ni mifano michache tu ya baadhi ya hujuma hizo baada ya Uhuru.
(1) Mwaka 1963 katika Barua ya Kichungaji, Kanisa Katoliki lilisema Waislamu walikuwa wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao, jambo ambalo ni hatari kubwa kwa hatima ya Wakristo wetu na Sivalon anabainisha kuwa Wakristo walimwomba Nyerere awasaidie kuvuruga umoja huo wa Waislamu. Ndio sababu ya Nyerere kutumia dola kuiparaganya EAMWS. Kwa kuwa Waislamu ni jamii inayotakiwa kuwa dhalili, hawatakiwi kuwa na umoja. Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao. Katika taifa moja haki hiyo ni ya Wakristo peke yao. Sote ni mashahidi kuwa mwaka 1994 serikali ilimwagiza Naibu Waziri Mkuu Mh. Augustino L. Mrema kuhakikisha kuwa Bakwata inapitisha katiba mpya inayotakiwa na serikali. Na Maaskofu wakachangia gharama. Waislamu ni maadui kidini na kisiasa, lazima wadhibitiwe.
(2) Mwaka 1992 Serikali ya Tanzania ilitiliana saini Makubaliano ya Itifaki rasmi na Makanisa ya TEC na CCT. Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye wakati huo alikuwa Mh. Edward Lowasa serikali imewajibishwa pamoja na mambo mengine, kutenga nafasi za masomo kwenye vyuo vyake vya Ualimu mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wanaopangwa kufundisha katika shule za Kanisa; pia kutoa ruzuku ya kuendeshea taasisi za Makanisa. Kuanzia 1992 hadi leo serikali imetoa mabilioni ya kodi za wananchi kwa Makanisa. Katika kipindi chote hicho Waislamu wamepinga ubaguzi huo. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwaimarisha Wakristo ambao ni jamii inayotakiwa kupewa nguvu zaidi dhidi ya jamii ya Waislamu ambao wanatizamwa kama maadui, serikali imeyapuuza malalamiko ya Waislamu. Lakini propaganda zinaendelea kuwa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na ni kisiwa cha amani.
(3) Waislamu wameiomba serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo itakayowezesha nchi yetu kupata misaada itakayotumika kuinua hali za Waislamu ambao wameachwa nyuma sana katika elimu na uchumi. Makanisa yote kwa kauli moja yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hilo. Sababu ya kupinga kwao ni kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu maadui hao. Serikali ilipofanya utafiti wake wa kina ikajiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote. Na Mh. Bernard Membe alitamka hilo Bungeni. Mara akaitwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Cardinali Pengo na kukumbushwa mkakati wa kuwadhoofisha Waislamu. Msimamo wa serikali ukabadilika. Lakini propaganda za kuwazuga Waislamu zinasema Watanzania wote ni kitu kimoja na nchi hii haina ubaguzi!
(4) Kwa kuwa tangu wakati wa ukoloni hadi leo mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanaminywa kadiri iwezekanavyo katika nafasi za uongozi na ajira, ndio maana hadi leo, miaka 50 baada ya Uhuru Waislamu ni wachache sana katika nafasi zote za uongozi na ajira katika sehemu muhimu serikalini na katika vyombo muhimu vya maamuzi. Kisingizio kinachotolewa ni kuwa Waislamu hawataki kusoma. Lakini ukitazama orodha ya Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa na sifa zao, utaona dhahiri kuwa wapo Waislamu wengi wenye sifa bora zaidi ambao wangestahili kuwa ma-DC. Waislamu hawateliwi kwa sababu mkakati uliopo ni kuwatenga Waislamu na ikiwezekana kuwaondosha kabisa katika sehemu muhimu za uongozi, kwa sababu kama wao hawajui ukweli ni kwamba hawatakiwi kushika nafasi zozote muhimu za uongozi au ajira. Ndio maana asilimia 75 ya Ma-DC wote ni Wakristo na karibu wasimamizi wote wa Uchaguzi katika wilaya ni Wakristo. Wabunge asilimia 75 pia ni Wakristo, na hali ni hiyo hiyo katika Vitengo vya serikali na Mashirika ya uma. Ndio maana hakuonekani tatizo lolote pale taasisi yote inapokuwa na Wakristo watupu. Na kelele nyingi maadui wa serikali na Kanisa wanapopewa nafasi hata kama wana uwezo kiasi gani. Katika sura ya nje Tanzania ni taifa moja, katika uhalisia wake ni kuna mataifa mawili, moja nyonge na jingine lenye nguvu.
(5) Kwa kuwa Waislamu wanahesabiwa kuwa ni maadui, ule mkakati uliowekwa na wakoloni wa kuwawekea vikwazo Waislamu katika kutangaza dini yao unaendelea hadi leo. Ipo mifano mingi sana ya Waislamu kukamatwa, kutiwa ndani na kunyanyaswa na vyombo vya dola kwa sababu tu ya kulingania hadharani dini yao. Kwa kuwa Waislamu ni maadui, basi ni muhimu kuhakikisha kuwa hawaongezeki. Wakristo wanayo haki ya kuitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa Yesu ni Mungu. Wao ni jamii inayostahiki ulinzi wa dola. Lakini pindi Mwislamu atakaposema hadharani kuwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi siyo Yesu mwana wa Mariamu atakuwa amekashifu dini ya dola na atakamatwa na kubughudhiwa. Lakini kipropaganda, Tanzania ni nchi moja na inafuata katiba moja. Lakini uhalisia ni tofauti.
(6) Msimamo wa serikali na makanisa kuhusiana na mauaji ya Waislamu katika msikiti wa Mwembechai ni kielelezo kingine cha ukweli kuwa Tanzania ni mkusanyiko wa jamii mbili zenye haki na hadhi tofauti katika taifa moja. Kwa kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na hatia yoyote. Waislamu waliiomba Mahaka, Bunge na hata Rais aunde Tume ya uchunguzi. Mihimili yote ya dola ilikataa. Kiongozi wa Kanisa Katoliki akenda mbali zaidi. Akahalalisha mauaji hayo. Kwa sababu waliouliwa ni wale maadui wa ile jamii nyoge isiyotakiwa kustawi. Lakini alipouliwa mbwa Imigresheni mwaka huo huo wa 1998, Jaji Mkuu wa wakati huo Mh. Francis Nyalali aliamuru uchunguzi wa kuuliwa mbwa huyo na hakimu akaadhibiwa. Jaji Mkuu alichukua uamuzi huo bila kuombwa na mtu. Lakini wale waliowauwa Waislamu walipongezwa na kupandishwa vyeo. Uhasama wa serikali na makanisa dhidi ya jamii ya Waislamu ni wa kiwango cha kutisha. Msimamo ukawa huo huo walipouliwa Waislamu Unguja na Pemba 2001 kwa kuandamana kudai Katiba Mpya. Lakini kipropaganda tunaambiwa Watanzania wote wanahaki sawa.
(7) Rais wa Marekani George W. Bush alipotangaza Vita vya Msalaba dhidi ya Waislamu mwaka 2001, serikali ya Tanzania ikapata uhalali zaidi wa kuzidi kuwakandamiza Waislamu. Serikali ikawa radhi kuvunja Katiba ya nchi kwa kupitisha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002 ili zipatikane fursa zaidi za kuwanyoongesha Waislamu. Waislamu waliipinga sheria hiyo kwa nguvu zao zote, lakini kwa kuwa wao ni jamii inayotakiwa kupigwa vita hawakusikilizwa. Bunge ambalo nalo lina Wakristo wengi likaipitisha haraka sheria hiyo. Naam, tangu imepitishwa hadi leo, sheria hiyo imetumika kuwadhuru Waislamu wasiokuwa na hatia yoyote, na kufunga taasisi zilizokuwa zikiwasaidia Waislamu. Misaada ni haki ya Wakristo, siyo Waislamu. Pamoja na madhila yote hayo Waislamu wanatakiwa waendelee kuamini kuwa Tanzania ni nchi moja inayojali raia wake wote.
(8) Wakati serikali ikidai kuwa Tanzania ni taifa ambalo raia wote wana haki sawa, lakini serikali hiyo hiyo kwa makusudi kabisa inafanya jitihada za waziwazi za kuwahamasisha Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni maadui zao na maadui wa taifa lao. Januari 2001 Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa serikali inazo taarifa kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na magaidi hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli hiyo Waislamu watatu wa Muhimbili ambao ni Waislamu akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa mbaroni. Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lengo la serikali la kupandikiza sumu ya chuki lilikuwa limetimia. Tarehe 24 Agosti 2001 Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali kupitia jeshi la polisi likawatangazia wananchi wote kuwa Waislamu wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na serikali ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na hiyo shari ya Waislamu. Lengo la uzushi huu ni kuwachochea Wakristo wawachukie Waislamu na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwapa kipondo. Hivi sasa huo umekuwa ni mchezo wa kawaida. Kila baada ya muda Fulani serikali kwa kpitia jeshi la polisi hutoa taarifa za kuonesha kuwa kuna mpango wa shambulio la kigaidi. Na watuhumiwa siku zote ni Waislamu. Serikali na makanisa yanawachukia Waislamu kiasi cha kuwa tayari kushirikiana na wasiokuwa Watanzania katika kuwahujumu Waislamu. Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, Maaskofu wakipata kisingizio chochote watakuwa tayari kuwauwa Waislamu kama walivyoshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda.
(9) Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania. Katika ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita [Commission of Armed Forces] ndani ya Kanisa hilo. Tangu wakati huo hadi leo Waislamu wameitaka serikali iwaondoshe hofu kwa kuweka wazi kazi za Tume hiyo ya Majeshi ya Kivita ndani ya Kanisa. Serikali haijajibu na wala haijajishughulisha na taarifa nzito kama hizo. Hatujui kama Tume hiyo ya Majeshi ya kivita inafanya kazi ndani ya Jeshi la Wananchi au nje ya jeshi hilo. Lakini kwa muktadha wa hali ya uhasama wa serikali na hasa wa Maaskofu dhidi ya Waislamu wanaowahesabu kuwa ni maadui zao, si vigumu kukisia kwa nini Kanisa Katoliki limeunda Tume ya Majeshi ya Kivita. Lakini serikali ambayo haishughulishwi kabisa na Tume ya Majeshi ya Kivita ya Wakatoliki imekuwa na tabia ya kuwakamata na kuwatia ndani Waislamu kwa kesi za kuwabambikia zisizokuwa na kichwa wala miguu. Lakini propaganda zinasema Tanzania ni nchi moja yenye katiba inayolinda haki za watu wote. Mwenye mach haambiwi tazama.
Dalili ya Mvua ni Mawingu
Alipokuwa akitoa mada yake juu ya Mifumo ya Viashiria vya Migogoro katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ulioandaliwa na REDET mwaka 2003, Mh. Bernard L. Membe alisema kwamba migogoro mingi duniani na hasa vita vya wenyewe kwa wenyewe vina dalili na viashiria vyake. Akasema miongoni mwa dalili kubwa kuwa nchi karibu itaingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kutokea kwa mgawanyiko au kutokea kutoelewana kwa viongozi ndani ya chama au serikali tawala.
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri wakipingana hadharani juu ya maamuzi waliyoyafanya wenyewe. Lakini pia katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia pia mgongano wa waziwazi kati ya wabunge wa CCM na Chama chao. Na wote hao hawachoki kujisifu kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini mwaka 1993, Nyerere katika Kitabu chake Tanzania! Tanzania! Aliandika na tunanukuu:
Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hoja ya hadhi ya Bunge. Ni nani huyu anayefanya kazi hii? Ni haki kabisa ya vyama vya upinzani kujaribu kugombanisha Wabunge wa chama kinachotawala na chama chao. Lakini viongozi wa chama kinachotawala pamoja na Serikali yenyewe wanapojaribu kufanya mambo ambayo yatagombanisha Wabunge wa CCM na chama chao, tuna haki ya kuwauliza viongozi hao wanafanya kazi hii kwa niaba ya nani, na chama chao ni chama gani? [uk. 41]
Pamoja na kuyajua yote hayo hivi sasa kuna msuguano ulio dhahiri kabisa baina ya Wabunge wa CCM na Chama chao. Kiashiria kingine alichokitaja Mh. Membe ni kwa serikali kushindwa kuyashughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayoelekezwa serikalini.
Maazimio ya Waislamu
Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu tumefikia maamuzi yafuatayo:
(1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.
Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu.
(2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.
(3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi na haki tofauti kabisa. Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. Mwalimu Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi. Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi
(4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu watateseka. Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.
WABILLAHI TAWFIQ
utanguzi:tamko la jumuiya na taasisi za kiislamu jijini mwanza kuhusu hali ya kisiasa, kauli za maaskofu, na mustakbali wa nchi lililotolewa jumapili tarehe 23 januari, 2011 katika viwanja vya shule ya msingi mbugani (muslim school), jijini mwanza
mwaka 2010 ulikuwa mwaka wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbali mbali wakiwemo madiwani, wabunge, wawakilishi, rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania na rais wa zanzibar.
kabla ya uchaguzi huo, baraza la maaskofu katoliki tanzania (tec), kupitia idara yake ya kichungaji ya tume ya haki na amani, lilitoa waraka wa kichungaji lililouita "mpango wa kuhamasisha huduma ya kichungaji katika jamii kuelekea uchaguzi mkuu 2010 na baada ya muda wakatoa walichokiita ilani ya uchaguzi na vipaumbele vya taifa. Huu ulikuwa mweleko mpya wa kanisa kuingia katika siasa mia kwa mia kwani huko nyuma kanisa halikuwahi kutoa waraka wenye maudhui kama hiyo na halikuwahi kutoa ilani ya uchaguzi na vipaumbele vya taifa.
kwa kuelewa hatari ya waraka na ilani hiyo ya kanisa, waislamu walipinga kwa nguvu zote mwelekeo huu mpya wa kanisa. Hata baadhi ya wanasiasa wenye upeo, akiwemo mzee kingunge ngobale mwiru, walikemea mweleko huo wa kisiasa wa kanisa katoliki lakini wakabezwa kwa kuambiwa kuwa wamezeeka na kufilisika kisiasa na hata kutakiwa wanyamaze kimya.
baada ya waislamu kuona kuwa wamepuuzwa, na kwa kuelewa nafasi yao kwa waislamu, shuura ya maimamu tanzania, ikatoa maelekezo kwa waislamu kupitia "mwongozo kwa waislamu" ili waislamu "wasidhulumu wala wasikubali kudhulumiwa" kama qur'an inavyoagiza (qur'an 2:279).
wakati wote wa kampeni za uchaguzi, msimamo wa maaskofu kutoka takriban makanisa yote ya kikristo nchini ulikuwa ni kuunga mkono mgombea urais wa chadema na wagombea wengine wa chama hicho nchi nzima( je hizi tetesi ni za kweli?). makanisa yakatumika kumnadi mgombea huyo kama waraka wao wa kichungaji ulivyoelekeza wazi(hivi makanisa yalitumika wapi kwa mda gani mbona mimi sikubahatika kuliona hili? Kama kuna mtu aliliona atuhabarishe tafadhali)kwa kusema;-
"mungu anakuhitaji, haya si maneno tu, bali ni uamuzi wa makusudi wa mungu anayetukabidhi wajibu huu. Kutopokea mwaliko huu unaotoka kwa mungu ni kushindwa kutimiza wajibu wetu, ni dhambi ya kutotimiza wajibu wa wito wetu wa kikristo. Wito wa kutimiza wajibu wa kijamii, ambao ni kutia chachu ya tunu za injili na mafundisho ya kristo katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa ya taifa letu". (tazama: mpango wa kuhamasisha huduma ya kichungaji katika jamii kuelekea uchaguzi mkuu 2010, uk. 2).
kwa kuwa padri slaa(huyu alifahamika na tume ya taifa ya uchaguzi kama peter wilbroad slaa na siyo padre slaa) aliamini kwamba yeye ni chaguo la kanisa, alijiridhisha yeye binafsi, wafuasi wake, viongozi wenzake wa chadema na maaskofu kuwa lazima atashinda na akasema wazi kuwa hatokubali matokeo mengine yoyote kinyume na ushindi wake kwani wakristo walishaambiwa kuwa kutokutekeleza waraka wa maaskofu ni dhambi(je maneno haya ni ya kweli? Aliyatamka wapi na nani na kwanini? Ninachokumbuka mimi chadema walisema hawatayatambua matokeo kama kutakuwa na ubabaishaji na dalili za wizi wa kura). ni muumini gani ataambiwa na viongozi wa dini yake kuwa kutokufanya jambo fulani ni dhambi kisha asilifanye?(ndugu zangu kufanya jambo fulani au kutolifanya huwa ni hiyali ya mtu, tumeona watu hawawatii wazazi wao sembuse na kanisa?)
mfano hai , huko sumbawanga, kanisa katoliki liliwatenga waumini wake kwa kile lilichodai kwenda kinyume na maelekezo ya kanisa kuhusu wagombea wa chama gani wapigiwe kura. Hali hiyo imepelekea waziri mkuu wa tanzania, mhe. Mizengo peter kayanza pinda kuwaomba radhi maaskofu kwa niaba ya serikali na chama chake kwa kile alichodai "kuwaudhi maaskofu hao wakati wa kampeni za uchaguzi"!
hatimaye tarehe 31 oktoba, 2010, taifa lilifanya uchaguzi mkuu na tarehe 5 novemba, 2010, tume ya taifa ya uchaguzi ikamtangaza mhe. Jakaya mrisho kikwete kuwa mshindi wa kiti cha urais na akaapishwa tarehe 6 novemba, 2010.
wagombea wote wa kiti cha urais walikubali matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi isipokuwa padri wilbrod slaa wa chadema na chama chake waliyakataa matokeo hayo na hata siku ya kutangazwa na siku ya kuapishwa rais si yeye padri slaa wala viongozi wengine wa chama chake cha chadema aliyeshiriki. Hata siku ya rais kikwete kuzindua bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania mjini dodoma, wabunge wote wa chadema walitoka nje ya ukumbi wa bunge kuonesha kuwa hawamtambui rais aliyetangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi(ina maana hamkuridhishwa na sababu walizozitaja chadema kwa kutofanya hayo mnayoyasema?).
baada ya kuona kuwa mpango wao wa kushika madaraka kupitia mgongo wa chadema umeangukia patupu, maaskofu na chama wanachokiunga mkono wakaamua kuhakikisha kuwa nchi haitawaliki(mna ushahidi kwa haya mnayoyasema?). Tunachoshuhudia sasa ni kutolewa kauli mbali mbali dhidi ya uongozi uliko madarakani hata kwa mambo ambayo hayakufanywa na uongozi huu uliopo sasa bali yalifanywa na awamu zilizotangulia.
kwa mfano, mikataba mibovu ya migodi ya madini inayolalamikiwa ilifanywa wakati wa awamu ya mkapa, kuuzwa mashirika ya umma kwa bei za kutupwa kulifanywa wakati huo huo wa mkapa, kuuzwa kwa nyumba za serikali katika maeneo ya serikali kwa bei ya kutupwa kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa serikali hivi sasa wanaishi nyumba za wageni (guest house) kulifanywa wakati wa mkapa. Aidha, uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, kufukiwa wachimba dhahabu bulyankulu, mauaji ya raia wasio na hatia – mwembechai, zanzibar, pemba, morogoro, ufisadi na rushwa, kuvunjwa maadili ya uongozi, kashfa za epa, meremeta, kagoda, net group solutions yote hayo hayakufanyika katika awamu hii bali wakati wa awamu ya mkapa.
wakati wa awamu ya mkapa, hatukusikia maaskofu wakijitokeza kuyakemea haya wala kulaani mauaji ya raia wasio na hatia kama wafanyavyo hivi sasa ila wamekuwa mbogo wakati wa uongozi huu kama walivyokuwa mbogo wakati wa awamu ya pili ya mzee mwinyi(kama ni hayo kwa nini msipige kelele nyinyi mlioona hayo na kumshinikiza raisi ambaye ni muislam kumchukulia hatua mkapa kwa hayo maovu aliyoyafanya?) . Kinachowasukuma si kingine bali kuogopa ile waliyoiita "dhambi" ya kutokutekeleza wito wao wa kichungaji wa kuhakikisha kuwa "tunu za injili na mafundisho ya kristo vinaonekana katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa za taifa". Laiti isingekuwa hivyo, basi wangesimamia uadilifu wa kukemea maovu katika jamii wakati wote.
aidha, kwa kuona kuwa mawakala wao wameshindwa kushika nafasi walizoamini kuwa ni haki yao, maaskofu na chama wanachokiunga mkono hivi sasa wamehamishia juhudi zao zote kudai katiba mpya ya tanzania kwa nguvu zote(je nyinyi hamkotiyari kuiona katiba mpya ya tanzania?)(by all means possible) ikiwemo hata kumwaga damu. Mmoja wa viongozi wa juu wa chadema, mabere marando, amesikika akisema wazi katika mdahalo wa katiba mpya ukumbi wa nkurumah chuo kikuu dar es salaam siku ya jumamosi tarehe 15 januari, 2011 kuwa "damu iliyomwagika arusha ndiyo wino wa kuandika dibaji ya katiba mpya tanzania".
watu waliotayari kumwaga damu za watanzania kwa malengo ya kisiasa na kudai katiba mpya ni hatari kwa amani na usalama wa nchi yetu kwa sababu katiba huandikwa kwa wino wa kalamu wala si kwa damu ya raia(mtume mhamad alifanya vita kwa ajiri ya uislam na damu zilimwagika kwa ajiri ya uislamu na mbaka leo waislamu hujilipua na mabomu na kuua wasio na hatia kwaajiri ya uislamu na huko misri mbaka leo watu 74 wameuwawa kwa ajiri ya kutaka mabadiliko tena kwa kushinikizwa na masheikh na waislamu wenzao, kama kweli hamko tiyari basi pazeni sauti kuwaambia waislamu duniani kote kuwa waache kumwaga damu kwa kujilipua na pia iombe selikali ya marekani imnyonge kabisa gailan kwa kosa la kusababisha vifo vya watu).
hii inaonesha mwelekeo wa hatari wa kundi hili la maaskofu na wanasiasa kwa amani na usalama wa taifa letu. Katiba ya nchi haiwezi kuandikwa kwa damu ya watanzania. Aidha katiba ya nchi haiwezi kuundwa katika mazingira ya vurugu, fujo, uasi kwa viongozi, dharau, kibri, uchu wa madaraka na ubinafsi. katiba itakayoundwa katika mazingira haya, haitokuwa kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi ya kanisa(sijui mnaongelea katiba ipi, katiba ya kanisa au katiba ya nchi? Na kama ni katiba ya nchi je watakaoandika ni maaskofu au watanzania? Kama watanzania ndo watakaoandika katiba hiyo je waislam hamtashiriki au? Kama mtashiriki je ni mkakati wenu hiyo katiba iwe kwa maslahi ya kanisa? Na kama ni kwa maslahi ya kanisa je ni katika nyanja zipi?).
hatari nyingine kubwa inayolinyemelea taifa letu, ni ile ya viongozi wa chama kilichopo madarakani na wale wa serikali kupingana kauli katika mambo ambayo wangepaswa kuwa na kauli moja (collective responsibility). Mwenendo huu unatishia mustakbali wa nchi yetu kwa sababu utawala uliogawanyika hauwezi kutekeleza majukumu yake kwa raia wake, na ndivyo maaskofu wanavyotaka iwe. Rais mmoja wa marekani alipata kusema "a house divided can not stand by itself"-yaani nyumba iliyogawanyika haiwezi kusimama yenyewe(ina maana nyinyi mnataka wote waitetee selikali hata katika dhuluma? Je haya ndo mafundisho ya uislamu ya kufichiana maovu? Kwa hiyo nyinyi waislamu hamtaki viongozi wanaotetea raia?). Tunaamini kwamba kugawanyika huku kwa mawaziri wa serikali iliyopo madarakani ni kazi ya kundi hili hili la maaskofu na mawakala wao katika chama tawala na serikali.
tamko la jumuiya na taasisi za kiislamu jijini mwanza.
kwa vile, baadhi ya maaskofu wamejitokeza wazi wazi kuupinga uongozi uliotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi wakati walikuwa kimya kipindi chote cha awamu ya tatu,
na kwa vile, mwelekeo na kauli za maaskofu hao vinapelekea kuiyumbisha nchi ili isitawalike wapate kudai kuwa rais aliye madarakani hafai bali chaguo lao padri slaa(dr wilbroad peter slaa) ndiye anayefaa,
na kwa vile, tayari madhara ya mwelekeo huu yameshajitokeza huko arusha kwa kuuawa watu katika vurugu zilizotokana na uchu wa madaraka ya umeya wa jiji hilo na kuchangiwa na kauli za maaskofu kutomkubali meya huyo,
na kwa vile, waislamu ni watu wapenda amani, haki na usawa kwa watu wote bila kujali rangi, jinsia, kabila, dini wala itikadi za kisiasa,(enyi wapenda amani wasihini watu wenu waache kujilipua kwa kujitoa mhanga kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na uislamu)
na kwa kuwa, kuna kila dalili ya kutoweka kwa amani kupitia kauli na vitendo vya maaskofu kuunga mkono chama maalum cha siasa,
na kwa kuwa, baadhi ya mawaziri wa serikali ya rais kikwete wameonesha wazi kuipinga serikali yake,(kwa hiyo mnataka mawaziri waseme sawa hata katika kuwadhulumu wananchi?)
sisi waislamu wa jiji la mwanza tunatamka yafuatayo;-
1. Tunaunga mkono mia kwa mia yote yaliyoandikwa katika tamko la waislamu lililotolewa diamond jubilee dar es salaam siku ya jumamosi tarehe 15 januari, 2011.
2. maaskofu kuunga mkono chama kinachopinga matokeo ya urais ni kitendo cha uhaini, u-dini na ni hatari kwa mustakbali wa taifa letu(hata maimamu na masheikh kuunga mkono dhuluma ya wananchi pia ni dhambi). hali kadhalika ni kukiuka hata maandiko ya biblia yao wenyewe yasemayo "heri walio wapatanishi kwa maana wataitwa wana wa mungu. ( mathayo: 5 msitari wa 9 ).
tulitaraji viongozi wa dini, maaskofu wakiwepo, wawe wapatanishi pale wanasiasa wanapogombana. Inapokuwa wao ndiyo sehemu ya ugomvi huo ni nani atawapatanisha wana siasa? Kama maaskofu wamekuwa wagomvi, watakuwa wana wa nani kama si wa shetani?
3. tunawaonya maaskofu waache kuivuruga serikali kwa matamshi yao yaliyojaa chuki za u-dini kwani watapelekea amani ya nchi hii kuvurugika kama walivyochangia mauaji ya kimbari ya rwanda mwaka 1994( je yale matamshi ya chuki dhidi ya wakristo yanayohubiriwa kwenye redio za kiislamu hayawezi kuhatarisha amani ya nchi? Kwa maana imeandikwa toa boriti kwenye jicho lako ndipo utoe kipanzi kwenye jicho la mwenzio).
4. kwa kuwa kauli za maaskofu huko arusha kutomtambua meya aliyechaguliwa kwa kufuata taratibu zote za kisheria, zilichangia kuuawa kwa watanzania wasio na hatia, tunaitaka serikali kuwafikisha mahakamani maaskofu wote waliotoa kauli hizo za uchochezi.(ina maana waislamu hamjui sheria kiasi hiki, kama kweli uchaguzi ulikuwa wa sheria marry chatanda alipiga kura kama nani? Na je idadi ya madiwani ilosheleza vigezo vya kupiga kura?)
hakuna mtu aliye juu ya sheria. Kama masheikh hufukishwa mahakamani na wengine hata kuswekwa kizuizini bila kupelekwa mahakamani, mfano al marhum sheikh al amin abdallah wa hapa mwanza na masheikh wengine mwaka 1964 na wengine kuswekwa ndani kwa kesi za kubumba, maaskofu wametenda kosa hili la uchochezi wazi wazi hivyo kwa nini sheria isichukue mkondo wake dhidi yao?(hata nyinyi mna haki ya kufungua kesi mahakamani ya kuwashitaki watu hawa je kwa nini hamjafanya hinyo?)
5. kama uchu wa madaraka ya umeya wa jiji la arusha tu umesababisha maisha ya watanzania watatu kupotea, damu za wengi kumwagika na mali kuharibiwa pamoja na kusimamisha shughuli za kiuchumi katika jiji hilo la kitalii, hali itakuwaje kwa uchu wa kutaka kiti cha urais?(je chaguzi zilizopita kuliuwa na hali gani?) ni watanzania wangapi watapoteza maisha yao na damu za watanzania wangapi zitamwagika ili padri slaa(dr wilbroad peter slaa) aingie ikulu?(je ni watanzania wangapi walipoteza maisha yao ili mwinyi na kikwete waingie ikulu? )
6. wakati wa ziara ya papa yohana paulo wa pili nchini tanzania mwaka 1990, kanisa katoliki lilimtaarifu kuwa linayo tume ya majeshi. Hivi jeuri hii ya maaskofu ni kwa kuwa wanayo hiyo tume ya majeshi? Hata kama wanayo hiyo tume ya majeshi, sisi waislamu kamwe hatuiogopi kwa sababu mwenyezi mungu anasema:
"je, mnawaogopa? Basi allah anastahiki zaidi ninyi kumuogopa ikiwa mu-waumini wa kweli" (qur'an 9 : 13).
pamoja na hayo, tunarudia kuitaka serikali kuueleza umma wa watanzania tume ya majeshi ya kanisa ni ya nini?(je nyinyi mlishawahi kuiona hiyo tume ya majeshi? Ina wanajeshi wangapi, inaongozwa na nani? Na ina makambi mangapi? Na vikosi vingapi? Na viko wapi? Na kama walisema mwaka 1994 mbona mnahoji leo?) au hawayaamini majeshi yetu ya ulinzi na usalama?
7. waislamu tunamtaka rais kikwete awawajibishe mara moja mawaziri wote wanaoipinga serikali yake kama mwalimu nyerere alivyomfanya kambona alipopinga sera ya utaifishaji ya serikali yake mwaka 1967. Tunamtaka rais asiwaonee haya hata kidogo mawaziri hawa wanaoipinga serikali yake kwani waswahili husema "mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe" na "mchelea mwiba, mguu huota tende"(kwa hiyo mnataka raisi awateue mafisadi na wala rushwa tu katika selikali yake na si waadilifu wanaokemea maouvo kama mnaowasema wafukuzwe?).
8. baadhi ya vyombo vya habari vimechangia sana kuzorotesha hali ya amani nchini kwa kuandika au kutangaza habari za uchochezi na hivyo kupelekea kuvunjika kwa amani. Tunavitaka vyombo hivyo vya habari kuacha mara moja kushabikia u-dini na vitende haki. Vinginevyo waislamu tutavitangaza hadharani na kuwahimiza waislamu wasivinunue, kusikiliza au kuvipa matangazo. Tukumbuke pia kuwa mauaji ya kimbari nchini rwanda yalichangiwa sana na vyombo vya habari.(mmesahau kabisa juu ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi za kiislamu ambavyo huubiri udini na kashfa juu ya imani ya wengine?)
9. vyombo vya dola navyo, jeshi la polisi, usalama wa taifa, jeshi la wananchi vitende haki kwa kufanya kazi zao kwa uadilifu, kwa ukweli na uzalendo na kutokupendelea chama au kundi jamii fulani kwani kwa kufanya hivyo vitasababisha kutoweka kwa amani nchini. kwa mfano, inapokuwa jambo linahusu masheikh au waislamu, vyombo hivyo, husuusan jeshi la polisi, huwa na ujasiri wa kuwapiga na kuwasweka ndani waislamu lakini ujasiri huo hatuuoni kwa maaskofu na viongozi wengine wa kikristo wanapovunja sheria.(hapa nimechoka kabisa, nilipoanza kusomaaya hii nilifikiri mnakemea polisi kwa kuwanyanyasa raia bila makosa na kuwatetea mafisadi na wala rushwa kama walivyofanya takukuru juu ya chenge na kuchelea kuwachukulia hatua mafisadi wakubwa au kwa kitendo cha mwema juu ya arusha au kwa kitendo cha polisi kuwaua raia wasio na hatia kule ubaruku, kumbe sinyo mna udini ndani yake.)
10. Kwa wanasiasa na wanaharakati wa mashirika ya kijamii, tunawataka waache kutoa kauli za uchochezi na vurugu kwani amani itakapotoweka hakutakuwa na wanachama wa kuwaongoza. tumieni busara zenu kujadili mambo kwa hoja na msiporidhika pelekeni malalamiko yenu mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.(ha! Ha! Haaaaaaa! Du! Mnanifurahisha kweli mbona nyinyi hajayapeleka malalamiko yenu hayo hapo juu mahakamani?)
11. Waislamu tunaunga mkono tamko la rais jakaya kikwete kuhusu kuundwa kwa katiba mpya. Pamoja na hayo, kwa mwenendo wa maaskofu na chama chao wanachokiunga mkono, tunamtahadharisha rais kwamba amebeba dhamana kubwa ya usalama wa watanzania wote hivyo asisite kuwachukulia hatua wale wote watakaotaka kutumia mjadala wa katiba mpya kwa njia zitakazohatarisha amani au kudhoofisha serikali.
12. Kwa kuwa mchakato wa katiba mpya ndiyo kwanza unaanza, waislamu tunamshukuru mwenyezi mungu kwani sasa kupitia katiba mpya tutadai haki zetu zote ikiwemo ya mahakama ya kadhi kuwepo katika katiba kama ilivyo nchini kenya, nigeria, ethiopia, gambia, zanzibar na hata uganda(kumbe kuna ajenda ya siri kwa waislamu juu ya katiba mpya? Sasa mbona juu mnasema katiba mpya itawanufaisha maaskofu? Je nqa nyinyi yakiwekwa haya mnayotaka yawekwe haitawanufaisha? Ndugu zangu waislamu unafiki nahisi ni dhambi kwenye maandiko yenu hivyo muuache mungu atawahukumu).
13. tunataka katiba mpya itamke wazi kuwa tanzania inaamini kuwepo kwa mungu muumba, serikali haina dini ila wananchi wake ndio wana dini mbali mbali. Katiba ya sasa haitambui kuwepo kwa mwenyezi mungu jambo ambalo linaifanya tanzania kuwa nchi ya kikafiri. Katiba za nchi nyingi duniani zimetamka kuamini kuwepo kwa mwenyezi mungu na hata baadhi kusema wazi "in god we trust" – tunategemea kwa mungu.(tunaposema tunataka katiba mpya itokane na wananchi inamaanisha watu wote washiriki kutoa mapendekezo yao likiwemo hili mnaloona linafaa hivyo muwahimize waislamu wenzenu wajiandae kutoa mapendekezo yao ya katiba mpya na muwaandae kwa kuwafundisha kuhusu katiba na manufaa watayoyapata kutokana na katiba mpya badala ya kukazana na huu unafiki)
kama hatuamini kuwepo kwa mwenyezi mungu kwa nini watu huapishwa mahakamani? Kwa viongozi, kwa nini waapishwe kwa kutumia vitabu vya dini, ikulu na bungeni na kwa nini kuwepo dua ya kuliombea bunge? Ni mungu gani huyo anayeombwa hapo?
14. tunataka katiba mpya ya tanzania iweke mgawanyo wa madaraka kwa uadilifu kwa kutamka wazi kuwa rais akiwa muislamu, waziri mkuu awe mkristo na rais akiwa mkristo, waziri mkuu awe muislamu kama ilivyo nigeria na lebanon ili kuepuka u-dini. Na vivyo hivyo kwa ngazi zote za madaraka mgawanyo uwe nusu kwa nusu.(je tanzania ni ya waislamu na wakristo tu? Na sisi tusioamini katika hayo ndo mnatutenga jumla? Ina maana sisi watu tusio waumini wa hizo dini za waarabu na wazungu hatuna haki katika taifa letu?)
15. tunataka iundwe wizara maalumu ya mambo ya dini ili ishughulikie masuala ya dini kuliko kuyaacha kama yalivyo sasa hayana wizara inayoyashughulikia. Kama mambo ya kipuuzi tu kama vile muziki na maagizo yana wizara maalum, vipi dini zisiwe na wizara yao?(mambo ya mungu inakuewaje yalatibiwe na wizara ina maana wajumbe wa mungu kama masheikh na maaskofu wameshidwa kazi?)
16. tunataka katiba mpya isiruhusu serikali kuingia mkataba wa upendeleo na kundi jamii moja kama ilivyofanya kupitia makubaliano ya maridhiano na makanisa ya kikristo mwaka 1992,(kama ni kweli basi mimi nawaunga mkono kwa hili kwani nchi si ya waislamu wala wakristo wala wale wanaoabudu dini za asili) makubaliano ambayo yanatekeleza andiko la bibilia "mwenye nacho ataongezewa na asiyekuwa nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho"(luka 8 msitari wa 18). wakristo walikuwa na shule, hospitali, vyuo vya ualimu, vyuo vikuu n.k huku waislamu wakiwa hawana kitu. Badala ya kupewa waislamu wasiokuwa na rasilimali hizo wakapewa wakristo na hivi sasa wanaongezewa kupitia makubaliano ya maridhiano kati yao na serikali(historia inaonyesha waislamu ni wabaguzi sana kwenye taassisi zao kuliko wakristo na pia wakristo ni wafanisi zaidi kuliko waislamu kwenye taasisi kama shule na hospitali. Kuna idadi kubwa ya waislam waliosoma kwenye shule za kikatoliki na wanaotibiwa kwenye hospitali za kanisa hivyo mimi sioni sababu ya waislamu kupewa hayo wanayodai wakati hayana tija kwa wasiowaislamu).
17. Kwa kuzingatia tamko namba 16 hapo juu, tunaitaka serikali iache mara moja kutekeleza maridhiano hayo batili kati ya serikali na makanisa na pia ituambie hadi sasa imeshayapa makanisa ya kikristo mabilioni mangapi tangu mwaka 1992? Aidha tunataka watendaji wote wa serikali waliohusika kuandaa na kupitisha maridhiano hayo ya u-dini wachukuliwe hatua za kisheria kwani huu nao ni ufisadi kama ule wa epa, kagoda, meremeta, dowans n.k.
18. Sambamba na hilo, tunaitaka halmashauri ya jiji la mwanza ikabidhi kwa waislamu shule ya msingi mbugani (muslim school) mara moja kama alivyoagiza rais mkapa miaka kumi na tano iliyopita. Hali kadhalika tunaitaka serikali irejeshe shule zote zilizokuwa muslim schools ambazo zilitaifishwa wakati waislamu walikuwa na shule chache kulinganisha na wakristo waliokuwa wakipata misaada kutoka serikali ya kikoloni na sasa kupitia makubaliano ya maridhiano na serikali tuliyoyaeleza hapo juu.
19. tunataka katiba mpya itamke wazi kuwa siku ya ijumaa nayo ni siku ya mapumziko ili waislamu nao waweze kwenda kusali sala ya ijumaa kwa utulivu pasina kuhofia kufukuzwa kazi au kukosa masomo kama ilivyo sasa ambapo kwenda kusali ijumaa ni fadhila tu. Kama hilo halikubaliki, basi siku zote tatu ijumaa, jumamosi na jumapili ziwe siku za kufanya kazi nusu siku ili sote tuwe sawa. mkao wa sasa wa mapumziko jumamosi na jumapili unaonesha kuwa nchi hii ni ya kikristo(hata sisi tusiowapagani tutengewe siku maarumu ya kuabudu na iwe ya mapumziko na pia tunataka kuwe na sikukuu za watu tunaoamini katika dini za asili yaani dini ambazo babu zenu na bibi zenu walizifata ingalau tano kwa mwaka kama wakristo na waislamu wanavyofanyiwa).
20. tunataka wimbo wa taifa uliopo ufutiliwe kwa mbali kwani unaonesha wazi tanzania ni nchi ya kikristo kwa sababu hakuna asiyejua historia ya wimbo huo kuwa ulianzia kanisani huko soweto afrika ya kusini. Kwa kizulu wimbo huo unaitwa "nkosi sikeleli afrika". Pia hakuna asiyejua kuwa upo katika kitabu kiitwacho "chuo kidogo cha sala na maombi cha kanisa katoliki". Hata mashahidi wa yehova huko mbeya waliwahi kuukataa.(haya ni marumbano yasiyo na msingi wowote hata huo wimbo mpya lazima utaandikwa na au mwislamu au mkristo au anayeabudu dini za asili hivyo tatizo litabaki palepale kila mmoja atadai haki ya kuandika huo mwimbo mwisho wa siku itakuwa vurugu)
21. tunataka katiba mpya itamke wazi kuwa rais akitoka bara, raisi wa awamu nyingine atoke zanzibar ili kuwatendea haki wazanzibari. Tayari hivi sasa, tanzania bara imeshatoa marais mara tatu, mwalimu nyerere, rais mkapa na rais kikwete. Ni rais mwinyi tu ndiye aliyetoka zanzibar kwa hiyo rais ajaye lazima atoke zanzibar kutoka chama chochote kile kiwacho.(sisi tunataka raisi ajaye awe ni yule anayeamini dini za asili yaani asiwe mkristo wala muislamu ili kuweka uwiano katika hili.pili hiyo siyo hoja ya msingi sana kwa sasa hasa ukizingatia kuwa zanzibar wana rais wao hivyo hawastahili kuwa na rais bara kwa kufanya hivyo ni kuidhurumu tanganyika utaifa wake)
22. Tunamtaka rais kikwete aongoze mchakato wa kuleta katiba mpya kwa amani, haki, ujasiri, bila woga wala upendeleo wowote. Katu asiruhusu dharau kutoka kwa kiongozi yeyote awe wa kisiasa ndani au nje ya serikali yake au hata kiongozi wa kidini. na pale atakapoona mazingira ya nchi hayapo katika utulivu na amani, ni kheri ausitishe mchakato wa katiba mpya kwani katiba haiandaliwi katika mazingira ya vurugu, chuki na uhasama kama tuliyo nayo hivi sasa.
hitimisho :
nchi hii ni ya watanzania wote. Hakuna aliye na haki zaidi ya mwingine. Kama taifa, watanzania tunafanana na watu walio katika merikebu. Hivyo tunapomuona mmoja wetu anataka kuitoboa merikebu yetu, hatupaswi kumwangalia tu atimize azma yake kwani akifanikiwa tutaangamia sote.
tunawataka watanzania wote kwa makundi jamii yao, vyama vyao, dini zao na tabaka zao mbali mbali kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwanza. Aidha tunawataka maaskofu kuheshimu imani za dini nyingine katika kutekeleza wito wao wa kichungaji. si lazima umkandamize mwingine asiendelee ili wewe uendelee.
tukumbuke kuwa hakuna mahali pengine ambapo watanzania wanapategemea kuishi wao na vizazi vyao hivyo tuilinde nchi yetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo.
kama ambavyo waislamu walimlinda mwalimu nyerere dhidi ya wakoloni na tukavumilia madhila yote tuliyofanyiwa ili kulinda na kudumisha amani, sasa tunasema wazi wazi kuwa hatutakuwa mhanga wa agenda za maaskofu na mfumo kristo bali tutakuwa tayari kuitetea dini yetu kwa hali na mali.
waislamu kamwe si wachokozi . lakini hapa tulipofikishwa na mfumo kristo, tunapenda maaskofu na mwingine yeyote yule aelewe wazi kuwa waislamu nchini tanzania hivi sasa tuko tayari kufa kuliko kuishi huku tukiiona dini yetu ikidhalilishwa kwani hatuna cha kupoteza- kwetu ni mawili tu, ima ushindi dhidi ya dhulma au kuuwawa tupate pepo(haya waislamu fanyeni hima muuwawe ili mpate pepo).
na mwenyezi mungu ndiye mjuzi na muweza wa yote.
wabillaahi tawfiiq.
wassalaamu alaykum warahmatullahi .
je tutafika?
mungu ibariki afrika,
mungu ibariki tanzania,
amen
Jamani kuna mtu aliyewahi (askofu) kwamba tumchague slaa mie nafikiri hata watu wenye uelewa kama majjid tuwe na wasi was nao kidgo, kabula sijaenda sana oneni hili tamko hap[a chini