Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Kuna tarimo huyu mbaba alikuwaga ni mbabe sana. Kuna siku akiwapangishia askari kwenye nyumba zake, sasa hawa askari wakawa hawampi kodi yake. Kuna siku akawaonyesha kwamba yeye ni muhuni.

Kipindi cha masika alikuja na mafundi bati akawalipa hela. Mafundi wakapanda juu ya bati wakang'oa mabati yotee. Jioni mvua ikanyesha kubwa. Chumba cha maaskari kikageuka bahari. Niliwaonea huruma watoto wa wale askari maana kila kitu kiliharibika. Mzee wa watu akarudi zake Kibisho.

Ila Mungu amrehemu yule mzee yaani mpaka nimeipenda roho yake alafu alikuwa jirani yangu sana
 
Kuna baba yake mbowe mzee Aikael Mbowe nilipewaga story na mama yangu nilishangaa. Huyu mzee alipataga msiba wa mke wake. Sasa akaajiri wapishi wa kusindikiza safari ya mke wake. Kuna kazee kamoja kalikuja kuomba supu. Kazee ka watu kakanywa supu kakabwa na mfupa mpaka akafa mzee wa watu.

Walipoenda kumpa mzee wake Mbowe habari, mzee aliwatolea pistol akawaamuru wakamzike chini ya mkahawa au la si hivyo atawapiga risasi wote. Wakamzika yule mzee huku baba wa Mbowe anaangalia hivi maana aliwaambia kuna msiba wa mke wangu msiniharibie siku au niwapoteze wote.
 
lucas Tarimo
Vïcent lasway

mawalla
Mberesero
mremi wa dar exp

Bosco Chuwa

Panjwani.

Hari singh
Rajinder

Mchuku wa Mangi.
Huyu Laswai muziki mnene mkuu marafiki zake ni watu wanene sana ,nadhani mnakumbuka harusi ya binti yake iliyofanyika viwanja vya gofu Moshi
 
Habari za mida wana jf

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia,wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani.Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi.Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.
Huyo mzee wa pembe za ndovu alikuwa akiitwa “Mayahudi”
 
Bakhressa kweli alikuwa anashona viatu!!!!
Ndio mkuu,hukumbuki wakati wa ufunguzi wa runinga yake,mzee wa Msoga alisema huyu mzee kaanzia mbali kwa sisi watoto wa mjini tulikuwa tunakula pilau kwenye vimigahawa vyake na pia kazi ingine aliyokuwa anaifanya kabla ya kufikia hapa hatuwezi kuisema akimaniisha mzee alikuwa mshona buti,kwa kifupi Mzee bakhresa kilichomtajirisha zaidi ni pale baada ya serikali kuchoma mchele wake na kusema haukufaa kwa chakula cha binadamu,nadhani unakumbuka wapelelezi,wakemia na wengi waliohusika na kuchukua sampo za huo mchele walikuwa wanapukutika mmoja baada ya mmoja na mzee akashinda kesi,nasikia fidia akapewa mali za NMC vikiwemo vinu vikubwa vya NMC Tazara,NMC Pugu rd,mengine sasa ni historia
 
Kipanga alikua jirani na yule baharia aliyekufa kwa viagra Simbard alikua na gari short chasses?
Philip Tairo wa bia za jumla pale (memorio) unakumbuka?
Philip Tairo huyu Mzee alikuwa poa sana, hakuwa na makeke kama warombo wengi wenye hela, gari yake ya kutembelea Simple tu Suzuki Godwin& mcha Mungu kweli hakosi ibada Kristu Mfalme
 
Back
Top Bottom