Matajiri wa manispaa ya Morogoro

Matajiri wa manispaa ya Morogoro

Pendaelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
12,891
Reaction score
37,866
Hope mpo na amani na tumaini la kufukia kilele cha mafanikio.

Wakati tukiendelea kupambana ili kufikia matarajio yetu Kuna wenzetu ambao ama kwa juhudi zao au za waliowatangulia wameweza kufikia walao hatua nzuri, basi kwetu tunaotazamia kufikia huko wao wana baki Kama kioo kwetu.

Wakati fulani niliwahi kuishi mkoa wa Morogoro pale manispaa, niliweza kushuhudia watu ama kampuni au familia walio matajiri kwa kiasi chake.

Naomba niwaorodheshe hapa japo sio kwa mtiririko sahihi, wawe Kama marejeo kwa wapambanaji.

Azizi Abood
Taji Mohammed
Omar Awadh
Islaam family
All Sayed
Ladwa
Hood family
BM au Makundi
Focas Munish
Epafras Meela
Machare
Christian Munish au Mashikao
Kihanga
Hare Kihongos
.
.
.


Orodha itaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo ni rahisi sana kuitwa tajiri ukiwa na hata euro elfu 25 ambayo ni kama million 60. Likizo yangu ya kwanza kurudi bongo nilikuwa na kama dollars za kimarekani elfu tatu hivi. Nilikuwa natinga suti kila siku na miwani ya giza mieusi. Niliitwa millionea. Nilikodisha kaprado flani. Nywesha maboya pombe na kutandaza miti at will. Zilipokaribia kuisha nikaingia mitini kujificha nikisubiria siku ya return ticket huku nikimpiga mizinga ya hatarii mbibi wangu akawa anatumia Western union kidogo kidogo. Niliacha gumzo
hiyo ni enzi za mwalimu sio sasa usd 3000 utamtambia nani bongo kwa sasa..
 
Meela ndio mwenye baa pale mjini ?
Taj Mohamed ndie aliekuwa mmiliki wa uwanja w jamhuri kabla hajapokonywa na CCM.
Taj Mohammed sio alikuwa mmliki wa uwanja wa jamhuri laa, bali yeye ndie alieujenga kwa garama zake walivyomalizana ndio wakaumiliki kwa 100%.
 
Hapa ndipo Watanzania tunapokosea. Mtu unakaa kudodosa utajiri wa mwenzako badala ya kutumia muda huo kujitafutia mafao ya kujikimu mwenyewe na familia yako. Halafu tunalalamika ugumu wa maisha. Piga kazi. Achana na ndoto za utajiri au umaskini wa mwenzako. Huo haukusaidii kitu.
 
Back
Top Bottom