Nimemuelewa vizuri sana, bado kwa sasa, toka kile cha mwanzo ambacho kilizuiliwa na Nyerere kilikuwa kijengwe na EAMWS, kwa sasa tuna vyuo vikuu vya kiislaam sio vya individually na tajiri mmoja mmoja bali na taasisi za kiislaam kama vile H. H. The Agakhan University, Morogoro Islamic University na soon Al Muntazir University.
Mtoa mada katoa wazo zuri ingawa si la mwanzo au si kuwa halifanyiwi kazi na Waislaam, linafanyiwa sana kazi na InshaAllah tutakuwa na Universities za Kiislaam iwe za matajiri au za institutions.
Si rahisi kwa matajiri pekee kuanzisha na kuendeleza vyuo vikuu, tumeona pale Bagamoyo kuna tajiri (nadhani Zakaria) amejenga chuo kikuu cha Kiislaam lakini nadhani tatizo ni kukiendesha kwa ufanisi, University si majengo pekee bali mfumo mzima wa uendeshaji wa chuo ndio muhimu zaidi na kwa matajiri individuals wa Kitanzania ni wazi kabisa bado hatujafikia kiwango cha tajiri kujenga, kukihudumia na kukiendesha chuo kikuu, lakini tutafika. Kwa hili sidhani hata kama kuna matajiri ambao si wa kiislaam Tanzania ambao wamefanya hivi, kama yupo simjui naomba nifahamishwe.