Mataifa ya Afrika tupieni jicho Uchaguzi wa Marekani

josias

Member
Jan 7, 2014
47
34
Leo ni siku ya Uchaguzi Mkuu Nchini Marekani ambapo Mwanasiasa Nguli Joe Biden atakuwa akichuana vikali na rais wa sasa wa Marekani Ndg. Donald Trump. Katika Uchaguzi huu wa mwaka huu Joe Biden anaonekana kuwa na nguvu zaidi ya Donald Trumpn kwani tafiti zinaonyesha kuwa uwezekano wa kushinda kwa Joe Biden ni 52% mbele ya Donald Trump ambaye uwezekano wake wa kushinda ni 42%.

Mpaka sasa Uchaguzi wa Marekani unaonekana kuwa na Kasoro nyingi haswa baada ya Team ya Kampeni yaDoanld Trump kuonekana kuwa inawashambulia na kuwafanyia fujo wafuasi wa Joe Biden. Lakini pia pamoja na hayo tayari katika majiji mbalimbali ya Marekani maeneo ya Biashara yamewekewa uzio maalumu ili kuweza kujikinga na uharibufu unaoweza kusababishwa na waandamanaji baada ya matokeo kutangazwa

Pamoja na mambo haya kuonekanaKuharibu sifa za uchaguzi wa Marekani bado kuna suala la wizi wa Kura ambalo miaka yote ya Uchaguzi limekuwa likiikumba Marekani kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita baada ya uchaguzi wa marekani kuingiliwa na Urusi.

Pamoja na joto la Uchaguzi kuwa juu nchini Marekani utaona ni kwa namna gani wananchi na viongozi wa nchi hiyo walivyo wazalendo kwa nchi yao. Hawatumii mitandao ya Kijamii kuchafua taswira ya nchi yao Kimataifa na pia hawatumii mitandao kuchochea ghasia, maandamano na fujo. Nadhani ni muda sasa wanasiasa haswa wa upinzani barani Africa kujitafakari na kuona ni kwa kiasi gani hawana uzalendo kwa mataifa yao.


usa.jpg
 
Back
Top Bottom