Kauli ya Raimondo yafichua angalau sifa tatu ilizo nazo serikali ya Marekani ya sasa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111482159450.jpg


Kuna msemo wa kale wa Kichina unaosema Jitumie Kuwahukumu Wengine, ambao unamaanisha kutumia mawazo yako mabaya kuwafikiria wengine. Ingawa ulitungwa katika Enzi ya Han ya China miaka 800 iliyopita, haujapitwa na wakati hata kidogo unapotumiwa kuelezea serikali ya Marekani ya sasa. Hivi majuzi, alipozungumza kuhusu kwa nini serikali ya Marekani inazuia uagizaji wa magari ya umeme ya China, Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo alisema kwamba magari ya leo ni kama "iPhone yenye magurudumu" ambayo yanaweza kukusanya taarifa nyingi. "kama kuna magari milioni 3 ya China kwenye barabara nchini Marekani, China inaweza kuzifanya zizime moto kwa wakati mmoja." Je, Raimondo anaashiria kuwa simu za Iphone ni zana zinazotumiwa na Marekani kukusanya taarifa binafsi za nchi nyingine kinyume cha sheria? Kweli haijulikani kwamba Ofisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Apple Tim Cook alisemaje baada ya kusikia kauli hiyo. Lakini kwa vyovyote vile, matamshi ya Raimondo yalifichua angalau sifa tatu ilizo nazo serikali ya Marekani ya sasa—kutoona haya, kutojiamini, na unafiki.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Marekani imefichuliwa mara kwa mara kuwa inawapeleleza kwa siri wanasiasa wa nchi nyingine, baadhi yao wakiwa hata maafisa waandamizi kutoka nchi washirika wakiwemo aliyekuwa chansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini. Lakini hata hivyo Bibi Raimondo alizishtumu nchi nyingine kwa "kukusanya taarifa za Wamarekani." Hii inaashiria kwamba Marekani haioni haya hata kidogo na inafikiri kwamba nchi nyingine ni mbaya kama wao. Muhimu zaidi ni kwamba wazo hili linaonyesha kuwa Marekani haijaamua kuacha kuvunja mamlaka ya nchi nyingine baada ya shughuli zake za udukuzi kufichukuliwa, na badala yake inafanya mchezo wa “kuvunja chupa iliyovunjika” na kuamua kuifanya "siri hii iliyo wazi" hadi mwisho, na kuwa tayari kwamba siku moja Marekani itafanya simu za mikononi za viongozi wa nchi nyingine "kuzima moto kwa wakati mmoja." Kama msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning alivyosema, "Kwa mujibu wa mantiki ya Raimondo, je na China pia inapaswa kuwa na wasiwasi zaidi kwamba Marekani inaweza kuchukua kisiri taarifa za mamilioni ya watumiaji wa simu za mkononi za Apple wa China na hata kuzizima moto kwa wakati mmoja?"

Bila shaka, matamshi ya kipuuzi na ya kijinga ya Raimondo hayamwakilishi yeye mwenyewe, lakini yanaidhinisha tu sera ya serikali ya Biden ya kupiga marufuku magari ya umeme ya China kuingia katika soko la Marekani. Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya magari ya China imepata maendeleo ya haraka, na kuipita Japan na kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa magari kamili duniani. Kinyume chake, sekta ya magari ya Marekani inafifia. Kile kinachoitwa "usalama wa taifa" sasa kimekuwa chombo cha Marekani cha kutekeleza sera ya kujilinda kibiashara. Bidhaa yoyote ya China ambayo ina ushindani zaidi kuliko Marekani inaweka chapa ya "kuhatarisha usalama wa taifa" na kuzuiwa kuingia kwenye soko la Marekani. Kwa hivyo, wakati magari ya umeme ya China yalipochukua nafasi ya magari ya umeme ya Tesla ya Marekani, yakawa kile wanasiasa wa Marekani wanakiita "iPhone yenye magurudumu." Je, Marekani inayojiamini iko wapi?

Kwa miaka mingi, serikali ya China imepinga kufafanua uhusiano kati yake na Marekani kwa neno "ushindani," lakini Marekani inashikilia kufanya hivyo. Basi kama tukisema ushindani, tunapaswa kudumisha kiwango cha juu cha kujiamini na kuwa na mawazo wazi, kama China ilivyokuwa kwa kufungua soko lake kukaribisha makampuni ya Marekani kuwekeza na kuanzisha biashara nchini China. Makampuni makubwa makubwa ya Marekani kama vile Microsoft, Apple, na Tesla yote yanaweza kuingia China bila kuzuiliwa. Lakini serikali ya Marekani inayosisitiza ushindani inatumia mamlaka mbalimbali za kitaifa kuzuia bidhaa za China kuanzia vifaa vya mawasiliano hadi magari ya umeme. Je, huu ndio ushindani ambao Marekani inaoita mdomoni mwake?

Kufuatia mazoea ya serikali ya Marekani ya sasa, itaanza uchunguzi kuhusu kile kinachoitwa "matishio yanayoweza kutokea dhidi ya usalama wa taifa la China" dhidi ya magari ya umeme ya China, na hatimaye kutoa ripoti isiyo na msingi. Hata hivyo, kitendo kama hicho kimethibitishwa mara kwa mara kuwa si cha upeo wa kuona mbali. Sio tu kwamba itasababisha makampuni ya Marekani kupuuza kuinua viwango vya teknolojia kwa sababu yanapoteza washindani, bali pia mwisho yataondolewa tu katika soko la kimataifa, na muhimu zaidi ni kwamba serikali ya Marekani kufanya suala la biashara kuwa la kisiasa kutashusha sifa ya Marekani kimataifa kuwa chini zaidi.
 
Back
Top Bottom