Mataifa 4 ya kiarabu yaipa Qatar masharti 13 kuafikia la sivyo itengwe

Balaa kwetu,litaanza pale OPEC,watakapopunguza kiwango cha mafuta wanayozalisha,
Bei ghafi itapanda,ukiongeza na kodi iliyoongezwa kwenye mafuta,hapa nyumbani,mkanda utazidi kubana
 
Mataifa manne ya kiarabu yameitumia Qatar masharti 13 ambayo ni sharti iafikie iwapo inataka kuondolewa vikwazo kulingana na vyombo vya habari.

Saudia, Misri, UAE na Bahrain zinataka taifa hilo kufunga kitu chake cha habari cha Aljazeera.
Pia wanaitaka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran na kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.

Qatar imekana kufadhili magaidi hatua inayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.
Taifa hilo limekabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa kipindi cha wiki mbili ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kati ya mataifa hayo ya Ghuba kwa miongo kadhaa.

Orodha hiyo ilitangazwa baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kuwaambia majirani wa Qatar ''kuweka mahitaji yao na kuchukua hatua''.

Waandishi wanasema kuwa Marekani ambayo inataka kutatua mzozo huo imekuwa na matatizo, kuhusu kipindi cha Saudia na mataifa mengine kuweka rasmi mahitaji yao.

Hakujakuwa na majibu ya moja kwa moja kutoka Qatar lakini waziri wa maswala ya kigeni Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani alisema awali kwamba Qatar haitafanya majadiliano yoyote hadi pale vikwazo hivyo vitakapoondolewa.




bbc swahili
Hawa Waarab ni wapuuz kweli. Ifungwe Al Jazeera kwa kosa gani?
 
kwa position ya qatar ilipo inaathirika sana na siege aliopigwa hamna hata haja ya vita hapo....wakae tu wayamalize kikubwa...qatar airways ishaathirika sana imeanza kupaki ndege sasa
Quatar ametoa offer ya kununua aslimia 10 ya hisa za American Airways kwahiyo inaonyesha bado yuko vizuri ki uchumi
 
Kiboko cha Iran ni Israel pekee, Saudia hawezi kupigana na Iran, atapigwa hadi Saudia yote ipinduliwe labda asaidiwe na Marekani.

For some reason naona hata Marekani imeanza kushtukia Ukoo wa Kifalme wa Saudia - leo kwa mfano Waziri wa mambo ya nje wa Merikani amehoji kuhusu demand lukuki za Saudia na washirika wake wanazo taka Qatar itekeleze within ten days - wanatoa ultamatum kwa nchi huru bila idhini ya Umoja wa Mataifa Saudia wana jeuri sana. Waziri huyo wa Merikani amesema demand za Saudia ni unreasonable, kwa nini wasimalize tofauti zao kistaarabu - baadae ikaja gundurika kwamba kumbe uhasama baina ya Qatar na Saudia ulikuwa unafukuta kichini chini kwa muda mrefu sio leo wala jana, inaelekea huko Saudia mambo siyo shwali, Ufalme unaogopa uprising/kuangushwa Utawala wao na Wasaudia wenyewe!!

Ufalme wa Saudia una suspect Qatar ndiye anawapa support wanao pinga utawala wa Kifalme wa Saudia, inavyo elekea ni kama vile Saudia inataka kushirikisha Mataifa mengine kuishambulia Qatar kijeshi na kumuondoa Madarakani Utawala wa Qatar - sioni kama Amerika inaweza ku-support upuuzi huo given kwamba ina base kubwa ya kijeshi huko Qatar, kitu kingine Uturuki imesema itaongeza nguvu zake za kujeshi huko Qatar kumlinda Kiongozi wa Qatar sina shaka na Iran itatafuta mbinu za kuilinda Qatar - binafsi naona kupakuka kwa Utawala wa Saudia kunaweza kuwatokea puani ikiwa Uturuki,Syria,Iran possibly na Russian watatoa msaada wa kuanzisha kundi la waasi wa kuitia msuko suko Saudia - sioni kama raia wa Saudia wataendeleaa kuvumilia utawala wa Kifalme kwa muda mrefu - wakisaidiwa from without wata support uasi - Saudia kwa hivi sasa inapaswa kuwa makini sana.
 
Kama ni kweli wanependekeza wafunge kituo chao cha kimataifa cha habari kikubwa kama ilivyo BBC basi Saud Arabia ni masheitwain na watakuwa wametumwa na American huo ushenzi maana marekani na washirika wao wanatakaaga mambo yao yajulikane tu hapa duniani

Mkuu sidhani kama Marekani inahusika moja kwa moja na ujinga wa Saudia, if anything mbona Al Jazeera ilikuwa inatumika sana kuendeleza propaganda za USA, yaani ungesikiliza taarifa za CNN na Al Jazeera zinafana kwa kila kitu unaweza kufikiri wanatumia script moja au tuseme handaout zilizo tayarishwa na Uncle SAM watangazie Dunia.
 
Mkuu sidhani kama Marekani inahusika moja kwa moja na ujinga wa Saudia, if anything mbona Al Jazeera ilikuwa inatumika sana kuendeleza propaganda za USA, yaani ungesikiliza taarifa za CNN na Al Jazeera zinafana kwa kila kitu unaweza kufikiri wanatumia script moja au tuseme handaout zilizo tayarishwa na Uncle SAM watangazie Dunia.
ukiachia saudia basi umewaunganisha waislam,so lazma ibanwe
 
Mkuu sidhani kama Marekani inahusika moja kwa moja na ujinga wa Saudia, if anything mbona Al Jazeera ilikuwa inatumika sana kuendeleza propaganda za USA, yaani ungesikiliza taarifa za CNN na Al Jazeera zinafana kwa kila kitu unaweza kufikiri wanatumia script moja au tuseme handaout zilizo tayarishwa na Uncle SAM watangazie Dunia.
Tusubiri mkuu maana sababu walizotoa hawa jamaa wa saudi Arabia ni zakijinga sana utata unakuja unakuja kuwa Saud Arabia hawezi fanya kitu bila USA kukibariki ndio mshaka yalipo hapo !!!
Shirika kubwa kama la Al jazeera siku likiwa upande wa china na Iran ni shida sana mkuu kwa mataifa ya magharibi!!!
 
Watu wengine, acheni uchochezi wa kijinga. Iran alishampiga nani. Mbona asiipige Israel awanyang'anye ardhi awape Wapalestina.

Tatizo lenu, mnapenda sana michapo ya kwenye mabaraza ya kahawa.
 
Watu wengine, acheni uchochezi wa kijinga. Iran alishampiga nani. Mbona asiipige Israel awanyang'anye ardhi awape Wapalestina.

Tatizo lenu, mnapenda sana michapo ya kwenye mabaraza ya kahawa.
sio kwamba Israel hawezi kupigwa,anachakazwa bila shida... tatizo ni kwamba nyuma ya Israel kuna nani? ukipigana na Israel tambua kuwa unapigana na NATO na USA
 
Ndilo hilo mkuu, mambo mengine ni gheresha tu - tatizo Ufalme wa Saudia hautaki raia wake waelezwe ukweli kuhusu utawala wao, wanaogopa sana kuondolewa madarakani kwa nguvu za umma/color revolution wako paranoid kweli kweli - wanataka raia wao wabaki mbumbubu kwa kusikiliza Kituo chao cha TV i.e Al Arabia (sijui kama nimepatia jina) kituo hicho kinatumika kutukuza utawala wa Ufalme na kuchochea nchi za Kiarabu zichukie IRAN - yaani Ufalme wa Saudi Arabia unajifanya ni semi Super Power wa Mashariki ya Kati - cha ajabu pamoja na silaha zao za kisasa bado waasi wa Yemen wanawapeleka puta karibu mwaka unakatika bila mafaniko yoyote, leo hii ndiyo wajitape kwamba wanaweza kupigana na IRAN - naona hizo ni ndoto za mchana.


Hayo mambo yapo huko kwenu, مملكت لعربي سعدي haiji kuongozwa kwa matakwa ya watu.

Waambieni hao Qatar wadindishe wakione, na uzuri upande ilioko Saudia ndio upande wa waislamu wote min ghairi ya mashia!

Sheria za kiislamu zitaendelea kutekelezwa Saudia na hamna atakaeamua fyoko fyoko!
 
Quatar ametoa offer ya kununua aslimia 10 ya hisa za American Airways kwahiyo inaonyesha bado yuko vizuri ki uchumi
saudi arabia,bahrain na qatar zmefunga mipaka yaoyote pamoja na anga zao kwa qatar,saudi amefunga mpk mpk wake wa nchi kavu......hali hii ikiendelea kwa muda mrefu itaathiri sana uchumi wa qatar cheki wanavyopakana hapa
800px-Arab_Gulf_States_english.png

watu wanaongea tu but kwa eneo alilopo qatar atapata shida sana iwapo mambo yataendelea hivi km yalivyo na ikitokea armed conflict basi gharama ya kuilinda qatar itakua kubwa mno ukizingatia wamepigwa siege pande tatu wanatumia upande mmoja tu ambao unapita kilometer nying za maji mpk utokee iran, hata saudi amekaza coz anaona ugum utaompata qatar
 
Back
Top Bottom