Mataifa 4 ya kiarabu yaipa Qatar masharti 13 kuafikia la sivyo itengwe

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,768
2,000
Mataifa manne ya kiarabu yameitumia Qatar masharti 13 ambayo ni sharti iafikie iwapo inataka kuondolewa vikwazo kulingana na vyombo vya habari.

Saudia, Misri, UAE na Bahrain zinataka taifa hilo kufunga kitu chake cha habari cha Aljazeera.
Pia wanaitaka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran na kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.

Qatar imekana kufadhili magaidi hatua inayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.
Taifa hilo limekabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa kipindi cha wiki mbili ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kati ya mataifa hayo ya Ghuba kwa miongo kadhaa.

Orodha hiyo ilitangazwa baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kuwaambia majirani wa Qatar ''kuweka mahitaji yao na kuchukua hatua''.

Waandishi wanasema kuwa Marekani ambayo inataka kutatua mzozo huo imekuwa na matatizo, kuhusu kipindi cha Saudia na mataifa mengine kuweka rasmi mahitaji yao.

Hakujakuwa na majibu ya moja kwa moja kutoka Qatar lakini waziri wa maswala ya kigeni Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani alisema awali kwamba Qatar haitafanya majadiliano yoyote hadi pale vikwazo hivyo vitakapoondolewa.
bbc swahili
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Wakiitenga Qatar ndio watazidi kuisogeza karibu na Iran kitu ambacho Marekani asingependelea...

Ukiondoa Uturuki, Marekani pia ina kambi yake ya kijeshi Qatar hivyo pamoja na Marekani sasa hivi kuonekana kama vile yuko upande wa Saudia lakini bado asingependa kuipoteza Qatar kama mshirika muhimu.
 
kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
3,287

Upo sahihi na hata Russia ameonesha nia ya kumsupport Qatar .

Hayo mataifa ya kiarabu sijui wana shida gan yaan full unafik
 
Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,026
2,000
Hayo masharti hayatekelezeki.waendelee kuitenga tu yapo mataifa mengine wataisaidia Qatar
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,111
2,000
Wanaiogopa aljazeera kwakuwa inawaumbua
Ndilo hilo mkuu, mambo mengine ni gheresha tu - tatizo Ufalme wa Saudia hautaki raia wake waelezwe ukweli kuhusu utawala wao, wanaogopa sana kuondolewa madarakani kwa nguvu za umma/color revolution wako paranoid kweli kweli - wanataka raia wao wabaki mbumbubu kwa kusikiliza Kituo chao cha TV i.e Al Arabia (sijui kama nimepatia jina) kituo hicho kinatumika kutukuza utawala wa Ufalme na kuchochea nchi za Kiarabu zichukie IRAN - yaani Ufalme wa Saudi Arabia unajifanya ni semi Super Power wa Mashariki ya Kati - cha ajabu pamoja na silaha zao za kisasa bado waasi wa Yemen wanawapeleka puta karibu mwaka unakatika bila mafaniko yoyote, leo hii ndiyo wajitape kwamba wanaweza kupigana na IRAN - naona hizo ni ndoto za mchana.
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,119
2,000
Kama ni kweli wanependekeza wafunge kituo chao cha kimataifa cha habari kikubwa kama ilivyo BBC basi Saud Arabia ni masheitwain na watakuwa wametumwa na American huo ushenzi maana marekani na washirika wao wanatakaaga mambo yao yajulikane tu hapa duniani
 
Bullava

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
526
1,000
Yaani eti KAMBI YA KIJESHI YA UTURUKI IFUNGWE KWA SIKU 10 TU. Nina uhakika ndani ya hizo siku 10 kuna mtu atakuwa ameshapinduliwa
 
nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
5,916
2,000
Hayo masharti hayakubaliki,
as long as Turkey yuko pale hawawezi kumshambulia,Turkey akiondoka tu ndani ya nusu saa huyo mfalme atakuwa kishapinduliwa,
kwa position ya qatar ilipo inaathirika sana na siege aliopigwa hamna hata haja ya vita hapo....wakae tu wayamalize kikubwa...qatar airways ishaathirika sana imeanza kupaki ndege sasa
 
wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,792
2,000
Ndilo hilo mkuu, mambo mengine ni gheresha tu - tatizo Ufalme wa Saudia hautaki raia wake waelezwe ukweli kuhusu utawala wao, wanaogopa sana kuondolewa madarakani kwa nguvu za umma/color revolution wako paranoid kweli kweli - wanataka raia wao wabaki mbumbubu kwa kusikiliza Kituo chao cha TV i.e Al Arabia (sijui kama nimepatia jina) kituo hicho kinatumika kutukuza utawala wa Ufalme na kuchochea nchi za Kiarabu zichukie IRAN - yaani Ufalme wa Saudi Arabia unajifanya ni semi Super Power wa Mashariki ya Kati - cha ajabu pamoja na silaha zao za kisasa bado waasi wa Yemen wanawapeleka puta karibu mwaka unakatika bila mafaniko yoyote, leo hii ndiyo wajitape kwamba wanaweza kupigana na IRAN - naona hizo ni ndoto za mchana.
Ndilo hilo mkuu, mambo mengine ni gheresha tu - tatizo Ufalme wa Saudia hautaki raia wake waelezwe ukweli kuhusu utawala wao, wanaogopa sana kuondolewa madarakani kwa nguvu za umma/color revolution wako paranoid kweli kweli - wanataka raia wao wabaki mbumbubu kwa kusikiliza Kituo chao cha TV i.e Al Arabia (sijui kama nimepatia jina) kituo hicho kinatumika kutukuza utawala wa Ufalme na kuchochea nchi za Kiarabu zichukie IRAN - yaani Ufalme wa Saudi Arabia unajifanya ni semi Super Power wa Mashariki ya Kati - cha ajabu pamoja na silaha zao za kisasa bado waasi wa Yemen wanawapeleka puta karibu mwaka unakatika bila mafaniko yoyote, leo hii ndiyo wajitape kwamba wanaweza kupigana na IRAN - naona hizo ni ndoto za mchana.
Kiboko cha Iran ni Israel pekee, Saudia hawezi kupigana na Iran, atapigwa hadi Saudia yote ipinduliwe labda asaidiwe na Marekani.
 
inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
6,211
2,000
Eti wana demand na military base ya uturuki ifungwe iliyo qatar, yani sidhani kama qatar atakubari
hao,mume wao marekani alitaka kuuza silaha kwa qatar tu,manake baada ya show ya urusi syria kila mtu anataman silaha zake,sasa mume kishauza muda si mrefu kila kitu kitakua poa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom