Matabaka yanavyoitafuna CHADEMA na kuvuruga Ustawi wa chama chetu

Matabaka yanavyoitafuna CHADEMA na kuvuruga Ustawi wa chama chetu

chagu wa malunde,

Wakafanyie creative segerea?
Hata katibu mkuu angekuwa ni Dr Slaa kwa sasa na yy angepwaya tu, mambo yamebadilika sio kama wakati huo,

Zaman kuna mtu alikuwa anaweza kumshika maalim seif? Mbona leo anapelekwa police kila siku
 
chagu wa malunde,
CHADEMA YA SLAA NDIO IMETUPATIA CCM IMARA YA MAFUFULI. VINGINEVYO MAFISADI , WAUZA UNGA NA WAPENDA NGONO WANGECHUKUA UONGOZI WA NCHI
 
CHADEMA haipo salama hata kidogo kutokana na kuwepo kwa matabaka ndani ya chama hicho yana wakatisha tamaa wanachama wa chini wenye mapenzi ya dhati na chama hicho. Ni ajabu sana kuona ndani ya chama kimoja kunakua na matabaka zaidi ya saba.

Tabaka la viongozi wakuu akiwamo Mwenyekiti Mbowe wao kazi yao ni kuzunguka na ndege kwenda kula raha kwenye mataifa mbalimbali bila ya kueleza lengo la ziara, matumizi na faida ya safari kwa chama.

Makundi mengine ni viongozi wa Kanda, Mabaraza, Mameya na Wabunge, Wajumbe wa kuchaguliwa, Sekretarieti, na wale wenye kazi isiyojulikana. Kwaujumla, makundi haya yote niliyoyataja ni miongoni mwa wapiga dili ndani ya CHADEMA wasiozoeleka kirahisi.

Kundi la mwisho ni la wale kajamba nani, yaani pangu pakavu tia mchuzi. Kundi hili ndio kubwa sana ukilinganisha na mengine. Hawa ndio wanaolipa michango ya uanachama na fedha hizo ndizo hutumiwa na wavimba matumbo.

Kundi hili la daraja la mwisho, ndio lina kazi ya kuyavusha makundi mengine. Pia hujulikana kama bendera fuata upepo yaani wakiambiwa waandamane huandamana, hukanyagana na kuuana wenyewe kwa wenyewe huku waliowaambia waandamane wakiwa na familia zao nyumbani wakila kuku.
 
Hapana Mkuu, Sidhani kama kuna matabaka, ila nionacho mimi CCM wameona ngome ya CHADEMA ipo Arusha kwa sana sana, ikifuatiwa na Moshi.

Hivyo wanajaribu kuivuruga kwa gharama yoyote ile. Ni wazi kuwa uenyekiti wa kanda ya kaskazini kati ya Lema na Selasini unadhani ninani mzalendo wa chama kati ya hao wawili angepewa?

Lema amekuwa mtu mpiganaji sana wa chama, amesulubiwa kwa sababu ya chama lakini zaidi Lema anaendesha siasa ngumu za uharakati, ili hali mzee Selasini ni mwenye siasa nyepesi.

Kwa wakati huu tunahitaji sana siasa ngumu na ndiyo maana lema alipita, zaidi sana CHADEMA ni ya siasa ngumu za uharakati, siasa zenye kujitoa kwa hali zote, sasa wanachama wenye siasa nyepesi ndiyo ambao kwao inakuwa rahisi sana kuwaattack wakacease.

Na hao ndio wanaotuangusha sana wakirubuniwa kidogo tu wanarudi nyuma. Na hao ndio wanaotengeneza matabaka.
 
Vipi kuhusu CCM, tuletee nao matabaka Yao 12 tuone Nani dhaifu zaidi japo wote dhaifu

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
Wewe ni wakuonea huruma sababu hajitambuwi

Ungefikiria zaidi yafuatayo

1. Ukosefu wa ajira kwa ndugu na jamaa zako na watanzania kwa ujumla

2. Kupotea ama kuathilika mazao muhimu ya biashara kunavyo athili uchumi wa Taifa
Kahawa
Pamba
Tumbaku
Korosho
Asali no

3. Ubora wa Elimu na ubunifu nini mkakati wa Taifa katika uzalishaji wa Elimu bora.

4. Mahitaji ya katiba mpya bora ya Warioba

5. Tume huru ya uchaguzi

Nknk

Badala yake unaleta propaganda, unafiki ......

Haitakusaidia wewe mwenyewe
Watoto wako
Ndugu zako
Taifa la Tanzania

Jitafakari.
 
Ringo Malisa,
Sisi waona mbali, tuliona mbali siku nyingi na tukashauri, tukaishia kubezwa!, sasa na akina nyinyi pangu pakavu sasa ndio mnaanza kuyaona!.


P
 
Sisi waona mbali, tuliona mbali siku nyingi na tukashauri, tukaishia kubezwa!, sasa na akina nyinyi pangu pakavu sasa ndio mnaanza kuyaona!.

P

Tatizo mnaona matawi lakini nyote mnafahamu mzizi wa matatizo ni pale Lumumba na fitna zote hupikwa pale.

Kuijadili Chadema ni rahisi sana sababu mnauhakika wa usalama wenu bila kupotezwa wala kutekwa

Na kujadili mzizi hamuwezi isipokuwa kulalamikia yule ambaye kwenu mnyonge bila kujishughulisha na chanzo halisi cha tatizo

Mkuu tusadie kumkwamuwa Kabendera kwanza. Mliko mchomekea Mungu atalipa tu.
 
Huna ushahidi kama wananunuliwa. Wao wanaridhika na utendaji wa JPM unataka uwalazimishe wabaki huko?
aisee kumbe wanaridhika na utendaji wa JPM ila huwa wanasubiri mpk katibu mkuu afanye ziara ndio wahamie, vipi katibu mkuu asipofanya ziara itakuaje?! na kwann wakija huko mnawarudishia vyeo vyao, kwani huko CCM hakuma watu wakugombea? kama sio makubaliano ya mkataba mnaoingia nao kbl hawajahama ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom