Albert Einstein
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 394
- 583
CHADEMA haipo salama hata kidogo kutokana na kuwepo kwa matabaka ndani ya chama hicho yana wakatisha tamaa wanachama wa chini wenye mapenzi ya dhati na chama hicho. Ni ajabu sana kuona ndani ya chama kimoja kunakua na matabaka zaidi ya saba.
Tabaka la viongozi wakuu akiwamo Mwenyekiti Mbowe wao kazi yao ni kuzunguka na ndege kwenda kula raha kwenye mataifa mbalimbali bila ya kueleza lengo la ziara, matumizi na faida ya safari kwa chama.
Makundi mengine ni viongozi wa Kanda, Mabaraza, Mameya na Wabunge, Wajumbe wa kuchaguliwa, Sekretarieti, na wale wenye kazi isiyojulikana. Kwaujumla, makundi haya yote niliyoyataja ni miongoni mwa wapiga dili ndani ya CHADEMA wasiozoeleka kirahisi.
Kundi la mwisho ni la wale kajamba nani, yaani pangu pakavu tia mchuzi. Kundi hili ndio kubwa sana ukilinganisha na mengine. Hawa ndio wanaolipa michango ya uanachama na fedha hizo ndizo hutumiwa na wavimba matumbo.
Kundi hili la daraja la mwisho, ndio lina kazi ya kuyavusha makundi mengine. Pia hujulikana kama bendera fuata upepo yaani wakiambiwa waandamane huandamana, hukanyagana na kuuana wenyewe kwa wenyewe huku waliowaambia waandamane wakiwa na familia zao nyumbani wakila kuku.
Morely John,
Mwanachama, Chadema,
Moshi.