Mkuu hii kitu ni kweli na kila mtu anajua.
Wakati wa kuformulate maazimio spika alisikika mara kwa mara akirudia kuwa hataki kugombana na mhimili mwingine kwani tayari kishagombana na mhimili mmoja.
Suala hili alirudia mara kadhaa na hata kushambulia wabunge kuwa shida yake amekwishasema hataki kugombana na huo muhimili ambao ni serikali. Nitakuwa spika gani mimi kugombana na mihimili yote??? aling'aka Anna.
HOJA: Iweje kama bunge limefanya kazi nzuri na kugundua wezi wa mali ya umma, spika Anna hata baada ya kujiridhisha kuwa kazi ya PAC ni nzuri na mapendekezo ya wabunge na BUNGE kwa ujumla ni mazuri bado ahangaike namna ya kuandika maazimio? illikuwa ni wazi kuwa BUNGE limeazimia RAIS awafukuze kazi Mhungo, Werema, Tibaijuka na Maswi.
Kigugumizi cha kuandika maneno hayo straight ni Spika kuogopa kuuambia muhimili wa serikali ukweli kwa maneno bayana. Woga huo unatokana na ama Makinda kutoiamini Serikali hivyo RAIS kuwa atasimama na watanzania na bunge lake inapofika ukweli na masuala makubwa ya nchi, kigugumizi hicho ndo kinaonesha kuwa Anna hana imani na RAIS. Ama Anna hana uwezo wa kuwa spika, yuko pale kujaza nafasi sio mtu mwenye uwezo na sifa za kuongoza bunge.
Hofu ya namna ya kuandika ukweli eti rais asigombane naye ni kumzalilisha rais na kuwambia watz kuwa rais wenu ama hana uwezo wa kutambua makosa kama ambavyo bunge limetambua makosa ya kina Tibaijuka, Werema, Muhongo na Maswi kisha bodi ya TANESCO.
HOfu ya Anna ni fedheha kwa BUNGE maana lilipaswa kuchambua na kuweka maazimio jinsi hali halisi ilivyo, kwa maneno yake hayo, iwapo kwa sababu moja ama nyingine rais hatawachukulia hatua hao watajwa, Anna atakuwa amethbitisha hofu yake kwa rais, na atakuwa ameonesha udhaifu wa rais kwa vitendo.
Je hali ya spika kutoamini mihimili mingine au hali ya spika kutokuwa na uwezo wa kumudu kiti cha spika, inalitafuna vipi bunge na hivyo nchi???
Je ilikuwa haki wezi nao wajadili formulations za maazimio ya bunge kwa akili ya kawaida??? Spika kuonesha wasiwasi kwa Rais, ni afya kwa nchi?
Nawasilisha.
Spika alisema bungeni kuwa siku zote mawaziri walipofanya makosa walijiuzulu na ikawa kazi nyepesi tofauti na hawa tunaotaka wawajibike leo. Hawa wamegoma. Je, watanzania wanajua kwanini hawa wamegoma?
1.Maswi ambae ni Katibu mkuu ni kachero anapiga dili na familia ya rais kupitia mkwe wa J.Kikwete Albert Marwa alomuoa mtoto wa Kikwete. Ni kupitia dili za Albert Marwa, Maswi amekuwa karibu na Ridhwani Kikwete. Na ni mtandao huo wa familia unaomiliki asilimia50% za kampuni ya PAP kwa kushirikiana na Singasinga.
Maswi ni mtu muhimu sana kwa familia ya rais na ndio sababu ndani ya Bunge na vikao vya wabunge wa CCM mtoto wa rais Ridhwan alidiriki kusema haamini kama kuchukua hatua ni kumsaidia rais bali kuwalinda wahusika ndio kukisaidia chama na rais. Hayo aliyasema akipinga kauli ya makam wa CCM Mzee Philip Mangula ambae yeye pamoja na Kinana misimamo yao iko wazi kuwa wahusika wawajibike.
Mazingira haya ambayo dili limepigwa kwa maelekezo ya Ikulu na ushiriki wa familia ya rais ndio msingi wa ugumu wa jambo hili hata kuifanya nchi ivuje damu kwa mateso ya kibajeti kutokana na vikwazo vya wahisani.
Ni ugumu huu uliosababisha Jakaya Kikwete kutamani kuvunja kabisa uhusiano wake na Ulaya na Marekani kwani kuchukua hatua katika hili kwake ni sawa na akate tawi la mti alokalia.
Maswi amesikika mara kadhaa akiwambia wajumbe wa kamati ya Nishati kuwa hakuna wa kumtoa nafasi yake nchi hii labda bada ya Jakaya Kikwete. Na ridhwan anasema hakuna wa kumtoa Maswi labda asiwepo.
Ugumu wa kumtoa Maswi ndio unasababisha ugumu wa kumtoa Waziri kwani huwezi kumtoa waziri peke yake kwa makosa ambayo kwa kiasi kikubwa yamefanywa na Katibu Mkuu kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambae nae anajitetea kuwa ilikua maagizo ya Ikulu.
Waziri mkuu nae anagoma kujiuzulu ingawa kosa ni kubwa kuliko la richmond kwasababu watendaji wa chini yake wanamzidi nguvu kutokana na familia ya rais kiasi cha kumfanya abaki kama boya.
Mungu akulinde sana mkuu .Wizara ya madini na nishati ndiko ambako biashara za Riz1 ziliko. Ana vitalu kadhaa vya utafiti wa dhahabu Musoma, maeneo ya Mrangi. Lakini pia Riz1 anashughulika na biashara ya mafuta. Sielewi ukaribu wa Kikwete/Riz1 na Muhongo lakini Riz1 yupo karibu sana na Masele. Na wengi wanasema Masele pamoja na kushindwa kwenye uchaguzi, Kikwete alinishinikiza atangazwe kuwa ameshinda, akatangazwa kuwa alishinda kwa kura 1.
Baadaye alimteua kuwa naibu waziri wa madini ili kulinda maslahi ya Riz1.