Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu: Gesi ya Mtwara - Pinda afanya Live Briefing Bungeni!

Jibu: Pinda "inawezekana kuwa kweli, ila vyama vya siasa pia vimechangia!, sasa tusitafute mchawi, tusonge mbele. Ushirikishwaji wa jamii!.

La mikataba, tutajielekeza, ila tufuate taratibu!.

Mbowe anauliza swali la nyongeza, na kumbana PM awe firm, mikataba iwe firm mikataba iwekwe wazi?

Pia amemtaka PM kukiri kuwa serikali inakuwa sikivu baada ya pressure zikiwemo maandamano?.

Sikio la kufa halisikii dawa, CCM wanaendesha nchi kwa kauli za uwongo! sasa Nchimbi anasema waliochochea vurugu za Mtwara watawajibishwa, halafu waziri mkuu anasema tusitafute mchawi, sasa wale wote waliokamatwa na kuwekwa ndani kwasababu ya hizo vurugu waachiliwe huru maana walikuwa misled na serikali ya CCM na viongozi wake kwa "kutokutoa taarifa sahihi kuhusu mradi wa gesi Mtwara" kama kuna ukweli wowote au wamejipindua kama mbayuwayu!
 
JIBU: PM, swali la Mbowe halina mashiko, serikali haifanyi kazi kwa mashinikizo, maandamano sio njia muafaka haswa yanapokuwa off hand!.

Hilo la kuweka wazi mikataba, kuna taratibu za kibunge kuliwezesha bunge kuomba mikataba yoyote kupitia ofisi ya spika ila mikataba nayo inayo masharti yake likiwemo la usiri, hivyo sio kuianika wazi magazetini!.

P.
Tunajua hakika serikali "Pinda" Kwalaghai wana mtwara...Kuwa wataalamu wake wamesema gesi haiwezekani kusafilishwa ikiwa haijawa process...Tunajua inawezekana...kabisa...ila tu ilikuwa ni kuwatuliza munkali wana mtwara.
 
The devil lies in the details, kwa nini wanakwepa kuweka mikataba wazi, tuone ufisadi na failure ya policies zao kwenye hiyo mikataba.

Hivi kwanza kunawezaje kuwa na Mkataba bila kuwepo sera ambayo ndo inatoa muongozo wa maslahi ya nchi katika uchimbaji wa gesi huo mkataba unabeba maslahi ya nani? Hili bunge letu ni dhaifu na la kipuuzi! Haliwezi kuisimamia serikali wala maslahi ya nchi! Inatia hasira sana!
 
Hivi kwanza kunawezaje kuwa na Mkataba bila kuwepo sera ambayo ndo inatoa muongozo wa maslahi ya nchi katika uchimbaji wa gesi huo mkataba unabeba maslahi ya nani? Hili bunge letu ni dhaifu na la kipuuzi! Haliwezi kuisimamia serikali wala maslahi ya nchi! Inatia hasira sana!

Dah! Yaani umeongea pointi mwana! Serikali ijibu hoja hizi. Mbona mchawi ni serikali yenyewe na mafisadi waliopo ndani yake?
 
Ili la serikali kufanya siri mikataba ya taifa ni tatizo bunge linatakiwa kujua mikataba yote ya serikali. Bunge ndiyo chombo kinachotuwakilisha sisi wananchi.
Like ya Kwanza Kwako na pia ungeongozea hiyo mkataba ichambuliwe kwanza na wasomi wenye uchungu na nchi ndipo isainiwe na hiyo iliyosainiwe kama ni mibovu ifutwe na iandikwe upya kwa manufaa ya wananchi tukiende hivi miaka michache tutakuwa nchi tajiri kama Mwenyezi aliyetupa hizi Mali zitufaidishe sote na si wachache
 
JIBU:Hilo la kuweka wazi mikataba, kuna taratibu za kibunge kuliwezesha bunge kuomba mikataba yoyote kupitia ofisi ya spika ila mikataba nayo inayo masharti yake likiwemo la usiri, hivyo sio kuianika wazi magazetini!.P.
hii inaonyesha wazi kuwa pm pamoja na kuwa na facilities za kisasa kumsaidia kujua kinachoendelea kwenye sayari ya dunia na washauri wa kutosha, inaelekea bado anang'ang'ania mawzo yale yaliyotufanya kuwa na matatizo tuliyonayo leo.
Mwizi au mhalifu yeyote daima hapendi ajulikane anachofanya! Kwani mkataba wa RICHMOND (?) ulivyowekwa hapa jf kuna mtu yeyote mwema serikalini aliyeathirika kwa hari yoyote?? Lakini si ilisaidia kujua undani wa kilichotokea na leo hii kuna Watanzania wengi tu ambao wanajua njia hata zaidi ya tatu za kutatua matatizo na kinachowakwamisha ni kupewa hiyo opportunity ya kuonyesha uwezo wao ambayo mara nyingi tunaambiwa tusubiri na Mtwara ndio hao wamechoka kusubiri
 
Kama kweli hili la gesi limekwisha na SERIKLI imeridhia huo mtambo ujengwe Mtwara basi ningewashauri Prof. Mhongo na Simbachawene waachie ofisi kwa kumshauri Mh Rais vibaya na kushindwa kusikiliza hoja za wananchi badala yake wakaongozwa na jazba na kuwatusi wananchi wa Mtwara.......
 
PM hajawa mkweli.

Makampuni mengi, hasa yaliyo kwenye sekta ya nishati na madini wanataka sana mikataba iwe wazi. Na hii ni kwa sababu huko wanakotoka wanatakiwa wawe transparent. Lakini kwa sababu wanazojua wenyewe wakubwa wa CCM wamekuwa wanang'ang'ania mikataba iwe siri. Kwa hili watanzania tunaingizwa mjini mchana kweupe. Na nadhani mikakati ya kudai uwazi wa mikataba sasa ujumuishe wanaharakati wa nchi zilizotoka haya makampuni. Mfano kuna makampuni toka Norway na UK. Wanaharakati wa Tanzania waanze kuwahusisha asasi za huko ili makampuni hayo yaweke mambo hadharani. Kuna ulaghai mkubwa kwenye hii mikataba.

Na huko tuendako, mikataba yote lazima ijulikane kwa jamii inayozunguka hizo rasilimali. Haiwezekani, kwa mfano, uchimbe Tanzanite, lakini wananchi wa Mererani hawajui chochote kuhusu mkataba wa uchimbaji madini? Hii ni fedheha na viongozi wetu waone aibu ya kutetea hii fedheha. Waafrica tunadharauliwa kwa upuuzi wa namna hii, tunatumia nguvu kubwa kufunika wizi wakati huo huo tunazidi kuomba chakula toka kwa mtu tuliyomruhusu atuibie! Very wrong.

CCM ni janga la kitaifa.tusipo ungana kuli-angamiza yata uzwa mpaka makaburi.
 
Ili la serikali kufanya siri mikataba ya taifa ni tatizo bunge linatakiwa kujua mikataba yote ya serikali. Bunge ndiyo chombo kinachotuwakilisha sisi wananchi.

Kuanzia nikujue leo ndio umeongea point ngoja nikugongee like naona ile roho yako ya kutetea ugamba kwa kila jambo imekutoka au umefukuzwa lumumba?isije ikiwa umevuliwa gamba au hujapewa posho nn? Ok bado ndugu yako chama.big up kwa hili ndugu yangu
 
Linaonyeshwa kwenye TV na Radio pia, tatizo Watanzania wengi hawana vingamuzi.

Umesema kweli kabisa Mh RTZ,BIGup. Maisha bora kwa kila mTZ/mfanyakazi bado ni ndoto.Ni vema tuamke maana ndoto hii haina mwisho (vinginevyo tutalala milele).
 
Kuanzia nikujue leo ndio umeongea point ngoja nikugongee like naona ile roho yako ya kutetea ugamba kwa kila jambo imekutoka au umefukuzwa lumumba?isije ikiwa umevuliwa gamba au hujapewa posho nn? Ok bado ndugu yako chama.big up kwa hili ndugu yangu

BIG UP Saaaaaaaana Kwa RTZ,ndo tunanata awe hivyo VERRY GOOD.
 
Back
Top Bottom