Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Mkono alijenga uhasama dhidi ya muhongo baada ya prof kugundua janja ya mkono na mawakili wake kuipa ushauri mbovu tanesco ili kesi ziwe endelevu na aingize mabilioni,muhongo alitoa kampuni ya uwakili ya mkono kuwa wakili wa tanesco,mkono akajenga kisasi ndo akala deal na kina kafulila kuanzisha kashifa ya escrow
 
Suala la umiliki wa fedha za escrow halina utata
Kumekuwapo na mchezo mchafu wa kisiasa wa kujaribu kupotosha ukweli kuhusu umiliki wa fedha zilizokuwapo katika akaunti ya escrow iliyojulikana kama Tegeta Escrow.
Ili kuelewa kwamba fedha katika akaunti hiyo zilikuwa zitaendelea kuwa ni za IPTL na kamwe hazijawahi kuwa za Tanesco wala Serikali ni muhimu kutambua ukweli tu kwamba mlipaji wa deni hawezi kuwa mmiliki wa deni analolilipa.
Akaunti ya Escrow ilifunguliwa kutokana na ushauri wa Mkono & Co. Advocates wa mwaka 2004 ambao walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme zilizokokotolewa kwa kutumia asilimia 22.31 ya urejeshwaji wa uwekezaji {IRR} zilikuwa hazikubaliki na hivyo Tanesco walikuwa wakitoa hati ya kupinga malipo kwa kila ankara ya malipo kupinga gharama hiyo kulingana na kifungu Na.6.8 cha mkataba wa ununuzi wa umeme {PPA}. Kifungu hicho kinaeleza kuwa ikiwa upande wowote haukubaliani na usahihi wa malipo katika ankara zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo ya gharama za umeme wanatakiwa watoe notisi {Invoice Dispute Notice} kwa upande mwingine.
Vile vile, mawakili wa Tanesco Mkono & Co. Advocates waliishauri kwamba kutokana na pingamizi hilo, ifunguliwe akaunti maalum {Escrow Account} kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zilitokana na ankara zilizokuwa zinapingwa.
Ushauri huo ulitekelezwa na Tanesco na mnamo Julai 5, 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mkataba wa kufungua akaunti maalum kwa ajili ya kuweka fedha zote za ankara zilizopaswa kulipwa kwa IPTL.
Kwa mantiki hiyo Akaunti ya Escrow ilifunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya IPTL yaliyokuwa yakisubiri kuthibitishwa na Tanesco kwa pamoja na IPTL kwa pamoja kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 6.8 cha mkataba wa ununuzi wa umeme yaani PPA.
Kwa mantiki hiyo basi ni vema ikafahamika na kueleweka kuwa fedha hizo zilikuwa za IPTL na wala siyo fedha za Serikali wala si za Tanesco.
Ni wazi pia kutambua kwamba wahusika walikuwa na uhuru wa kuweka fedha hizo katika akaunti nyingine yoyote kutegemea na makubaliano yao yaani ya IPTL na Tanesco.
Hivyo basi kitendo cha fedha hizo kuhifadhiwa katika akaunti iliyofunguliwa na kuhifadhiwa katika Benki Kuu haina maana kuwa fedha hizo zilikuwa za Serikali.
Kwa mujibu wa kifungu namba 7.7 cha mkataba wa Akaunti hiyo ya Escrow fedha zilizomo kwenye akaunti hiyo zingeendelea kuhifadhiwa na Wakala wa Escrow {Escrow Agent}, hadi muafaka utakapofikiwa kati ya Tanesco na IPTL kuhusiana na mabishano ya ankara.
Kwa mujibu wa mkataba wa escrow, Benki Kuu ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia na kuendesha akaunti ya Escrow hadi hapo Tanesco na IPTL watakapofikia muafaka na akaunti kufungwa.
Baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliotolewa na Jaji Utamwa wa kuiondoa IPTL kwenye ufilisi na kuitambua PAP kama mmiliki wa asilimia 100 wa IPTL, Tanesco ilifanya mazungumzo na IPTL na kukubaliana na kiasi ambacho Tanesco ilikuwa inadaiwa na IPTL.
Baada ya makubaliano kati ya Tanesco na IPTL serikali ilisaini makubaliano na IPTL kuruhusu fedha za akaunti ya Escrow zilipwe kwa IPTL na Benki Kuu ikaagizwa kuzilipa fedha hizo na hatimaye kuifunga akaunti hiyo.
Oktoba 21, 2013 Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na IPTL walisaini makubaliano ya kutoa fedha zilizomo katika akaunti ya Escrow ili zilipwe kwa IPTL. Makubaliano hayo yaliyojulikana kama Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited yaliambatana na muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya IPTL na Tanesco pamoja na barua ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwasilisha makubaliano hayo na kuiomba Benki Kuu iruhusu malipo hayo kwenda IPTL kama uhakiki ulivyobainisha, na kwa vile matakwa ya kifungu 7.7 cha mkataba wa Akaunti ya Escrow unavyosema yalikuwa yametekelezwa kikamilifu.
Kufuatia maombi ya Benki Kuu kwenda Wizara ya Fedha ya kufunga akaunti ya Escrow kutokana na kumalizika kwa mgogoro kuhusu mali ya uwekezaji na kwa kuzingatia uamuzi wa Mahakama Kuu, mwezi Desemba 2013 akaunti hiyo ya Escrow ilifungwa rasmi.
Wakati wa kufunga akaunti hiyo ya Escrow, Tanesco ilikuwa ikidaiwa na IPTL jumla ya dola za Marekani milioni 79.05 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 125.04 zilizotokana na tozo ya uzalishaji {capacity charges} ambazo hazijalipwa. Kimsingi fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow wakati wa kuilipa IPTL na kufunga akaunti hiyo zilikuwa kidogo kuliko madai ya IPTL.
Ikumbukwe kwamba kuanzia Septemba 2009 Tanesco iliacha kulipa fedha za tozo ya uzalishaji umeme {capacity charges} kwenye akaunti ya Escrow kwa sababu ya ukata wa TANESCO/ Serikali.
 

malizia na hili....
na amesaidia sana KUKIBORESHA CHAMA na kukiongezea mvuto huku akiongeza IMANI YA WANANCHI kwa CCM NA SERIKALI YAKE. CCM oyee!
 

umemjibu vizuri sana mkuu maana huyu kiroboto FaizaFoxy ni mgumu sana wa kuelewa.

msingi wa maazimio yale ulijengwa kwenye msingi kwamba zile zilikuwa fedha za UMMA, sasa kwa kuwa rais anasema SIO FEDHA ZA UMMA, maana yake ni kwamba HAKUNA KESI. ni nini kinachochunguzwa zaidi kama sio kuzidi kuchezea fedha za UMMA?
 
Last edited by a moderator:

sasa kama rais yuko sahihi ni nini kinachunguzwa zaidi? Wewe mwehu nini?
 
Daima maji hufuata mkondo,ndio maana uchaguzi wenye RUSHWA huzaa Serikali ya wala RUSHWA,CCM isiyoshinda kihalali inakosa BARAKA ZA MOLA WETU.MUNGU ni MTAKATIFU na hivyo hawezi kuibariki serikali inayoiba na kutembea kifua mbele ikijisifia kwa wizi iliyoufanya,ndio maana CCM imejaza wezi watupu,ambao hawataki kufanya kazi na hivyo kuelekeza nchi kuwa ombaomba,mpaka mataifa ya wenzetu yanatushangaa na rasilimali zote tulizonazo,Rais mzururaji ameamua kuwa Vasco da Gama,sindibad the sailor.Wenzetu wanatoza wananchi wao kodi kutufadhili sisi,kibaya zaidi baadhi ya mawaziri kama akina Pombe Magufuli wanasema eti mwacheni Rais azulule atutafutie fedha kumbuka hayo maneno yanatoka kwenye mdomo wa Doctor sasa jiulize kuna Elimu kwenye kichwa cha namna hiyo kama sio upumbavu na janga kwa Taifa.Tukumbuke kwamba kuombaomba na kutegemea misaada ni UTUMWA na FEDHEHA KWA TAIFA.Wengine kama akina Andrew Chenge na Willam Ngeleja kila dili wamo nadhani hata mshipa wa AIBU Ulishakufa wanataka hadi vitukuu vijue kuwa wao ni wezi konkodi.MAWAZIRI wengine wanaoitwa maprofesa wanasema eti watanzania wanaweza kuwekeza kwenye juisi peke yake na siyo gesi,anatamka hivyo baada ya kulewa madaraka na kujisahau kwamba anatumikia ofisi ya UMMA na UMMA ndio uliomtuma kazi anayofanya kama waziri wa nishati na madini na si kutoa matusi kwa watanzania.Kumbe watanzania tusishangae haya yanayoendelea na matunda ya namna serikali ilivyopatikana.Wengine wakajiita maspika wa standard and speed kumbe ni vichaa tu,walishachanganyikiwa zamani.Tunaisihi CCM na serikali yake isichezee AKILI ZA WATU WENYE MAARIFA.Ndugu zangu watanzania tujifunze hasa tunapokuwa kwenye OFISI ZA UMMA kuwatumikia watanzania wenzetu maskini na kuacha majigambo,majivuno,dharau,kejeli,matusi ili kuwatumikia watanzania kwa upendo mkuu bila kujali rangi,kabila wala dini ya mtu.
 
sasa kama rais yuko sahihi ni nini kinachunguzwa zaidi? Wewe mwehu nini?
Punguza hasira na twende taratibu,kunapotolewa shutuma kama hizi za wizi,lazima ziwepo chunguza kama njia ya kujiridhisha.palipo na uchunguzi haina maana kwamba patapatikana makosa.
sasa kama bunge lilikua na hakika kuwa ni fedha za umma na zimeibiwa kwanini azimio namba 3 linataka pawepo uchunguzi?.
pia yataka ukubali tu kwamba bunge lilitawaliwa na mihemko ya kisiasa na kutokua na information sahihi baadhi ya maazimio yako kimhemko zaidi kuliko common sense .lakini pia suala la miamala ya mkombozi bank vilevile linataka uchunguzi na ndo maana ya kuwepo uchunguzi.
 
Siyo kajiudhuru ni kajiuzulu. Siyo kujiudhuru ni kujiuzulu na siyo akaamuwa ni akaamua.


Wewe ukikaa na wenzako na ukishikwa na haja inayokubidi uwawache huwa unatoa uzulu au udhuru?.

Wakati unajishauri hilo ka mwanzo hebu sema kwa sauti "akaamua".

See how stupid you are? Akaamuwa ndiyo sahihi.
 
hizo za bomba la gesi na sukari zitawapunguzia sana ccm kura 2015, hiki chama kitakufa mbele ya m/kiti wao.
 
Ajuza kuwa na udhuru na kujiuzulu ni vitu viwili tofauti acha kuonyesha upumbavu wako hadharani. Kama hujui uliza badala ya kujifanya unajua kila kitu.


Wewe ukikaa na wenzako na ukishikwa na haja inayokubidi uwawache huwa unatoa uzulu au udhuru?.

Wakati unajishauri hilo ka mwanzo hebu sema kwa sauti "akaamua".

See how stupid you are? Akaamuwa ndiyo sahihi.
 

Wrong!mgogoro ulihusu iptl na tanesco kwa ajili ya capacity charges..ndo ikafunguliwa ac ya escrow BOT mpaka watakapokubaliana!swala la VP eng..aliyekuwa na30%ya hisa alienda mahakamani kublock ac za PAPakiwa ndo mmiliki wa 70%ya hisa zaiptl ili ashinikize alipwe 30%ya hisa zake baada ya kujua kuwa pesa zishatolewa kwenye ac ya escroe BOT!....usipotoshe watu!
 
Ajuza kuwa na udhuru na kujiuzulu ni vitu viwili tofauti acha kuonyesha upumbavu wako hadharani. Kama hujui uliza badala ya kujifanya unajua kila kitu.


Huyo ajuza atakuharibia siku mkuu, mwambie shigongo anatafuta proof reader. Sio jf. Pia hakawii kukuambia tatizo ni dini yako.
 
Reactions: BAK

Nimeelewa,kwa hiyo Mh Muhongo sio jasiri ndio maana kakataa kujiuzulu,pia aliemteua sio jasiri ndio maana kamuweka kiporo
 
Ajuza kuwa na udhuru na kujiuzulu ni vitu viwili tofauti acha kuonyesha upumbavu wako hadharani. Kama hujui uliza badala ya kujifanya unajua kila kitu.


Mmevifanya kuwa viwili tofauti kwa kutokujuwa kwenu Kiswahili fasaha na chimbuko la maneno.

"uzulu" ni simply broken udhuru ambayo mimi siikubali mpaka leo na hata useme nini. "Uzulu" si Kiswahili fasaha, kujiudhuru ni kutoa udhuru kama alivyofanya Werema, kajiudhuru kuwachia wadhifa wake kama AG.
 
Nimeelewa,kwa hiyo Mh Muhongo sio jasiri ndio maana kakataa kujiuzulu,pia aliemteua sio jasiri ndio maana kamuweka kiporo

Mhongo hakutowa maamuzi yoyote na wala hakuombwa maoni kuhusu utoaji wa fedha za escrow, yeye au kupitia katibu mkuu wake aliomba maelekezo ya kisheria kutoka kwa Werema, kwanini ajiudhuru kwa hilo?
 
Bosi wangu wa zamani aliniasa kuwa, Ukitaka kusema uongo mmoja yaani mara moja, inabidi ujifunze kusema uongo mwingine mara mia moja kwa ajili ya kuulinda huo uongo mmoja. Mkulu wetu hayajui hayo.
 

Hilo kutokuwa fedha za umma ni moja lililokuwa halina ufafanuzi wa wazi kutoka kwa AG. Au umesahau inawezekana ikawa za umma na inawezekana ikawa za IPTL?

Kuna maazimio manane unaweza kuyaainisha hapa na ututatulie ulitaka yafanyiwe vipi kazi badala ya alivyoyafanyia Kikwete?

Hapo sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…