Maswali na ushauri kwa Malinzi

..Malinzi habari;
Naomba kufahamu kuhusu suala la uwekaji nyasi bandia kwenye viwanja vya mikoani,uwanja wa kaitaba kwa sasa unawekwa nyasi hizo. Je, kuna mipango yoyote TFF kuendekea kuwekea nyasi bandia na viwanja vingine kama sheikh amri abeid, Jamhuri stadium na vingine.?
#asante!
 
J malinzi usituhadae wadau wa michezo kwa wale wanaotoa rushwa ile sheria feki ya kadi tatu za njano hapo kulikua na rushwa asilimia 100 halafu tff mkajifanya mnaifuta hiyo sheria bila maelezo ya kina inadhihirisha sheria ilikuwa mifukoni.
leo unamtafuta mtoa rushwa usitake kutufanye wadau wajinga swala la rushwa umeshindwa au unamtafuta mnyonge ndio umkamate?
Hakuna kitu ambacho Jamal Malinzi namchukia kama kukubali tff kuwa ya watu fulani, ameifanya kuwa kundi la watu kujitungia sheria na kufanya lolote watakalo.
Kuna kundi la watu kutokana na nguvu yao pale tff walitunga sheria kwa lengo la kuibeba timu fulani, wakatuletea kanuni ya mchezaji mwenye kadi 3 za njano kuomba match ya kuikosa, wewe Jamal Malinzi kutokana na udhaifu wako ukakubali ile kanuni itumike kabla klabu hazijapata barua za kuvijulisha juu ya kanuni hiyo mpya.

Lakini watanzania walipohoji lile wewe kwa ujanja wako kabla ya kutoa majibu ya kwann timu fulani ilipata barua ya kuitarifu juu ya kanuni mpya ya ligi na timu nyingine zikiwa hazina taarifa wewe ukakimbilia kuifuta ile kanuni.!!!

Tff chini ya wewe Jamal Malinzi umeshindwa kutuambia nani alikuwa ameghushi mkataba ktk lile sekeseke la Mchezaji Ramadhan Singano na klabu yake ya zamani ya timu ya Simba.
Yapo mengi sana pale tff yaliyofanywa na hao wanaoiona tff kuwa ni kikundi chao na wewe kutokana na udhaifu wako umeshindwa kuchukuwa hatua yoyote.
 
Bro malinzi hongera sana,kazi inaonekana japo wanao ponda na kukubeza ni wengi,nakusihi usikate tamaa songa mbele,sisi tunaojua kuwa soka halijengwi kwa siku moja tunakuunga mkono usonge mbele bila kupumzika,
Hongera kwa kurudisha kombe la tff lilopotea kwa miaka kumi na tatu na kupata wadhamini,pia hongera kwa kupata wadhamin wa ligi daraja la pili startimes,hongera sana kaka tunategemea hapo badae kuwa na timu strong ya taifa hapo badae isiyo yakubahatisha bahatisha.
 
Ni lini mtampa mkwasa timu ya taifa kama kocha rasmi sio sasa mara yanga na taifa?au kuna plan nyingine ya kuleta kocha mkuu mwingine?
 
Soka letu bado ni la woga hasa kwa vilabu. Hakuna sheria inayowabana viongozi wa vilabu kuwa na maendeleo binafs. Hata ile sheria ya viwanja vya mazoezi imefifia. Inabidi kuvibana vilabu ili viwe na maendeleo binafsi!~
 
Jamal Malinzi mpira sio siasa usiogope kuwaambia ukweli wamiliki wa viwanja vya mikoani ambao ni CCM kuwa vibovu wavilekebishe kwa hadhi ya kuchezea mpira kama hawarekebishi vifutwe mara moja
 
Mhe.Malinzi wakati unagombea urais sera yako kubwa ilikuwa soka la vijana, iliishia wapi hili suala??mikakati ikoje kuhusu timu ya u13?
 
Jamal Malinzi mpira sio siasa usiogope kuwaambia ukweli wamiliki wa viwanja vya mikoani ambao ni CCM kuwa vibovu wavilekebishe kwa hadhi ya kuchezea mpira kama hawarekebishi vifutwe mara moja
Viwanja siyo Vya CCM ni Vya halmashauri CCM walifanya uhuni nakuhakikishia ni swala la muda tu...Tutaanza na uwanja wa sheikh Amri Abeid
 
Malinzi unaonaje mechi official's has a wa mechi ya simba na yanga muqw mnawatoa nje ya Tz ili kuondoa malalamiko na pressure wanazotoa mashabiki wa mpira viwanjan?
 
Jamal Malinzi mpira sio siasa usiogope kuwaambia ukweli wamiliki wa viwanja vya mikoani ambao ni CCM kuwa vibovu wavilekebishe kwa hadhi ya kuchezea mpira kama hawarekebishi vifutwe mara moja
Yaani timu ambazo ndio wanufaikaji hazina viwanja na zina mpaka milioni 500 za kufanya usajili wa sifa, na wewe unakuja kutoa 'fatwah' kuwa CCM ndio ikarabati viwanja vyake yenyewe wanavyotumia watu wengine na wao hata tim hawana?

Elimu, elimu, elimu!
 
Back
Top Bottom