Maswali magumu: Utetezi wa Jakaya Kikwete dhidi ya tuhuma za chuki binafsi dhidi ya Hayati Magufuli msibani

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
JK leo tumekusikia ukijitetea kuwa watu wameanza kuzusha mitandaoni eti wewe ulikuwa unamchukia JPM na pengine ukawa mmoja wa maadui zake wakati wa utawala wake. Majibu yako yalikuwa mepesi mno kama kawaida yako "Mswahili" nanukuu "Eti kama kweli ningekuwa namchukia JPM nisingeweza kupitisha jina lake katika mchakato wa kuwania Urais 2015 kwani mimi (kama Rais na Mwenyekiti wa chama) ndiye niliyepeleka majina matano (5) Halmashauri" na ukaenda mbele zaidi ukasema katika kuchagua majina matano jina la kwanza lilikuwa la JPM alafu yakafuatia mengine manne. Umeenda mbele zaidi na kusema kuwa alikuwa jembe lako katika baraza lako la mawaziri huku ukijikanganya zaidi na kusema mlipokuwa mnatifuana JPM alikimbilia kupeleka mashtaka kwa kaka yako mkubwa ambaye ni marehemu sasa.

Maswali magumu:

(i) Je, kwani wewe ndiye uliyependekeza hayo majina matano au ni CC ya chama chako ndiyo iliketi na kukuletea wewe kwa ajili ya kuyawakilisha Halmashauri? Labda tusaidie kwani hayo majina ulitoka nayo nyumbani kwako kwa kushauriana na familia yako?

(ii) Je, si kweli JPM aliingizwa katika tano bora baada ya kuona "mamvi" hawezi kuaminika katika chama na wananchi wanataka mchapakazi asiyekuwa na doa ili kukikomboa chama kilichokuwa kinaelekea kuanguka na sio kwa mapenzi yako binafsi?

(iii) Hivi mashtaka aliyokuwa anapelekea JPM kwa kaka yako mara kwa mara yalihusu nini kama kweli alikuwa jembe lako katika baraza lako?

(iv) Mwisho japo sio kwa umuhimu. Unajuaje pengine watu wanasema chuki zako dhidi ya JPM zimeanza kuonekana zaidi baada ya yeye kuwa tayari ni "Mkuu" kwa maana ya kuwa hukuwa na jinsi tena ya kubatilisha maamuzi yako?
 
Tuache msiba uishe salama ,msiba ni wetu sote

Majibu kama unayo mkuu yanakutosha wewe
Magufuli alikuwa mtu mtata na amefariki na kuacha utata. Hata siku aliyokufa exactly haijulikani. Watu watata hata wakifa mambo yao hayaishi ghafla kwa hiyo wacha watu wajadili kwa uwazi.

Itachukua muda legacy ya ukweli ya huyu kipenzi cha watu fulani fulani kutulia.
 
Magufuli alikuwa mtu mtata na amefariki na kuacha utata. Hata siku aliyokufa exactly haijulikani. Watu watata hata wakifa mambo yao hayaishi ghafla kwa hiyo wacha watu wajadili kwa uwazi.

Itachukua muda legacy ya ukweli ya huyu kipenzi cha watu fulani fulani kutulia.
Mkuu kwani si tulitangaziwa kuwa Rais alikufa tarehe 17 kama sikosei.
 
Mi sioni sababu ya kuhoji aliyoyaeleza JK, yeye ndiyo kasema JPM alikuwa jembe na rafiki yake hadi akatafutiwa kiwanja Chato, sasa unapopinga na kuhoji unamaanisha nini? Yaani unabishana na mtu anaekuelezea yake ya moyoni mwake!Hii nayo ni habari nyingine sasa mkuu.
 
JK leo tumekusikia ukijitetea kuwa watu wameanza kuzusha mitandaoni eti wewe ulikuwa unamchukia JPM na pengine ukawa mmoja wa maadui zake wakati wa utawala wake. Majibu yako yalikuwa mepesi saana kama kawaida yako "Mswahili" nanukuu "eti kama kweli ningekuwa namchukia JPM nisingeweza kupitisha jina lake katika mchakato wa kuwania Urais 2015 kwani mimi (kama Rais na Mwenyekiti wa chama) ndiye niliyepeleka majina matano (5) Halmashauri" na ukaenda mbele zaidi ukasema katika kuchagua majina matano jina la kwanza lilikuwa la JPM arafu yakafuatia mengine manne. Umeenda mbele zaidi na kusema kuwa alikuwa jembe lako katika baraza lako la mawaziri huku ukajikanganya zaidi na kusema mlipokuwa mnatifuanaJPM alikimbilia kupeleka mashtaka kwa kaka yako mkubwa ambaye ni marehemu sasa

Maswali magumu:

(i) Je, kwani wewe ndiye uliyependekeza hayo majina matano au ni CC ya chama chako ndiyo iliketi na kukuletea wewe kwa ajili ya kuyawakilisha Halmashauri? labda tusaidie kwani hayo majina ulitoka nayo nyumbani kwako kwa kushauriana na familia yako?

(ii) Je, si kweli JPM aliingizwa katika tano bora baada ya kuona mamvi hawezi kuaminika katika chama na wananchi wanataka mchapakazi asiye kuwa na doa ili kukikomboa chama kilichokuwa kinaelekea kuanguka na sio kwa mapenzi yako binafsi?

(iii) Hivi mashtaka aliyokuwa anapelekea JPM kwa kaka yako mara kwa mara yalihusu nini kama kweli alikuwa jembe lako katika baraza lako?
Mkuu acha ushambenga
 
Back
Top Bottom