Wakuu wa JF poleni na majukumu ya kila kukicha katika kuhakikisha taifa hili linasonga mbele hususani katika masuala ya uwazi na uwajibikaji.
Leo ninaleta taarifa mpya kabisa kutoka mamlaka ya mapato(TRA) mkoani Arusha nah ii si nyingine ni kuhusu wasichana wawili ambao ni mapacha na watumishi wa mamlaka hii mkoani hapa.
Mapacha hawa wa kike mmoja anaitwa Carolight Ntinku na mwingine anaitwa Caroline Ntinku,hawa kwa taarifa tulizonazo hawana muda mrefu tangu wapate ajira ndani ya ofisi hii.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko ya chini kwa chini kutoka kwa baadhi ya watumishi wa TRA Arusha kuhusu wasichana hawa na miongoni mwao ni kuhusu suala la upendeleo unaofanyika kwa watu hawa.
Baadhi ya watumishi wanalalamika chini kwa chini sisi tumeamua kuanika wazi sasa kwamba wanapendelewa nafasi za mafunzo kupitia TRA nje ya nchi na taarifa za ndani ni kwamba hivi karibuni wamepata scholarship nje ya nchi kupitia mgongo wa TRA kwenda kusoma .
Baadhi ya watumishi wanadai kwamba wao wana muda mrefu ndani ya ofisi hii na walishajaribu mara kadhaa kuomba nafasi ya kwenda kimasomo nje ya nchi kupitia TRA lakini hawajapata nafasi hizo lakini kwa muda mchache wasichana hawa wamepata nafasi ghafla hali ambayo inaibua mzozo mkubwa.
Kuna taarifa ambazo si rasmi kwamba kuna kigogo wa TRA makao makuu kwenye nafasi ya Human Resource wana undugu naye wa karibu na yeye ndiye amekuwa akihusishwa na mpango wa kuwatengenezea mchongo wasichana hawa.
Kingine ni kuhusu malalamiko kwamba wasichana hawa wamekuwa na kiburi na jeuri ndani ya TRA katika majukumu yao ya kikazi,kwa kuwa wanalindwa na baadhi ya vigogo ndani ya TRA H.Q mwenye ukweli juu ya hili atuletee tuwajue.
Lakini kuna taarifa nyingine zilizozagaa hapa mjini Arusha kuwa wasichana hawa mapacha wamekuwa wanadaiwa kwamba wamekuwa wakitumia vyeo vyao kuwatishia baadhi ya wafanyabiashara kufunga biashara zao,na madai ya kuomba na kupokea rushwa tunaomba TAKUKURU Arusha sasa waingilie kati hili.
Wadau tunaomba mtu yoyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu atumwagie data za wasichana hawa kama ni kweli au la ili tuujue ukweli wa ndani,naamini tutachangia bila jazba kwa lengo la kujenga na si kubomoa,asante tumeweka na picha ya mmoja wa wasichana hao aitwaye caroline
wadau